Mchezaji gani aliyefariki ulikuwa unamkubali sana?

Namkumbuka saana mshambuliaji hatari wa Gungu Rangers ya kigoma mbaluku kubaza huyu mwamba alifunga Goli 23 kwenye mechi 6 za ligi ya ng'ombe huko kigoma Alifariki mwaka 2008 huko Tanzania military academy (alijiunga na jeshi akafia mafunzoni)
 
Lissu
 
Hamis thobias gaga
Ulikuwa kwenye akili yangu mkuu,,

Huyu jamaa hadi sasa sijaona mchezaji wa kitanzania,,
Kiungo wa aina yake..

--Mguu sumaku,,
--Pasi za macho,
--Mpira anahamisha upande mmoja kwenda mwingine.

Enzi zake akikutana na Athuman China wa yanga,,
Burudani kabisa dimbani..
 
Kwa soka la nyumbani ni hawa :
1.Edward Chumila.(Simba)
2.Said Mwamba 'kizota' (Yanga)
3.Hamis Gaga (Simba, Volcano, Yanga,)
4.Ramadhani Lenny (Simba)
5. Willy Mwaijibe (Simba)
6.Athumani Juma Chama (Yanga)
7.Joseph Katuba (Yanga, Simba)
8.Juma Mkambi Jenerali (Yanga)
9. Method Mogella (Simba, Yanga)
10. Seif Hassan Majebella ( Berlin FC, Temeke)
 
Nani anamkumbuka Machepe?mtangazaji wa radio Tz alisema haya pale alipofunga Simba against Yanga"Machepe anaichepea Yanga" ... alikuwa na umri mdogo , kipaji kikubwa lakini ndio hivyo mchezaji huyo aliyekuwa kipenzi Simba akapotea na kufariki mapema.
Duh sikujua kama Machepe ni marehemu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…