Mchengerwa aagiza Mchakato wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Jjiji la Dar uanze

Ndio umeyajua haya sasa hivi? Mbona hukusema hivyo wakati Chato ilipotaka kufanywa mkoa??
 
Unajificha kwenye kichaka, umeulizwa ubora wa muundo huo ulikuwa upi unasema huna jibu, kusema tu halmashauri ilijumuisha wilaya zote pasipo kusema ni vipi ilikuwa effective zaidi ni maneno matupu, nimekuwekea ni excerpt ya historical reforms za jiji la dsm inayoonyesha vunja unda vunja, kama one all encompassing council was the best format nayo ikapigwa chini huoni tatizo lipo? Halmashauri moja ilikuwa too big to give equal attention to all surbubs utoaji huduma ulizorota hasa kwa maeneo ya pembezoni, Unakalia iliyovunjwa ilikuwa bora huo ubora kimuundo uliovonjwa na sumaye huusemi.
 
Kama ambavyo nimesema sina ufafanuzi zaidi ili tuendelee kubishana pasipo na tija yoyote.
Hiyo historia uliyoiweka siyo kitu cha kujisifu na kujiona mjuaji maana kila mtu anaweza kuisoma kwenye website ya Halmashauri ya jiji ulichofanya ni ku copy na ku paste.
 
huna ufafanuzi ni jibu zuri
 
Hii sasa inachekesha sana Magufuli alilifunja jiji leo Mchengerwa analirudisha ! Ama kweli Ukishangaa ya Mussa utaona ya Firauni !
 
Huu muundo wengi hawauelewi. Maana hakuna eneo la kiutawala linaitwa Dar. Ni Kama ilivyo Ruvuma, Kagera

Mchanganyiko huu pia ulifanya hata mkapa akavunja halmashauri ya jiji la dar.

Magufuli alichukua muundo wa majiji mengine, Arusha jiji ina eneo la kiutawala sababu kuna wilaya ya Arusha mjini, mbeya jiji Ina eneo la kiutawala sababu kuna wilaya ya mbeya mjini, hivyo hivyo kwa Tanga, mwanza. Mbeya ni jiji lakini haimaanishi aliyepo kyela au chunya nae yupo jiji la mbeya. Jiji ni mjini, hii ndio ilikua idea ya magufuli

Mchengerwa hajamaamisha hivyo ulivyosema, nadhani anakuja na ule muundo wa mkapa(tume ya jiji) ili kusimamia manispaa zote
 
Hii sasa inachekesha sana Magufuli alilifunja jiji leo Mchengerwa analirudisha ! Ama kweli Ukishangaa ya Mussa utaona ya Firauni !
Hakuna ajabu maamuzi huwa yanategemea wakati, mkapa alilivunja pia
 
Nisaidie kunielelewesha utofauti wa halmashauri ya jiji na tume ya jiji muundo wake ulikuwa vipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…