Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258

MCHEZAJI chipukizi wa timu ya vijana ya Coastal Union ya Tanga, amefariki dunia jioni ya Jumamosi baada ya kuanguka Uwanja wa Mkwakwani kufuatia kugongana na mchezaji na mwenzake.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Coastal Union dhidi ya uliotangulia kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Coastal na Mwadui FC ya Shinyanga uliomalizika kwa sare ya 0-0.
Taarifa zinasema mchezaji huyo aligongana mwenzake kabla ya kuanguka na kupoteza fahamu, kasha kukimbizwa hospitali ya Bombo, ambako umauti ulimfikia.