Huwa nikisema kuwa huko Yanga SC kuna ' Njaa Kali ' tena kuliko hata Wanachama na Mashabiki wake wanavyoaminishwa kuna Watu huniona GENTAMYCINE nasema Uwongo au Nazusha tu na nina Chuki na Yanga SC. Sasa nawaomba na leo wale wana Yanga SC waliojazana hapa JamiiForums waje waibishie na hii taarifa iliyotolewa na hili Gazeti la Mtanzania ambalo tena kwa Kuwasadia tu ni kwamba Mwandishi wa hiyo Habari pamoja na Mhariri wake ni wana Yanga SC watupu ila wameamua kuweka kando ' Unafiki ' wao na Kueleza ukweli.
Kama Mchezaji muhimu na Mwandamizi Kelvin Yondan anakosa Mazoezi kwasababu tu ya ' Chai ' vipi kwa Wachezaji wengine ' Wachanga ' kama akina Abdallah Makame na Paul Godfrey?