Mchengerwa: Wanafunzi wote wa kutwa wapate chakula shuleni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kuhakikisha wanafunzi walio katika shule zote za kutwa za umma na binafsi wanapata chakula bila kujali ni wa madarasa ya mitihani ama lah na kamati za shule ziimarishe usimamizi wa chakula kinachotolewa na wazazi kwa ajili ya mpango wa chakula shuleni.
Snapinsta.app_457245674_18341997856193701_6027776350016502373_n_1080.jpg

Snapinsta.app_457655786_18341997931193701_5870765209689528489_n_1080.jpg
Pia amewataka kuendelea kusimamia kikamilifu fedha zote zinazopangwa za kutekeleza afua za lishe na kusimamia ubora wa taarifa ili taarifa zinazoletwa katika ngazi za juu ziwe zinaakisi uhalisia katika jamii.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa mkutano wa tathimini ya mkataba wa lishe na kutambulisha mpango wa taifa wa uwekezaji katika afya ya mama na matoto nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa Jiji - Dodoma kuanzia tar 30 - 31 Agosti,2024.

Pia amesema kwa Shule za bweni zinazopata fedha kwaajili ya chakula ni vyema kuhakikisha chakula kinachutumika mashuleni ni kile kilichoongezewa virutubishi na ameelekeza wazabuni wa chakula shuleni kupeleka chumvi yenye madini joto,unga na mafuta ambayo hayameongezwa virutubishi.
Snapinsta.app_457235445_18341997865193701_2394551881124032900_n_1080.jpg

Snapinsta.app_457621982_18341997895193701_3320956113664060163_n_1080.jpg
Pia amewataka kusimamia ubora wa huduma za Afya na kutokomeza kabisa malalamiko ya wananchi dhidi ya ubora wa huduma na vitendo vingine vinavyochonganisa Serikali na wananchi na kukamilisha ujenzi na ukarabati wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya.

Kwa upande wa Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya kujipanga kutoa elimu kuhusu bima ya afya kwa wote na kuhakikisha wanafanya kampeni ya mtu ni afya ili kuondoa magonjwa ya mlipuko hasa magonjwa ya kipindupindu.

“Kwa uwekezaji ambao umefanywa na serikali katika utoaji wa huduma za afya tukishindwa kukiondoa kipindupindi tutakuwa hatujitendei haki sisi watanzania.”

“Pia twendeni tukapambane tukahakikishe uonjwa wa homa ya nyani hauingii ndani ya nchi yetu, tukishakosea kidogo na ugonjwa ukaingia nchini madhara tutakayopata ni makubwa na kuundoa inaweza kuwa kazi ya ziada."

Pia soma:
~ Shule ya Msingi na Sekondari Goba Mpakani zinawarudisha nyumbani na kuwachapa wanafunzi wasio na hela ya chakula
~ Bunda: Programu ya chakula Shule ya Sekondari Mwibara ina shida
~ Je, umewahi kutoa pesa ya mchango kwaajili ya huduma ya chakula cha mchana shuleni kwa mwanao?
 
Kuhusu chakula ni jambo jema Sana Ila wazazi washirikishwe maana baadhi ya wazazi hugoma kutoa Hela ya chakula kwa watoto wao.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kuhakikisha wanafunzi walio katika shule zote za kutwa za umma na binafsi wanapata chakula bila kujali ni wa madarasa ya mitihani ama lah na kamati za shule ziimarishe usimamizi wa chakula kinachotolewa na wazazi kwa ajili ya mpango wa chakula shuleni.
Pia amewataka kuendelea kusimamia kikamilifu fedha zote zinazopangwa za kutekeleza afua za lishe na kusimamia ubora wa taarifa ili taarifa zinazoletwa katika ngazi za juu ziwe zinaakisi uhalisia katika jamii.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa mkutano wa tathimini ya mkataba wa lishe na kutambulisha mpango wa taifa wa uwekezaji katika afya ya mama na matoto nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa Jiji - Dodoma kuanzia tar 30 - 31 Agosti,2024.

Pia amesema kwa Shule za bweni zinazopata fedha kwaajili ya chakula ni vyema kuhakikisha chakula kinachutumika mashuleni ni kile kilichoongezewa virutubishi na ameelekeza wazabuni wa chakula shuleni kupeleka chumvi yenye madini joto,unga na mafuta ambayo hayameongezwa virutubishi.
Pia amewataka kusimamia ubora wa huduma za Afya na kutokomeza kabisa malalamiko ya wananchi dhidi ya ubora wa huduma na vitendo vingine vinavyochonganisa Serikali na wananchi na kukamilisha ujenzi na ukarabati wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya.

Kwa upande wa Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya kujipanga kutoa elimu kuhusu bima ya afya kwa wote na kuhakikisha wanafanya kampeni ya mtu ni afya ili kuondoa magonjwa ya mlipuko hasa magonjwa ya kipindupindu.

“Kwa uwekezaji ambao umefanywa na serikali katika utoaji wa huduma za afya tukishindwa kukiondoa kipindupindi tutakuwa hatujitendei haki sisi watanzania.”

“Pia twendeni tukapambane tukahakikishe uonjwa wa homa ya nyani hauingii ndani ya nchi yetu, tukishakosea kidogo na ugonjwa ukaingia nchini madhara tutakayopata ni makubwa na kuundoa inaweza kuwa kazi ya ziada."
Ni wazo zuri, lakini chakula hicho kitatoka wapi? Wazazi wote Wana uwezo huo wa kugharamia upatikanaji wa chakula?
 
Ni aibu kama taifa suala la chakula kwa wanafunzi ni suala la kujadili miaka hii!

Miaka 63 ya Uhuru na 60 ya Muungano tunajadili ugali kwa wanafunzi?

Tusipoweza kuwalisha tuliowazaa tutaweza nini? Basi tusizae!
 
Kuwe na muongozo pia wa aina ya chakula cha kuwapa hao watoto na sio tunazungumzia lishe halafu tunaenda kuwapa watoto UGALI NA MAHARAGE.

Kuwe na menu kabisa, mtoto wa lakwanza mpaka lanne ale chakula gani asubuhi na mchana, mtoto wa latano mpaka lasaba ale nini.

Unapozungumzia lishe unazungumzia samaki, matunda, mboga za majani, nyama nk tusije kuwalisha DONA NA UBWABWA watoto.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kuhakikisha wanafunzi walio katika shule zote za kutwa za umma na binafsi wanapata chakula bila kujali ni wa madarasa ya mitihani ama lah na kamati za shule ziimarishe usimamizi wa chakula kinachotolewa na wazazi kwa ajili ya mpango wa chakula shuleni.
Siyo rahisi kiasi hicho
Makosa yako katika planning, baadhi ya shule zinajengwa tens of Kilometres away kutoka makazi ya watu bila kufikiria usafiri, huduma za maji, umeme na miundombinu ya kuzifikia na uwezo wa wazazi kulipia gharama za chakula na usafiri matokeo yake ndiyo haya
 
Kuwe na muongozo pia wa aina ya chakula cha kuwapa hao watoto na sio tunazungumzia lishe halafu tunaenda kuwapa watoto UGALI NA MAHARAGE.

Kuwe na menu kabisa, mtoto wa lakwanza mpaka lanne ale chakula gani asubuhi na mchana, mtoto wa latano mpaka lasaba ale nini.

Unapozungumzia lishe unazungumzia samaki, matunda, mboga za majani, nyama nk tusije kuwalisha DONA NA UBWABWA watoto.
Ni wazo zuri sana lakini tusibase kwenye shairi la "Eat More the Slogan says"

Mie nadhani tuanze kwanza kwa hatua, Ugali maharage upatikane kwanza then baadae tufuatie hatua hiyo uwiwazayo.
(Direction is more important than speed).

Asante
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kote nchini kuhakikisha wanafunzi walio katika shule zote za kutwa za umma na binafsi wanapata chakula bila kujali ni wa madarasa ya mitihani ama lah na kamati za shule ziimarishe usimamizi wa chakula kinachotolewa na wazazi kwa ajili ya mpango wa chakula shuleni.
Pia amewataka kuendelea kusimamia kikamilifu fedha zote zinazopangwa za kutekeleza afua za lishe na kusimamia ubora wa taarifa ili taarifa zinazoletwa katika ngazi za juu ziwe zinaakisi uhalisia katika jamii.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa mkutano wa tathimini ya mkataba wa lishe na kutambulisha mpango wa taifa wa uwekezaji katika afya ya mama na matoto nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa Jiji - Dodoma kuanzia tar 30 - 31 Agosti,2024.

Pia amesema kwa Shule za bweni zinazopata fedha kwaajili ya chakula ni vyema kuhakikisha chakula kinachutumika mashuleni ni kile kilichoongezewa virutubishi na ameelekeza wazabuni wa chakula shuleni kupeleka chumvi yenye madini joto,unga na mafuta ambayo hayameongezwa virutubishi.
Pia amewataka kusimamia ubora wa huduma za Afya na kutokomeza kabisa malalamiko ya wananchi dhidi ya ubora wa huduma na vitendo vingine vinavyochonganisa Serikali na wananchi na kukamilisha ujenzi na ukarabati wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya.

Kwa upande wa Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama amewaomba wakuu wa mikoa na wilaya kujipanga kutoa elimu kuhusu bima ya afya kwa wote na kuhakikisha wanafanya kampeni ya mtu ni afya ili kuondoa magonjwa ya mlipuko hasa magonjwa ya kipindupindu.

“Kwa uwekezaji ambao umefanywa na serikali katika utoaji wa huduma za afya tukishindwa kukiondoa kipindupindi tutakuwa hatujitendei haki sisi watanzania.”

“Pia twendeni tukapambane tukahakikishe uonjwa wa homa ya nyani hauingii ndani ya nchi yetu, tukishakosea kidogo na ugonjwa ukaingia nchini madhara tutakayopata ni makubwa na kuundoa inaweza kuwa kazi ya ziada."

Pia soma:
~ Shule ya Msingi na Sekondari Goba Mpakani zinawarudisha nyumbani na kuwachapa wanafunzi wasio na hela ya chakula
~ Bunda: Programu ya chakula Shule ya Sekondari Mwibara ina shida
~ Je, umewahi kutoa pesa ya mchango kwaajili ya huduma ya chakula cha mchana shuleni kwa mwanao?
Atuletee hicho chakula sasa. Wananchi wamekuwa wazalendo sana kodi zinatoka kwa wakati, michango shule haijakoma kila kukicha mlundikano wa michango.

Mama katufikia waalimu wanabubujikwa na machozi ya furaha kwa mishahara minono na marupu rupu kibao

Mama samia mitano tena
 
Back
Top Bottom