Mchengerwa aagiza Mchakato wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jjiji la Dar uanze

Mchengerwa aagiza Mchakato wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jjiji la Dar uanze

MCHENGERWA: MCHAKATO WA KUANZISHA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM UANZE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameelekeza mchakato wa uanzishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Jiji la Dar es salaam uanze mara moja ili kuratibu maendeleo yote yanayofanyika kwenye Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara katika halmashauri tano za Mkoa wa Dar es salaam leo Oktoba 24, 2024 kwenye viwanja vya Mwengeyanga Manispaa ya Temeke.

Amesema Mkoa wa Dar es salaam unatakiwa kuwa Kioo cha nchi na wageni wote wanapokuja hapa wanatakiwa kuona sura ya Tanzania hivyo inapaswa kuwa na chombo kinachoratibu maendeleo yake na kuhakikisha kuwa mipango yote ya maendeleo inayofanyika na inakua na muunganiko.

Ameongeza kuwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji ma Dar es salaa awamu ya Pili (DMDP II) kuna miradi mikubwa inayotekelezwa kama ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara na uendelezaji wa bonde la mto msimbazi hivyo miradi mikubwa kama hiyo kwenye halmashauri inahitaji chombo cha kusimamia.

"Hata majiji makubwa duniani yote yanakuwa na ‘Metropolitan City’ na sio halmashauri zinazojitemea kila moja inapangwa kivyake kunatakiwa kuwa na chombo ambacho kinaunganisha jitihada zinazofanywa kwenye halmashauri zote na kuzitaribu ili Jiji husika liweze kukua kwa viwango vya kimataifa."

"Nataka hii Dar es salaam iwe ya viwango na ubora na ukuaji wake uratibiwe kwa taratibu maalunu na sio kukua kiholela tu hii itafanya hadhi ya Dar es salaam isikue haraka na kuwa na hadhi ya kimataifa,"amesema.

&&&
 
Jiji wakati wa awamu ya tano lilivunjwa kwakuwa lilikuwa linahang tu halina vyanzo vyake binafisi wala eneo la kiutawala na lilikuwa linategemea manispaa kuingiza kipato.

Lilikuwa mzigo tu. Hawa wanasiasa wanatuchanganya na Dana Dana zao kila siku.

Kwa staili hii ya kupiga hatua moja na kurudi nyuma maendeleo tuyasikie kwa wengine tu.

Huyo mchengerwa apambane na mwendokasi kwanza wateja wapo ila mabasi hakuna.
Ndiyo maana ni muhimu kuwa na jiji moja linalomiliki hizi manispaa zote kama ilivyokuwa zamani kabla halijavunjwa na Waziri mkuu wa awamu ya tatu Frederick Sumaye na kuunda muundo wa ovyo ambao baadaye ukavunjwa na Magufuli, lakini naye akafanya makosa pale alipoamua kuifanya manispaa ya Ilala pekee ndiyo iwe na hadhi ya jiji,ebu fikiria inakuwaje sehemu kama chanika au vingunguti iwe sehemu ya jiji lakini eti masaki au Kinondoni kuwe sehemu ya manispaa!
 
Mkuruohkaji,wale ni sampuli Nyerere alisema Kila wanachoambiwa na wake zao wanafanya
Nadhani, Magufuli alikuwa na lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa jiji lisilokuwa Wilaya. KWASABABU JIJI LA DSM LILIONEKANA LINALETA UTATA KWENYE CHANZO CHAKE CHA MAPATO( KWAHIYO, JIJI LA DSM MAPATO YAKE LILIKUWA LINATEGEMEA KUTOKA HALMASHAURI ZA MANISPAA ZA ILALA, KINONDONI, TEMEKE, UBUNGO, NK.
HIVYO MKURUGENZI WA JIJI HANA ENEO LA UTAWALA ( HATA WATENDAJI WAKE HAWANA ENEO LA UTAWALA). KATIKA MAZINGIRA HAYO KUFUTWA ILIKUWA LAZIMA, ILI KUONDOA MKANGANYIKO.
 
Bado hii taarifa ya TAMISEMI haiwaambii wakazi, tamko hili lina mguso gani kwa wakaazi wa jiji hili kubwa kukiko yote Afrika ya Mashariki.
 
Kwani Dar es Salaam sio jiji??
Lilivunjwa na Magufuli alisema Haiwezekani Mkoa Mzima Ukawa Jiji akasema Inayopaswa Kuwa Jiji ni Ilala na Sio Mkoa Mzma kwahyo akapandisha Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji la Dar es salaam huku Wilaya zingine zikiwa Manispaaa
 
Ninachoona ni njia ya upigaji dar uiite hata PORI LA AKIBA haisaidiii kitu watu wanaishi na kaz znaendelea kama kawaida mngepambana hv miaka ya 80 au 90 sio sasa Naona mnapagawa na Uchaguzi tu
 
Nadhani, Magufuli alikuwa na lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa jiji lisilokuwa Wilaya. KWASABABU JIJI LA DSM LILIONEKANA LINALETA UTATA KWENYE CHANZO CHAKE CHA MAPATO( KWAHIYO, JIJI LA DSM MAPATO YAKE LILIKUWA LINATEGEMEA KUTOKA HALMASHAURI ZA MANISPAA ZA ILALA, KINONDONI, TEMEKE, UBUNGO, NK.ngeHIVYO MKURUGENZI WA JIJI HANA ENEO LA UTAWALA ( HATA WATENDAJI WAKE HAWANA ENEO LA UTAWALA). KATIKA MAZINGIRA HAYO KUFUTWA ILIKUWA LAZIMA, ILI KUONDOA MKANGANYIKO.
Alipolivunja angelirudisha katika muundo wa awali uliokuwepo kabla ya kuvunjwa na Frederick Sumaye,na tena Sumaye ndiye aliyelivuruga jiji hadi kutokea mkanganyiko wote huu kwa kuunda manispaa tatu wakati ule na halmashauri ya jiji lisilo na eneo la utawala wala shughuli mahsusi.
 
Back
Top Bottom