Mchepuko unakaribia kuvunja ndoa yangu

Mchepuko unakaribia kuvunja ndoa yangu

Ni waathirika wapya 72,000 kila mwaka sawa na watu 200 kila siku, jitahidi kujiondoa kwenye hiyo list kila siku.
 
Michepuko mna nini lakin? Wakuu ninaandika kwa masikitiko na majonzi makubwa saana. Nimeoa takribani miezi Tisa sasa. Kama mjuavyo kwetu sisi wanaume hatuachi kuchepuka ikiwa ndo asili na hulka yetu.

Namshukuru Mungu,nimebahatika kupata mwanamke mzuri,mwenye upendo na pia Ni mcha Mungu. Tatizo ni huyu mchepuko niliye naye,anani control mnooo.Yaan ananifanyia visa sijapata kuona.

Inafikia nyakati Mke wangu simjali Wala kumheshimu tena,najikuta nguvu zote nazielekeza kwa mchepuko. Na mbaya Zaid mchepuko ananipeleka vile anavyo jisikia,namfanyia Mambo mengi kuliko hata ninayo yafanya kwenye familia yangu,

Lakini naambulia matokeo hasi kutoka kwa huyo mchepuko. Mchepuko anaweza kunihitaj hata saa tano usiku,ntajikuta nmedanganya kwa wife ili tu niweze kutoka.

Kuna nyakati mchepuko atanifanyia vitimbi na vibweka kiasi kwamba napoteza kabisa mood ya kazi. Nkirudi nyumbani,mke wangu namdanganya then atanifariji na kunitia nguvu na maisha yanaendelea.

Imefikia hatua nataka niachane kabisa na mchepuko,nashindwa kabisa yaan.ntampotezea Leo lakini kesho ntamtafuta Tena Bila kujali madhila anayo nifanyia.

Nimechoshwa na hii Hali wakuu,natamani kujinasua katika hii Hali ninayo pitia. Nahitaji kujikita kwenye familia yangu. Kinacho niumiza zaidi naweza kukaa hata wiki sijapiga game nyumbani,ila nataka kupiga tu game na mchepuko.

Mke wangu anakuwa mnyonge mnoo. Najutia saana kuwa na mchepuko,najitahid kutafuta njia nzuri ya kutoka na hatimaye kuacha kabisa.

Ushauri wangu kwa vijana wenzangu ambao mmeoa. Kama unaweza please tulia na mke wako ili usipitie Hali ambayo naipitia.

Nb:Mke wangu Ni mzuri na ametimia kila idara kuliko hata mchepuko.

Cc Extrovert
Ni kujiendekeza tu mkuu
 
Mkuu hapo si bure itakua unapewa mnduku tu a.k.a JICHO. kama nihilo hulaumiki Zaidi ya tukupe pole kwa mitihani
 
Bado humpendi mke wako kama unakaa week hupigi show unamtaka mchepuko hapo unadanganya umma
 
Nyumba ndogo nina watoto nina mke na nina maza/
Cha ajabu nkipata mtonyo tu nakuwaza/
Raha tunapata wote ila nina toa changu/
Na unapokea bila ya huruma na ndoa yangu/
Unanivua koti, unanipa maji, unanipa majina ya kifalme unanipa hadhi/
Unanipa masaji, unanipa kazi ambayo hata nyumba kubwa huwa hainipagi/
Kutwa nne sita kwa sita unajipinda/
Nisikuzoee kila nikija mitindo mipya/
Mingine ya kitanga na kichina/
Nalia kama mtoto mpaka nashindwa kutaja jina/

NYUMBA NDOGO BY DIZASTA VINA

Mkuu anza Kufatilia Hip hop kuanzia leo
Hiyo mitindo mipya anjifunza kwa wanaume wenzio halafu anakuja kuku uzia wewe, na unakenua mpaka pengo lako linaonekana [emoji23], kumbuka huwa yanamwisho hayo!
 
Hizi jumbe nyingine hata hazina maana, mwanaume hamheshimu mke wake, ndio maana ana mchepuko, iweje mchepuko uwe na heshima kwa huyo mke?
sio kila anaechepuka ni kukosa heshim kwa mkewe.
 
Bro baki na mkeo dhambi unayotengeneza itawatesa watu wengine ambao haiwahusu
 
Back
Top Bottom