Mchengerwa aagiza Mchakato wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jjiji la Dar uanze

Mchengerwa aagiza Mchakato wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jjiji la Dar uanze

JPM alishangaza hakuna Jiji lenye vijiji kama kangaroo,Yani ufike Tokyo, New York,London ukute Jiji ndani yake Kuna tujiji ni aibu Ile afadhali ameindoa,lengo lilikuwa ni kupambana tu na CHADEMA,yule Mzee alikuwa WA ajabu sanaaaa
 
Kwani huko nyuma ilikuwaje?
Hadi linavunjwa na Waziri mkuu Frederick Sumaye wakati huo Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam lilikuwa limejumuisha wilaya zote tatu wakati huo Ilala, Kinondoni na Temeke.
Lilivyoundwa upya mwaka 2000 ndiyo zikaanzishwa manispaa tatu kila moja ikiwa na mamlaka kamili katika eneo lake la utawala na kisha kuundwa Halmashauri ya jiji ambalo kimsingi halikuwa na jukumu la maana zaidi ya kuundwa kisiasa tu.
 
Hii habari mbona kama ya mwaka 1975? Dar iwe jiji? Mchengerwa amekosa la kuagiza au ana weweseka
Hajasema Dar iwe Jiji, amesema ianzishwe Mamlaka ya Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam, ambayo sasa itakuwa juu ya Manispaa za Kindondoni, Temeke na Ilala. Unajua kwa sasa ni kwamba hizi manispaa zinajitegemea, kwa hiyo Jiji linakuwapo kama halipo. Kwa hiyo analipa meno ya kuwa juu ya hizi Manispaa tatu. Wakurugenzi wa Manispaa watawajibika kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uendelezaji Jiji, japo wote ni wateule. Itakuwa kama mkuu wa mkoa na wakuu wake wa wilaya.

Kuna fursa za kazi na kuteuliwa hapo. Nadhani ingefaa niteuliwe kuwa Director General wa Dar es Salaam City Development Authority (DACIDA) kwa sababu mimi nimemuelewa sana.

Mchengerwa nitafute tuongee basi!
 
Unamaanisha Halmashauri moja iwajibike kwa Halmashauri nyingine? Unadhani ni kitu kinachowezekana?

Labda kama hizo halmashauri nyingine zitavunjwa na hakutakua tena na wakurugenzi wa hizo wilaya, vinginevyo Mkurugenzi wa Jiji ataendelea kubaki kivuli na hatakua na sauti yoyote kwenye mapato na matumizi.
 
Umemsikia Mchengerwa lakini? Anasema mipango yote itapangwa na Mamlaka ya Jiji, kwa sababu siku zote kutakuwa na mwingiliano wa miradi ya Jiji la Dar kati ya manispaa na manispaa. Chukulia barabara ya Ubungo kwenda Posta Mpya. Inaanzia Kindondoni na kuishia Ilala. Au ile ya Mandela, inaanzia Kindondoni na kuishia Temeke. Sasa kama ni planning, nani afanye hiyo combined planning? Kindondoni? Ilala? Temeke? Ndio maana Mchengerwa anataka kuwepo na Mamlaka inayoangalia development planning ya Jiji la Dar es Salaam, bila kuwa na context ya mipaka na mamlaka za Halmashauri, na kisha Halmashauri zinakuwa sehemu ya utekelezaji.

Mradi wa BRT hiwezi kusema ni wa Ilala, Kindondoni na Temeke.Unatekelezwa katika context ya Jiji la Dar es Salaam. Sasa ikiwa Manispaa zitaachwa ziendeleze manispaa zao, huwezi kutokeza kitu kama Mradi wa Mwendokasi ambao una context ya Jiji badala ya Manispaa. Lazima uwe na Mamlaka ya Jiji. Sasa Je, City Development Authority itasimamia miradi kama Mwendokasi? Mimi nitasema ndio, kwa sababu ni miradi haiwezi kuwa chini ya usimamizi wa Manispaa fulani au ksema Manispaa zisimamie Mwendokasi katika maeneo yao.

Kwa hiyo kinachohitajika ni Mamlaka ambayo itapanga uendelevu wa JIJI bila kuwa na mtazamo wa mipaka ya Manispaa, kwa sababu wao wanachoangalia ni maendeleo ya Jiji kama jurisdiction moja, integrated city development, bila kujali mradi utatekelezwa katika Manispaa ipi. Kwa mfano, ukisema tujenge uwanja wa Olympic Dar es Salaam, nani atapewa hiyo kazi au kuamua ujengwe wapi? Kila Manispaa itasema ujengwe kwetu. Sasa Mchengerwa ndio hataki maendeleo ya jiji kuwa constrained na jurisdictional context ya hizi municipals.

Kuhusu manispaa kuwajibika kwa jiji, kutakuwa na mipaka. Kuna vitu vitaachwa kwenye manispaa, ila lazima wakubali mamlaka yao katika miradi ya maendeleo itapunguzwa na uwepo wa City Devepment Authority. Kumbuka DACIDA haitakuwa ikifanya kazi za utawala wa Jiji - wao shughuli yao iyakuwa ni City Development tu. Mambo ya parking, leseni za biashara nk, yatabaki kwenye manispaa. Ila vitu kama ujenzi nk, wanaweza wakawa na saui zaidi, kwa sababu hata ujenzi wa nyumba binafsi ni suala na Ciy Development, na tunataka kupunguza ujenzi holela. Mfano centrlized sewage sysem ya Dar, itaingia upande wa Ciy Development Authority, lakini ada za sewage services wataachiwa Manispaa wakusanye toka residents wao

Bado Mchengerwa anitafute - we think alike😀
 
Nadhani, Magufuli alikuwa na lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa jiji lisilokuwa Wilaya. KWASABABU JIJI LA DSM LILIONEKANA LINALETA UTATA KWENYE CHANZO CHAKE CHA MAPATO( KWAHIYO, JIJI LA DSM MAPATO YAKE LILIKUWA LINATEGEMEA KUTOKA HALMASHAURI ZA MANISPAA ZA ILALA, KINONDONI, TEMEKE, UBUNGO, NK.
HIVYO MKURUGENZI WA JIJI HANA ENEO LA UTAWALA ( HATA WATENDAJI WAKE HAWANA ENEO LA UTAWALA). KATIKA MAZINGIRA HAYO KUFUTWA ILIKUWA LAZIMA, ILI KUONDOA MKANGANYIKO.
Ilikuwa roho ya visasi ya shetani mdogo Magu. Alikuwa na visa vyake binafsi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji ndg Kabwe.
Hamna tofauti na alichofanya Kwa Tume ya Mipango na Mamlaka ya Uendelezaji wa Blonde la Rufiji ambazo zote zimerudishwa.

Magu alikuwa anaipeleka nchi hii kuzimu. Yule mtu alikuwa na roho ya kutu kuliko Shetani.
 
Kuna halmashauri hazijaunganishwa na barabara za lami hadi leo, naona bajeti ya ujenzi kila Siku ni Dar, Kodi ya karagwe inajenga Dar wakati wenyewe vumbi tupu
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ameelekeza mchakato wa uanzishaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam uanze mara moja ili kurataibu maendeleo yote yanayofanyika kwenye halmashauri za mkoa wa Dar es salaam.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara katika halmashauri tano za Mkoa wa Dar es salaam leo tarehe 24.10. 2024 kwenyz viwanja vya Mwengeyanga Manispaa ya Temeke.

Amesema Mkoa wa Dar es salaam unatakiwa kuwa Kioo cha nchi yetu na wageni wote wanapokuja hapa wanatakiwa kuona sura ya Tanzania hivyo mkoa huu unatakiwa na chombo kinachoratibu maendeleo ya mji huu na kuhakikisha kuwa mipango yote ya maendeleo inayofanyika hapa inakua na muunganiko ili kulete ile sura tunayoitegemea.

Ameongeza kuwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji ma Dar es salaa awamu ya Pili (DMDP II) kuna miradi mikubwa inayotekelezwa kama ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara na uendelezaji wa bonde la mto msimbazi, miradi mikubwa kama hii ikiachwa kwenye halmashauri inaweza isiweze kujiendesha hivyo kuwe na chombo cha kusimamia miradi mikubwa kama hii na kuhakikisha inaungana na jitihada zingine za maendeleo zinazofanywa katika halmashauri za mkoa huu.

Hata majiji makubwa duniani yote yanakuwa na ‘Metropolitan City’ na sio halmashauri zinazojitemea kila moja inapangwa kivyake kunatakiwa kuwa na chombo ambacho kinaunganisha jitihada zinazofanywa kwenye halmashauri zote na kuzitaribu ili Jiji husika liweze kukua kwa viwango vya kimataifa.

Nataka hii Dar es salaam iwe ya viwango na ubora na ukuaji wake uratibiwe kwa taratibu maalumu na sio kukua kiholela tu hii itafanya hadhi ya Dar es salaam isikue haraka na kuwa na hadhi ya kimaraifa.

TAMISEMI
Matumizi mabaya ya ofisi
Dar es salaam ianzishwe mara ngapi, Dar imebanana mno, hayo ilibidi yakafanyike Dodoma, ingesaidia kupunguza msongamano wa watu na changamoto zisizo za lazima. Watu wakienda kujenga mabondeni watasema serikali haihusiki...💀
Matumizi mabaya ya ofisi. Inatengenezwa duplication itakayoongeza gharama za kiutawala. ,mamlaka kuingiliana huku mamlaka mpya ikijiona superior hasa kstika miradi yenye rushwa kubwa.

Mchengerwa ajiulize kwa nini CDA ya Dodoma ilifutw.a
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ameelekeza mchakato wa uanzishaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam uanze mara moja ili kurataibu maendeleo yote yanayofanyika kwenye halmashauri za mkoa wa Dar es salaam.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara katika halmashauri tano za Mkoa wa Dar es salaam leo tarehe 24.10. 2024 kwenyz viwanja vya Mwengeyanga Manispaa ya Temeke.

Amesema Mkoa wa Dar es salaam unatakiwa kuwa Kioo cha nchi yetu na wageni wote wanapokuja hapa wanatakiwa kuona sura ya Tanzania hivyo mkoa huu unatakiwa na chombo kinachoratibu maendeleo ya mji huu na kuhakikisha kuwa mipango yote ya maendeleo inayofanyika hapa inakua na muunganiko ili kulete ile sura tunayoitegemea.

Ameongeza kuwa kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji ma Dar es salaa awamu ya Pili (DMDP II) kuna miradi mikubwa inayotekelezwa kama ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara na uendelezaji wa bonde la mto msimbazi, miradi mikubwa kama hii ikiachwa kwenye halmashauri inaweza isiweze kujiendesha hivyo kuwe na chombo cha kusimamia miradi mikubwa kama hii na kuhakikisha inaungana na jitihada zingine za maendeleo zinazofanywa katika halmashauri za mkoa huu.

Hata majiji makubwa duniani yote yanakuwa na ‘Metropolitan City’ na sio halmashauri zinazojitemea kila moja inapangwa kivyake kunatakiwa kuwa na chombo ambacho kinaunganisha jitihada zinazofanywa kwenye halmashauri zote na kuzitaribu ili Jiji husika liweze kukua kwa viwango vya kimataifa.

Nataka hii Dar es salaam iwe ya viwango na ubora na ukuaji wake uratibiwe kwa taratibu maalumu na sio kukua kiholela tu hii itafanya hadhi ya Dar es salaam isikue haraka na kuwa na hadhi ya kimaraifa.

TAMISEMI
Anawatengenezea watu nafasi ya ajira. Sijui kama itaendana na mapato.
 
TOKA MAKTABA :

TOKA MAKTABA

Jumatano Februari 24, 2021.

Magufuli
-“Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndio iwe jiji".

View: https://m.youtube.com/watch?v=G2MoZU_GB68

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam na kuchagua manispaa moja katika jiji hilo itakayopandishwa hadhi na kuwa Jiji lengo likiwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizindua daraja la juu la Ubungo leo Jumatano Februari 24, 2021.

Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndio iwe jiji itategemea na namna mambo yatakavyokwenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu wanachangiwa fedha na hawana miradi ya maendeleo hili nitalikataa.”

"Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa.

Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na ninafikiri Ilala inafaa kuwa jiji maana ndio ipo katikati.

Ubungo itasubiri maana barabara bado hazijatengenezwa,” amesema Rais Magufuli. Amewataka viongozi ambao walijiandaa kuwa mameya wa jiji wajue hilo limekwisha.

“Haiwezekani unakuwa na madiwani wamekaa tu wanatengewa bajeti hizo fedha ni vizuri zikapelekwa kwenye miradi ya maendeleo ya barabara hayo ni matumizi bora ya fedha za walipakodi kwa hiyo mjiandae kisaikolojia meya atapatikana katika manispaa ya Ilala,” amesisitiza.
Source : GILLY BONNY ONLINE TV
 
Ilikuwa roho ya visasi ya shetani mdogo Magu. Alikuwa na visa vyake binafsi na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji ndg Kabwe.
Hamna tofauti na alichofanya Kwa Tume ya Mipango na Mamlaka ya Uendelezaji wa Blonde la Rufiji ambazo zote zimerudishwa.

Magu alikuwa anaipeleka nchi hii kuzimu. Yule mtu alikuwa na roho ya kutu kuliko Shetani.
We nawe una chuki zako tu! Kwani Dar ishawahi kuwa Manispaa?
 
2021 24 February

Rais Magufuli atangaza rasmi kulivunja Jiji la Dar- es Salaam! ''huyu nataka achelewe kujinyonga''​

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam na kuchagua manispaa moja ya Ilala katika jiji hilo itakayopandishwa hadi na kuwa Jiji lengo likiwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizindua daraja la juu la Ubungo leo Jumatano Februari 24, 2021.

View: https://m.youtube.com/watch?v=3UQZiNdlGRA
 
TOKA MAKTABA :

TOKA MAKTABA

Jumatano Februari 24, 2021.

Magufuli
-“Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndio iwe jiji".

View: https://m.youtube.com/watch?v=G2MoZU_GB68

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam na kuchagua manispaa moja katika jiji hilo itakayopandishwa hadhi na kuwa Jiji lengo likiwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizindua daraja la juu la Ubungo leo Jumatano Februari 24, 2021.

Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndio iwe jiji itategemea na namna mambo yatakavyokwenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu wanachangiwa fedha na hawana miradi ya maendeleo hili nitalikataa.”

"Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa.

Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na ninafikiri Ilala inafaa kuwa jiji maana ndio ipo katikati.

Ubungo itasubiri maana barabara bado hazijatengenezwa,” amesema Rais Magufuli. Amewataka viongozi ambao walijiandaa kuwa mameya wa jiji wajue hilo limekwisha.

“Haiwezekani unakuwa na madiwani wamekaa tu wanatengewa bajeti hizo fedha ni vizuri zikapelekwa kwenye miradi ya maendeleo ya barabara hayo ni matumizi bora ya fedha za walipakodi kwa hiyo mjiandae kisaikolojia meya atapatikana katika manispaa ya Ilala,” amesisitiza.
Source : GILLY BONNY ONLINE TV

Kwaiyo Mchengerwa kajipangaje na ao Madiwani watakaokuwa wanasubiri bajeti za manispaa?
 
Naomba kujua barabara zilizotiwa sauni ya ujenzi kuanza ni zipi? Je barabara za kwenda kitunda.magole.mwanagati zipo? Huku hali ni mbaya sana.anauliza raia mwema wq kitunda
 
Kwenye hili nakubaliana na Mchengerwa,jiji la Dar es Salaam lipo tofauti na majiji mengine.
Majiji mengine wamechukua lile eneo la mjini ndiyo imepewa hadhi ya jiji na kuziacha zile halmashauri za pembezoni kuwa manispaa na halmashauri za miji lakini Dar es Salaam yote ni mjini hivyo huwezi kuifanya wilaya ya Ilala tu ndiye iwe jiji halafu uiache Kinondoni, Oysterbay,Masaki n.k eti ziwe katika manispaa hii siyo kweli.
Tena napendekeza liundwe jiji kama ilivyokuwa awamu ya kwanza na ya pili kwamba halmashauri ya jiji iwe moja na iwe na kanda za Ilala,Kinondoni, Temeke,Ubungo na Kigamboni lakini Mkurugenzi ni mmoja tu hao wa kanda waitwe vyovyote lakini bosi wao ni mmoja tu isiwe kama jiji lilovunjwa na Magufuli ambapo wilaya zote zilikuwa manispaa na jiji likawa lipo kisanii tu lisilo na jukumu wala nguvu yoyote kwa sababu kila halmashauri ilikuwa ndiyo wenye ardhi,shule,vituo vya afya n.k.
Mbona huu mfumo aliouleta magufuli ndio unatumika na majiji makubwa duniani hata marekani new york ni limji likubwa lakini manhattan pekee ndio jiji la new york ,mwanza nyamagana ndio jiji ilemela manispaa
 
Back
Top Bottom