KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nakumbuka kuna Mwaka niliwahi shiriki Ligi ya Wilaya sehemu fulani wakati ule nilikuwa na miaka 25 lakini Vyeti tulivoletewa na vilikuwa na majina yetu na usajili sahihi kabisa wa kutoka kwenye bodi husika nilisomeka nina miaka 17.
 
Mwamba kazingua huwezi mjibu hivyo rafiki yako mwamba alitaka chochote kitu kwenye swala la kubadili jina kurudi ndio mtiti ulipo sasa kesi kule NIDA na sheria iko wazi kutoa taarifa za uongo kuna faini na kufungwa jera cha msingi wayamalize wao kwa wao wasifike huko maana wote wamekiuka sheria
 
Nakumbuka kuna Mwaka niliwahi shiriki Ligi ya Wilaya sehemu fulani wakati ule nilikuwa na miaka 25 lakini Vyeti tulivoletewa na vilikuwa na majina yetu na usajili sahihi kabisa wa kutoka kwenye bodi husika nilisomeka nina miaka 17.
Wewe hujui kuna umri wa uwanjani na kuna umri wa mtaani ni vitu viwili tofauti unaweza kuamini kuwa sele gomez anamiaka 20 kweli? Hahahaha
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani TFF ilivyo dhaifu mpaka mchezaji anatumia nyaraka za kughushi na anacheza Ligi Kuu Yenyewe haina habari. Hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya wahusika wote. NI AIBU
Mkuu hadi bunge lako linawatu wana nyaraka kibao za kughushi nabado wapo kule na sio hao tu kuna wakuu wa Idara kibao tena sehemu nyeti wako na nyaraka hizo..Au umesahau ya Mkuu wa Kaya.?


We unadhani kwanini Magu alianza na issue ya dizain hii mapema tu alipoingia ofisini.,?
 
Umemwaga mboga ila ugali utakapomwagwa ujue na wewe kwishnei babuji..
Na mimi kama shabiki wa Simba na mtanzania mzalendo :AlienPls: nataka sheria ifuate mkondo ,,,, wewe na yeye wote ni wahalifu mwende jela mkalipe mlichopanda kama ni kweli hili limefanyika..

  • Kifungu cha 337 Penal Code (Cap. 16) “Mtu yeyote anayegushi nyaraka yoyote anatenda kosa la felony na anaweza kufungwa hadi miaka 7.”
  • Kifungu cha 338 Penal Code (Cap. 16) Kama nyaraka ni rasmi (cheti cha kuzaliwa, rekodi ya mahakama, hati ya ardhi, n.k.), adhabu inaweza kufikia kifungo cha maisha.
  • Kifungu cha 22–24 Penal Code (Cap. 16) Wale wanaoshiriki, kusaidia au kuruhusu kosa (aiding and abetting) wanahesabiwa pia kama wahusika wakuu.
  • Kifungu cha 22–24 → Aiding and abetting: yeyote anayesaidia au kushiriki katika kosa anahesabiwa kama mhusika mkuu na adhabu ni sawa na ya aliyefanya kosa.

  • Mchezaji (Kakoti)
    • Anaweza kushitakiwa kwa kutumia nyaraka za kughushi na kujipatia faida kwa utambulisho wa uongo.
    • Adhabu: kifungo cha miaka 7–maisha kulingana na nyaraka.
  • Kameta (aliyetoa cheti)
    • Anaweza kushitakiwa kwa kusaidia kosa (aiding and abetting).
    • Adhabu: kifungo sawa na mhusika mkuu (hadi miaka 7 au zaidi).
Hawa ni vijana hawatakiwi kufika huko as long as inahusisha mpira na si mambo ya kitaaluma .
Mambo yaishe juu juu tu kwa busara za watu wazima au wazee.
Kupeleka Hawa vijana jela tena ni ujinga wakati kuna mafisadi wanakunja nne tu kwa kutafuna rasimali za tanzania
 
Mimi sitakubali! Hata mimi nina jina la mtu tulibadilishana lakini la kwangu nikaenda nikaongezea u-bin mwingine! Sasa wakinifuata nawauliza wa kwenu alikuwa anaitwa nani? Wanaishia kutaja la kwanza na la kati wakifika kwenye surname wanakwama!
Watoto wako wanatumia majina yako mapya au ya zamani?
 
Shauri yake , Anajiona kajipata so anamkataa jamaa 😆😆

Huwenda alimpa ahadi kwamba akitusua atamshika mkono

Ilitokea hivyo Kwa 2face alikuwa mshikakaji mkubwa sana wa Emanuel eboue 2face alipokuja kutoboa kimziki Akaanza kumfungia mwenzake vipo yaani full madharau

Mungu sio athumani Emanuel akatoboa na kwenda kucheza Chelsea akawa star mkubwa kuliko 2face na Hela kibao , to good enough Emmanuel kutokana na ushawishi wa umaarufu wake akaoa mtoto wa bilinear now wana mihela kibao ,

Ushkaji wa watu wawili ambao bado wapo kwenye kipindi Cha kujitafuta unakuwaga wa kinafki sana mmoja anapo tangulia kuanza kupata
Eboue kacheza Chelsea ipi tena mkuu?
 
Naitwa David Frank Kameta, baada ya kupata wakati mgumu muda mrefu ikiwepo kusalitiwa na mtu ambaye nilimuamini, sasa naona ni bora Dunia ijue kinachoendelea. Hapa nazungumzia usaliti wa rafiki yangu Emmanuel Robert Kakoti jina lake maarufu wengi mnalijua, kwa sasa ni mchezaji maarufu katika klabu kubwa katika Ligi Kuu Bara.

Alichukua jina langu kwa makubaliano maalum kuwa atalitumia muda mfupi lakini amenigeuka na kuendelea kulitumia kwa miaka mingi, hataki kurejea katika jina lake halisi huku akinisababishia hasara nyingi na mzozo katika familia yangu.

Stori yetu ipo hivi…
Tuliishi pamoja Mbeya, tulisoma wote ingawa alikuwa mbele yangu darasani, mimi umri wangu ni miaka 32 (nilizaliwa 1994), yeye mwenzangu alianza kucheza mpira tukiwa wadogo, hayo hayakuwa mambo yangu.

Mwaka 2017 au 2018 (sikumbuki vizuri), Emmanuel akiwa timu ya Mbeya City alionyesha utovu wa nidhamu, uongozi ukamfungia usajili pamoja na kufungiwa kutumia majina yake yote halisi kwenye soka. Hiyo ilimfanya aonekane kama amefutwa kwenye Ulimwengu wa soka.

View attachment 3657241
Kikosi cha Mbeya City cha Msimu wa 2017/2018 ambacho Emmanuel Robert Kakoti alikuwepo (jina la nne kutoka juu).​

Kuna siku ilikuwa deadline ya usajili, Emmanuel aliniomba, "Mwanangu, usajili unafungwa leo na nimekosa nafasi, naomba nisaidie cheti chako cha kuzaliwa nitumie kwenda Mbeya Kwanza. Nikianza tu kucheza, nitabadilisha jina kwenye leseni na kurudisha jina langu halisi."

Sababu ya urafiki na huruma, nilimpa cheti changu, akafanikiwa kusajiliwa Mbeya Kwanza kwa jina langu la David Frank Kameta. Aliendelea na maisha yake ya soka katika timu ya Lipuli ya Iringa, lakini ilikuwa ni kinyume na ahadi yetu, hakubadilisha jina hilo. Nilimsisitiza kuwa anatakiwa kurejea katika jina lake halisi lakini aligoma.

Aliposajiliwa katika timu yake ya sasa ya Kariakoo, akaanza kunikwepa, akawa ananipa majibu ya mkato. Huku nyuma mimi nikaingia katika mgogoro wa kifamilia wakiniambia nimeuza jina.

View attachment 3657258
Document yangu ya TRA

View attachment 3657260
Cheti changu cha kuzaliwa​

Baada ya msiba wa mzee wangu, familia ilikaa kikao na kunisema sana, nilipompigia simu Emmanuel mbele ya familia hakupokea. Nilituma ujumbe kumtaka ache kutumia jina langu, alinijibu kwa dharau: "Fata sheria yoyote, mimi siachi kulitumia."

Nilipofuatilia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Pasipoti, nilikuta mfumo unaonyesha uwepo wa watu waliofungamana japokuwa yeye aliandika amezaliwa Mwaka 2000 au 2001.

Hali hiyo imeniletea athari kubwa sana kiakili na kisheria kwani jamii inaamini niliuza utambulisho wangu na kuna fursa kadhaa nimezikosa kwa sababu yake, nimeamua kuandika hapa baada ya kuona uungwana wangu umeniponza na mtu ananiletea dharau.
Nenda kwa timu anayochezea umueleze meneja a mpaka z.
 
Ila najaribu kufikiria Duchu ndo rafiki yako ulimsaidia na kafanikiwa kiasi hiki halafu wewe upo huna ishu, unakula vumbi la mbeya huna hata buku 2000 ya kula.. Unamcheki Duchu akusaidie hata buku teni ukanunue dakaa na unga watoto wale ndo kwanza hapokei simu na meseji hajibu na mwisho anaku block kabisa... Lazima nimlipue kama alivyomlipua mshkaji hata kama sitamuharibia basi walau afadhaike na apate sress kidogo.
😄😄😄 It's hurting
 
Back
Top Bottom