Mchengerwa: Hali ya Jenista Mhagama ilikuwa mbaya, madaktari walifanya kazi kubwa

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Waziri wa Afya, Mohammed Mchengerwa, amefichua kuwa licha ya jitihada kubwa zilizofanywa na madaktari wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kuokoa maisha ya aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, hali yake ilikuwa mbaya sana alipowasili hospitalini hapo na baadaye alifariki dunia.

Akizungumza leo Jijini Dodoma, nyumbani kwa marehemu Itega, Mchengerwa amesema alipokea taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwamba madaktari walipambana kwa nguvu zote tangu walipompokea marehemu, lakini licha ya juhudi hizo, Mungu alimchukua.

1765568625028.png

“Nichukue fursa hii kuwashukuru madaktari wote waliomhudumia pale Benjamin Mkapa. Walifanya kazi kubwa sana mpaka dakika za mwisho ambapo Katibu Mkuu alinifahamisha kuwa hali yake ilikuwa mbaya sana na baadaye Mwenyezi Mungu akamchukua,” amesema Mchengerwa.

Aidha, Waziri Mchengerwa amewataka madaktari wa hospitali hiyo kuendelea kuwa na moyo wa kutoa huduma bora kwa wagonjwa wengine kama walivyofanya kwa marehemu Jenista Mhagama. Vilevile, ameahidi kuwa Wizara ya Afya itaendeleza na kutekeleza maono, dira na miradi aliyoiacha Jenista Mhagama mara baada ya kumkabidhi kijiti cha uongozi ndani ya wizara hiyo hivi karibuni.
 
Hapo sasa ni MBWA anapokula watoto wake. Sisi tunafanya mahesabu .... 1, .....!! Wakimaliza mambo yao tunatoa idadi.
 
Mara baada ya Jenister Mhagama kumkabidhi ofisi ndugu Mchengerwa, alipata kizunguzungu na kudondoka (Jenister) chini, akateguka mguu na kupoteza fahamu.

Akibanwa vizuri Mchengerwa ataeleza alifanya nini mama wa watu.
 
hizi politics za tanzagiza huwa sizielewi, hivi familia haiwezi kukataa mtu xyx kuja “kutoa pole”? yaani hawana haki ya kuamua nani aje na nani asije? na wazike wapi au daktari gani afanye autopsy? …
 
Mara baada ya Jenister Mhagama kumkabidhi ofisi ndugu Mchengerwa, alipata kizunguzungu na kudondoka (Jenister) chini, akateguka mguu na kupoteza fahamu.

Akibanwa vizuri Mchengerwa ataeleza alifanya nini mama wa watu.
Mkuu, haiwezi kuwa ni kihoro cha kukosa uwaziri? Lema alisema huyu mama anapenda uwaziri sana.
 
Back
Top Bottom