Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa amekosoa utaratibu unaotumika wa abiria kuingia na kutoka stesheni kuu ya treni ya mwendokasi (SGR) Dodoma, kuwa umekuwa ukileta adha kwa abiria, hivyo ametoa maagizo kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha ndani ya siku saba wanabadilisha utaratibu huo.
Soma Pia: Treni ya SGR kutoka Dar kwenda Dodoma yadaiwa kukwama tena baada ya Umeme kukatika Stesheni ya Kilosa
“Ninawataka Wakurugenzi wote wa majiji lakini hasa Jiji hili la Dodoma ndiyo Makao Makuu ya Nchi, Mkuu wa Mkoa, Wilaya nendeni mkajipange hasa pale eneo la stesheni ya rel, utaratibu wa watu kuingia na kutoka haujakaa vizuri, nendeni mkakae pamoja na TRC muweke utaratibu mzuri, haieleweki, Rais hawezi kutuelewa”