Mchezaji wa NBC Premier League atakayewafanya akina Bangala, Aucho na Mayele watembelee 'Magongo' kwa Mechi zilizobakia ana Zawadi yangu Nono sana

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Niliwaamini akina Abdi Banda wa Mtibwa Sugar FC, Kelvin Yondan wa Geita Gold FC na huyu Bwege wa juzi Andrew Vicent wangenifanyia vyema hii Kazi yangu Maalum kumbe ndiyo Kwanza wakawa Wanawachekea tu mpaka hata Kuwazawadia Magoli ya Michongo na sasa hatukai kwa Amani hapa Mjini.

Natamani mno Umri wangu urejee na nicheze Mpira (Fabo) hasa zile namba zangu za Beki Mbili au Beki namba Nne au Kiungo cha Chini (Ukabaji) ili niwaonyeshe hawa Wachezaji wa sasa (Wadogo zangu) jinsi ya Kumalizana Ki Roho Mbaya na Watu kama Bangala, Aucho na Mayele.

Na hakuna Mchezaji mwepesi kama ukiwa na PhD ya Kucheza Rafu Kali (ila za Kiufundi) wa kumpeleka haraka ICU au Muhimbili kwa Bibi Cheza akaanze Mazoezi yake ya Viungo kama Mchezaji Fiston Mayele.

Yaani anawafunga na bado anawatusi?
 
Mpira ni Amani,mpira ni kazi,sasa kumuombea au kutaka Binadamu mwenzako avunjwe mguu kisa Tu mahaba yako Kwa team Fulani nafikiri si sahihi,Ile siyo Vita mkuu,ni mchezo Tu...Let enjoy the football.
 
hahahahahaah!kawatukanaje tena mkuu>??
 
Wewe unasifia kiwango cha wachezaji wa timu ile inayoweza kwa Mkapa tu. Lakini kumbe una hofu na wachezaji wa timu nyingine ambao wana viwango unavyovikubali kimya kimya ambao unataka wawe vilema ili wachezaji wa kwa Mkapa wapate urahisi
 
Subiri upigwe BAN Tena,unahubiri chuki na kuumizana michezoni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…