Mchengerwa aagiza Mchakato wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jjiji la Dar uanze

Mchengerwa aagiza Mchakato wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jjiji la Dar uanze

Jiji wakati wa awamu ya tano lilivunjwa kwakuwa lilikuwa linahang tu halina vyanzo vyake binafisi wala eneo la kiutawala na lilikuwa linategemea manispaa kuingiza kipato.

Lilikuwa mzigo tu. Hawa wanasiasa wanatuchanganya na Dana Dana zao kila siku.

Kwa staili hii ya kupiga hatua moja na kurudi nyuma maendeleo tuyasikie kwa wengine tu.

Huyo mchengerwa apambane na mwendokasi kwanza wateja wapo ila mabasi hakuna.
Uko sahihi wengine hawaelewi
 
Soma uelewe kinachoundwa sio halmashauri ni chombo cha usimamizi
Unamaanisha Halmashauri moja iwajibike kwa Halmashauri nyingine? Unadhani ni kitu kinachowezekana?

Labda kama hizo halmashauri nyingine zitavunjwa na hakutakua tena na wakurugenzi wa hizo wilaya, vinginevyo Mkurugenzi wa Jiji ataendelea kubaki kivuli na hatakua na sauti yoyote kwenye mapato na matumizi
 
Alipolivunja angelirudisha katika muundo wa awali uliokuwepo kabla ya kuvunjwa na Frederick Sumaye,na tena Sumaye ndiye aliyelivuruga jiji hadi kutokea mkanganyiko wote huu kwa kuunda manispaa tatu wakati ule na halmashauri ya jiji lisilo na eneo la utawala wala shughuli mahsusi.
Halafu , Fredrick sumaye ndio kasoma law Harvard 😂, nyie, niacheni ninywe 🍻
 
Naomba kujua barabara zilizotiwa sauni ya ujenzi kuanza ni zipi? Je barabara za kwenda kitunda.magole.mwanagati zipo? Huku hali ni mbaya sana.anauliza raia mwema wq kitunda
Ninyi mnatakiwa muunganishwe kutokea kwa mpalange Ili muamue kupitia Yombo Buza au Mbagala Nzasa.

Ila wasiwasahau watu wa Kivule
Waipige Rami njia hii kuunganisha na Msongola na Banana.

Maana tupo jijini hata wakati wa kamanda jiwe akiwa madarakani
 
Ndiyo maana ni muhimu kuwa na jiji moja linalomiliki hizi manispaa zote kama ilivyokuwa zamani kabla halijavunjwa na Waziri mkuu wa awamu ya tatu Frederick Sumaye na kuunda muundo wa ovyo ambao baadaye ukavunjwa na Magufuli, lakini naye akafanya makosa pale alipoamua kuifanya manispaa ya Ilala pekee ndiyo iwe na hadhi ya jiji,ebu fikiria inakuwaje sehemu kama chanika au vingunguti iwe sehemu ya jiji lakini eti masaki au Kinondoni kuwe sehemu ya manispaa!
Si ajabu awamu ya saba tukashuhudia tangazo jipya tukirudi kule kule tulikokuwa.

Watakuja na sababu zao ambazo tutakubaliana nazo.

Mimi nadhani tuwe na by-laws ambazo zitafanya limitations kwa wanasiasa kufanya maamuzi ya kisera wenyewe bila kushirikisha jamii.

Mfano jambo hili lingepelekwa kwenye baraza la madiwani likajadiliwa na kuamuliwa.

Ila sio kama hivi kila mara ni mabadiliko. Mnawachanganya raia.
 
Hajasema Dar iwe Jiji, amesema ianzishwe Mamlaka ya Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam, ambayo sasa itakuwa juu ya Manispaa za Kindondoni, Temeke na Ilala. Unajua kwa sasa ni kwamba hizi manispaa zinajitegemea, kwa hiyo Jiji linakuwapo kama halipo. Kwa hiyo analipa meno ya kuwa juu ya hizi Manispaa tatu. Wakurugenzi wa Manispaa watawajibika kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uendelezaji Jiji, japo wote ni wateule. Itakuwa kama mkuu wa mkoa na wakuu wake wa wilaya.

Kuna fursa za kazi na kuteuliwa hapo. Nadhani ingefaa niteuliwe kuwa Director General wa Dar es Salaam City Development Authority (DACIDA) kwa sababu mimi nimemuelewa sana.

Mchengerwa nitafute tuongee basi!
We jamaa unastahili uteuzi hujaacha pointing hata Moja hahahah
 
Hadi linavunjwa na Waziri mkuu Frederick Sumaye wakati huo Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam lilikuwa limejumuisha wilaya zote tatu wakati huo Ilala, Kinondoni na Temeke.
Lilivyoundwa upya mwaka 2000 ndiyo zikaanzishwa manispaa tatu kila moja ikiwa na mamlaka kamili katika eneo lake la utawala na kisha kuundwa Halmashauri ya jiji ambalo kimsingi halikuwa na jukumu la maana zaidi ya kuundwa kisiasa tu.
Huo muundo wa jiji uliovunjwa na Sumaye ulikuwaje? Bila shaka utakuwa unaongelea Tume ya jiji (Keenja). muundo wake ulikuwaje tofauti na miundo iliyofuata? Uora wake ulikuwa upi?
Maboresho na mageuzi ya kiutawala kwa jiji yapo toka uhuru vunja unda vunja unda imekuwa ni tukio linalojirudia. Hii inaashiria uwepo wa tatizo kubwa ambalo halijapata jawabu.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa inaliongoza Jiji kutoka mwaka 1961 mpaka mwaka 1972, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizivunja Halmashauri zote nchini na kuwa chini ya Usimamizi wa Serikali Kuu (Madaraka Mikoani)

Serikali Kuu ilizirudisha Serikali za Mitaa Nchini, Chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na. 8 ya mwaka 1982, ambapo Halmashauri ya Jiji ilianza kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwaka 1983.

Mwaka 1996 Serikali Kuu iliivunja Halmashauri ya Jiji na kuunda Tume ya jiji la Dar es Salaam, kwa Tangazo la serikali Na. 110 na 111 ya tarehe 28 Juni mwaka 1996.

Tume ya jiji ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka minne, ambapo mwaka 2000 Serikali iliunda mamlaka nne za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya Mwaka 1982, kama ilivyo rekebishwa kwa sharia na. 6 ya mwaka 1999.
 
Jiwe alikuwa mwehu yule.

Alikuwa anatafuta gia ya kutaka kukipatia hadhi ya jiji kile Kijiji cha Chato.

Alikuwa mshamba na mjinga sana yule jamaa.
Kwa akili yako Unadhani Magufuli ndio wa kwanza kulivunja jiji kujaribu muundo mbadala,Na hawa walikuwa wehu waliovunja jiji kabla ya Magufuli?

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa inaliongoza Jiji kutoka mwaka 1961 mpaka mwaka 1972, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizivunja Halmashauri zote nchini na kuwa chini ya Usimamizi wa Serikali Kuu (Madaraka Mikoani)

Serikali Kuu ilizirudisha Serikali za Mitaa Nchini, Chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na. 8 ya mwaka 1982, ambapo Halmashauri ya Jiji ilianza kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwaka 1983.

Mwaka 1996 Serikali Kuu iliivunja Halmashauri ya Jiji na kuunda Tume ya jiji la Dar es Salaam, kwa Tangazo la serikali Na. 110 na 111 ya tarehe 28 Juni mwaka 1996.

Tume ya jiji ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka minne, ambapo mwaka 2000 Serikali iliunda mamlaka nne za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya Mwaka 1982, kama ilivyo rekebishwa kwa sharia na. 6 ya mwaka 1999.
 
Nafikiri sisi tumekumbwa na hali ya kukariri jina maarufu la sehemu husika.

Mfano:- Songea na ni Wilaya pia ni Manispaa ikitokea imekuwa kihadhi basi itapandishwa hadhi na kuwa Jiji na itapaswa kuitwa Jiji la Songea ijapokuwa iko mkoa wa Ruvuma.

Bukoba- Wilaya/ Manispaa ikipanda itakuwa Jiji la Bukoba sio Jiji la Kagera.

Moshi Manispaa unasikia wanaomba hadhi ya Jiji sio Kilimanjaro ndiyo inaomba na hivo ikipata itapaswa kuitwa Jiji la Moshi sio Kilimanjaro.
Wewe ndio umenielewesha vizuri
 
Kwani Dar es Salaam sio jiji??
Kuna jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Dar es Salaam. Magufuli aliifanya Manispaa ya Ilala peke yake ndiyo iunde jiji la Dar es Salaam na Manispaa zilizobaki ziwe tu mkoa wa Dar es Salaam.

Kauli hii ya Mchengerwa ni kama inabatilisha maamuzi ya Magufuli na kurudisha muundo wa zamani wa Manispaa zote za Dar es Salaam kuunda jiji la Dar es Salaam.

Ova
 
24 February 2024 Breaking:​

Rais JPM Alivunja Jiji la Dar, Aipandisha Ilala​

DAR-1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameivunja rasmi Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na kwa mamlaka aliyonayo ameipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuanzia leo Jumatano Februari 24, 2021.
IMG-20210224-WA0346-688x1024.jpg

PM alivunja Jiji la D'salaam, aipandisha hadhi Manispaa ya Ilala​

1729819935503.jpeg

Imewekwa tarehe: February 24th, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amelivunja Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Halmashauri ya Jiji.

Rais, Dkt. Magufuli amefanya maamuzi hayo leo tarehe 24 Februari, 2021 kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo.

Waziri Jafo alisema kuwa, kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 84 cha Sheria ya Serikali za Mitaa, sura ya 288, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia tarehe 24 Februari, 2021.

“Kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 5 (1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za miji) sura ya 288, Rais, Dkt. John Magufuli ameipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam” alisema Waziri Jafo.

Waziri Jafo alisema kuwa taratibu nyingine za kisheria zitakamilishwa ikiwa ni pamoja na kuhamisha shughuli za iliyokuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo imevunjwa kwenye Halmashauri mpya ya Jiji la Dar es salaam na kuwapangia vituo vipya vya kazi watumishi wa halmashauri iliyovunjwa.

Aidha, mgawanyo wa mali na madeni ya iliyokuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo imevunjwa utafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za miji) sura ya 288 na Sheria nyingine zinazohusika.

Leo wakati Rais, Dkt. Magufuli akizindua daraja la juu la Kijazi, lililopo Ubungo, Dar es Salaam alisema kuwa anakusudia kulivunja Jiji hilo ili gharama zilizokuwa zinatumika kuendesha halmashauri hiyo zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.

“Nategemea kufanya mabadiliko kidogo, mabadiliko haya ya kuwa na manispaa ambazo zinawakilisha maeneo halafu unakuwa na jiji ambalo linakaa halina maeneo yoyote, natarajia Jiji la Dar es Salaam kulivunja, nawaambia hapa ili tutengeneze Jiji la eneo fulani” alisema.

“…lakini kuwa na madiwani wanakaa juu, wanachangiwa hela na hawana miradi ya maendeleo, wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu. Hili nitalikataza. Wale wanaojiandaa kuwa mameya wa Dar es Salaam na wanakaa hawana maeneo, wajue hilo limekwisha” alisema Rais, Dkt. Magufuli

View: https://m.youtube.com/watch?v=sWFQ1rInPRE

Rais John Magufuli leo Februari 24 2021 ameivunja Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Halmashauri ya jiji hilo. Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo imesema Rais Magufuli ametumia mamlaka yake chini ya kifungu cha 84 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Miji) Sura ya 288 kufanya mabadiliko hayo.
 
Huo muundo wa jiji uliovunjwa na Sumaye ulikuwaje? Bila shaka utakuwa unaongelea Tume ya jiji (Keenja). muundo wake ulikuwaje tofauti na miundo iliyofuata? Uora wake ulikuwa upi?
Maboresho na mageuzi ya kiutawala kwa jiji yapo toka uhuru vunja unda vunja unda imekuwa ni tukio linalojirudia. Hii inaashiria uwepo wa tatizo kubwa ambalo halijapata jawabu.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa inaliongoza Jiji kutoka mwaka 1961 mpaka mwaka 1972, ambapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizivunja Halmashauri zote nchini na kuwa chini ya Usimamizi wa Serikali Kuu (Madaraka Mikoani)

Serikali Kuu ilizirudisha Serikali za Mitaa Nchini, Chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) na. 8 ya mwaka 1982, ambapo Halmashauri ya Jiji ilianza kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma kwa wananchi kuanzia mwaka 1983.

Mwaka 1996 Serikali Kuu iliivunja Halmashauri ya Jiji na kuunda Tume ya jiji la Dar es Salaam, kwa Tangazo la serikali Na. 110 na 111 ya tarehe 28 Juni mwaka 1996.

Tume ya jiji ilifanya kazi kwa kipindi cha miaka minne, ambapo mwaka 2000 Serikali iliunda mamlaka nne za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dar es Salaam kwa sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Na. 8 ya Mwaka 1982, kama ilivyo rekebishwa kwa sharia na. 6 ya mwaka 1999.
Nimeeleza hapo kwamba halmashauri ya jiji ilikuwa moja tu ikijumuisha wilaya zote tatu zilizokuwepo wakati huo baadaye ndiyo ikavunjwa na kuundwa tume ya jiji kabla haijaundwa upya na kuweka manispaa tatu Ilala,Temeke na Kinondoni na Halmashauri ya jiji ambayo nimesema kimsingi sikuona jukumu lake hasa(labda iliundwa kisiasa tu).
Lakini kwa jinsi ulivyokuwa mgumu kuelewa unaniuliza eti hilo jiji lilovunjwa na Sumaye lilikuwaje! Na eti labda nazungumzia tume ya jiji iliyokuwa ikiongozwa na Keenja! Inaonekana ni mzito sana kuelewa.
Sina ufafanuzi zaidi.
 
Mbona huu mfumo aliouleta magufuli ndio unatumika na majiji makubwa duniani hata marekani new york ni limji likubwa lakini manhattan pekee ndio jiji la new york ,mwanza nyamagana ndio jiji ilemela manispaa
Kwahiyo wewe unaona sawa kule pugu mnadani kuwa jiji lakini kule Magomeni kuwe manispaa!
 
Back
Top Bottom