Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijaelewa ilikuwaje Dar ikawa jiji ilihali haikuwa kuwa Wilaya wala Manispaa?Jiwe alikuwa mwehu yule.
Alikuwa anatafuta gia ya kutaka kukipatia hadhi ya jiji kile kile Kijiji bjs cha Chato.
Alikuwa mshamba na mjinga sana yule jamaa.
Ndiyo Magufuli alifanya Ilala kuwa Jiji then Temeke na Kinondoni zikabaki katika hadhi ya manispaa!hivi kumbe jiji lilikuwa ni ilala peke yake?
Hayo ndiyo maamuzi sahihi CCM acheni kukurupuka katika maamuzi nchi si mali ya kiongozi bali ni mali ya Raia.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, ametoa agizo la haraka kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuhakikisha mchakato wa uanzishwaji wa Jiji la Dar es Salaam unakamilika kabla ya mwaka 2025.
Hivi wadau mnambuka kuwa Rais Magufuli alivunja rasmi halmshauri ya jiji la Dar es salaam na kuipandisha hadhi halmashauri ya Ilala kuwa Jiji, Februari 24, 2021?
==========
Waziri Mchengerwa ametoa agizo hilo Oktoba 24, 2024, wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara katika halmashauri tano za Mkoa wa Dar es Salaam, hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Mwembeyanga, Temeke, mkoani humo.
"Ni lazima Dar es Salaam hii, hapa ndipo makao makuu na kitovu cha biashara... Dar es Salaam hii tukiijenga vyema maana yake taifa letu litaongeza mapato, kodi zitaongezeka, wageni mbalimbali watakuja hapa kuishi na kufanya biashara," amesema Waziri Mchengerwa.
Aidha amesisitiza umuhimu wa kuboresha miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza mapato ya serikali. Ameainisha kwamba ujenzi wa masoko, ukarabati wa barabara, na utekelezaji wa miradi mingine mikubwa ya maendeleo unaolenga kuboresha hali ya miundombinu ya Dar es Salaam unapaswa kwenda sambamba na uanzishwaji wa Jiji la Dar es Salaam.
"Tunajenga masoko, tunakarabati na kujenga barabara zote; karibu kilomita 250 zimezungumzwa hapa, na mikataba inakwenda kusainiwa leo," amesema Waziri Mchengerwa.
Pia soma:
Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Ameeleza kuwa tayari mikataba ya ujenzi wa barabara hizo itasainiwa na kuanza kutekelezwa mara moja, akisisitiza kuwa mji wa Dar es Salaam una nafasi muhimu sana katika kuchangia uchumi wa nchi.
Aidha, Waziri Mchengerwa amewataka watendaji wa wizara yake kufanya kazi kwa ufanisi na kuharakisha mchakato wa kuanzishwa kwa jiji hilo, akisisitiza kuwa agizo hilo ni sehemu ya maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.
"Mchakato wa uanzishwaji wa jiji la Dar es Salaam usichelewe ufanyie mara moja...Wataalamu wapo, waharakishe wasinichokonoechokonoe," amesema Waziri huku akitoa angalizo kwa Katibu Mkuu wa TAMISEMI.
Wakati wa hafla hiyo, Waziri Mchengerwa amebainisha kuwa maboresho ya miundombinu yanayofanyika jijini Dar es Salaam ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha huduma za kijamii na kuongeza tija katika sekta mbalimbali za kiuchumi.
Kwa mujibu wa Mchengerwa, utekelezaji wa mikataba ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa karibu kilomita 250 katika mkoa wa Dar es Salaam ni hatua muhimu kuelekea katika kutengeneza jiji lenye miundombinu ya kisasa na ya kuvutia zaidi.
TAMISEMI
Acha ujinga.Hii habari mbona kama ya mwaka 1975? Dar iwe jiji? Mchengerwa amekosa la kuagiza au ana weweseka
Jiwe alibadilisha hilo, yaani yule jamaa alikuwa hatari sana kwa ustawi wa Taifa letuKwani Dar es Salaam sio jiji??
Hatuwezi kuendelea kuishi katika zama za giza za kugeuza Chato kuwa jiji.Jiji ni Dar es Salaam na siyo Ilala.Jiji ni ilala ndiyo iliyopewa hadhi kipindi cha mwendazake naona anataka kurudisha kile mwendazake alichokivunja
Marehemu anapiganaje vita? Au na wewe zimetoka kama Sukuma gang wenzio. Jiwe alishashindwa vita kwa ujinga wake mwenyewe. PeriodMwendelezo wa vita dhidi ya marehemu.
Magufuli alikuwa kivuruge.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, ametoa agizo la haraka kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuhakikisha mchakato wa uanzishwaji wa Jiji la Dar es Salaam unakamilika kabla ya mwaka 2025.
TAMISEMI
Alilivuruga yule kivuruge wa chato aliyeko kuzimu sasa hiviJiji lililokuwepo lilipelekwa wapi?
Ilala pekee ndio ilikuwa jiji.Kwahyo dar ilikuwa nini ? Manispaa au Mkoa?
Hizo Wilaya za Dar ziwe majijini, halafu kuwe na Greater Dar es Salaam halafu hizo nyingine ziwe miji ndogondogo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, ametoa agizo la haraka kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuhakikisha mchakato wa uanzishwaji wa Jiji la Dar es Salaam unakamilika kabla ya mwaka 2025.
TAMISEMI
Jiji wakati wa awamu ya tano lilivunjwa kwakuwa lilikuwa linahang tu halina vyanzo vyake binafisi wala eneo la kiutawala na lilikuwa linategemea manispaa kuingiza kipato.Kwenye hili nakubaliana na Mchengerwa,jiji la Dar es Salaam lipo tofauti na majiji mengine.
Majiji mengine wamechukua lile eneo la mjini ndiyo imepewa hadhi ya jiji na kuziacha zile halmashauri za pembezoni kuwa manispaa na halmashauri za miji lakini Dar es Salaam yote ni mjini hivyo huwezi kuifanya wilaya ya Ilala tu ndiye iwe jiji halafu uiache Kinondoni, Oysterbay,Masaki n.k eti ziwe katika manispaa hii siyo kweli.
Tena napendekeza liundwe jiji kama ilivyokuwa awamu ya kwanza na ya pili kwamba halmashauri ya jiji iwe moja na iwe na kanda za Ilala,Kinondoni, Temeke,Ubungo na Kigamboni lakini Mkurugenzi ni mmoja tu hao wa kanda waitwe vyovyote lakini bosi wao ni mmoja tu isiwe kama jiji lilovunjwa na Magufuli ambapo wilaya zote zilikuwa manispaa na jiji likawa lipo kisanii tu lisilo na jukumu wala nguvu yoyote kwa sababu kila halmashauri ilikuwa ndiyo wenye ardhi,shule,vituo vya afya n.k.