KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
😄😄😄 It's hurting
Kweli mkuu japo sio lazima kwake akusaidie lakini kibinadamu inaumiza sana... ndo maana tunaambiwa unapotoa msaada usi-expect chochote kwa uliyemsaidia.. unakuta kweli huku expert chochote lakini unakuta imefika stage kwenye maisha umekosa hata buku 2000 ununue dagaa za watoto wale ila mshakaji akashindwa kukusev Kweli.
 
Kuna wachezaji wengi wanatumia majina feki na umri pia feki....!! Wachezaji wengi wa kibongo wanaodai kuwa na miaka 20-29 kiuhalisia wana miaka 35 kwenda mbele.

Huwa nacheka sana nikiona wachezaji ambao tuliwatumia kwenye timu za ndondo mitaani miaka ya 2012-2016 wakisema kuwa sasa hv wana miaka 24-26....Wakati tunawachukua kwenye ndondo walikuwa na miaka isiyopungua 25.

Huyo duchu ni mzee mimi nilidoubt performance yake kitambo sana. Haya ukweli umetoka kumbe ana miaka isiyopungua 34.

Nenda mahakamani ukapate haki yako.
 
Mi naona kuna ishara za wivu na tamaa , ulimpa jina mwenyewe hukumpa kipaji, unadai unaathirika embu elezea vizuri kama sio ndugu zako wanataka mgao na wao… kama mwanao malizana nae kama mlivyoanza acha Tamaa
Huwezi kumhukumu kwa hisia zako .
Lazima
Mwamba kazingua huwezi mjibu hivyo rafiki yako mwamba alitaka chochote kitu kwenye swala la kubadili jina kurudi ndio mtiti ulipo sasa kesi kule NIDA na sheria iko wazi kutoa taarifa za uongo kuna faini na kufungwa jera cha msingi wayamalize wao kwa wao wasifike huko maana wote wamekiuka sheria
Aliyezingua ni duchu,mtoa mada hana cha kupoteza kama ilivyo kwa Duchu.

Kumbuka lazima kuna ahadi waliwekeana kama washikaji....na aliyetangulia kuvunja makubaliano ni duchu.

Sioni haja ya kumlaumu mtoa mada kwani ni wangapi wenye vipaji lakini hawana njia za kutokea.
 
Naitwa David Frank Kameta, baada ya kupata wakati mgumu muda mrefu ikiwepo kusalitiwa na mtu ambaye nilimuamini, sasa naona ni bora Dunia ijue kinachoendelea. Hapa nazungumzia usaliti wa rafiki yangu Emmanuel Robert Kakoti jina lake maarufu wengi mnalijua, kwa sasa ni mchezaji maarufu katika klabu kubwa katika Ligi Kuu Bara.

Alichukua jina langu kwa makubaliano maalum kuwa atalitumia muda mfupi lakini amenigeuka na kuendelea kulitumia kwa miaka mingi, hataki kurejea katika jina lake halisi huku akinisababishia hasara nyingi na mzozo katika familia yangu.

Stori yetu ipo hivi…
Tuliishi pamoja Mbeya, tulisoma wote ingawa alikuwa mbele yangu darasani, mimi umri wangu ni miaka 32 (nilizaliwa 1994), yeye mwenzangu alianza kucheza mpira tukiwa wadogo, hayo hayakuwa mambo yangu.

Mwaka 2017 au 2018 (sikumbuki vizuri), Emmanuel akiwa timu ya Mbeya City alionyesha utovu wa nidhamu, uongozi ukamfungia usajili pamoja na kufungiwa kutumia majina yake yote halisi kwenye soka. Hiyo ilimfanya aonekane kama amefutwa kwenye Ulimwengu wa soka.

View attachment 3657241
Kikosi cha Mbeya City cha Msimu wa 2017/2018 ambacho Emmanuel Robert Kakoti alikuwepo (jina la nne kutoka juu).​

Kuna siku ilikuwa deadline ya usajili, Emmanuel aliniomba, "Mwanangu, usajili unafungwa leo na nimekosa nafasi, naomba nisaidie cheti chako cha kuzaliwa nitumie kwenda Mbeya Kwanza. Nikianza tu kucheza, nitabadilisha jina kwenye leseni na kurudisha jina langu halisi."

Sababu ya urafiki na huruma, nilimpa cheti changu, akafanikiwa kusajiliwa Mbeya Kwanza kwa jina langu la David Frank Kameta. Aliendelea na maisha yake ya soka katika timu ya Lipuli ya Iringa, lakini ilikuwa ni kinyume na ahadi yetu, hakubadilisha jina hilo. Nilimsisitiza kuwa anatakiwa kurejea katika jina lake halisi lakini aligoma.

Aliposajiliwa katika timu yake ya sasa ya Kariakoo, akaanza kunikwepa, akawa ananipa majibu ya mkato. Huku nyuma mimi nikaingia katika mgogoro wa kifamilia wakiniambia nimeuza jina.

View attachment 3657258
Document yangu ya TRA

View attachment 3657260
Cheti changu cha kuzaliwa​

Baada ya msiba wa mzee wangu, familia ilikaa kikao na kunisema sana, nilipompigia simu Emmanuel mbele ya familia hakupokea. Nilituma ujumbe kumtaka ache kutumia jina langu, alinijibu kwa dharau: "Fata sheria yoyote, mimi siachi kulitumia."

Nilipofuatilia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Pasipoti, nilikuta mfumo unaonyesha uwepo wa watu waliofungamana japokuwa yeye aliandika amezaliwa Mwaka 2000 au 2001.

Hali hiyo imeniletea athari kubwa sana kiakili na kisheria kwani jamii inaamini niliuza utambulisho wangu na kuna fursa kadhaa nimezikosa kwa sababu yake, nimeamua kuandika hapa baada ya kuona uungwana wangu umeniponza na mtu ananiletea dharau.
Aisee kuna watu wanaishi na siri nzito mioyoni mwao! Kwa ushahidi huu, nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kama umeleta taarifa ya uongo! Sema tu kuna makosaa umefanya kutokana na kukosa elimu ya uraia.

Hata mimi miaka hiyo kuna dogolasi wangu wa heshima aliomba nimpatie cheti changu cha kidato cha nne ili akasomee ualimu, nikamkatalia. Magufuli alipofanya uhakiki wa vyeti, nikakumbuka kingenilamba.

Kwa hiyo Duchu ana miaka 30+ lakini kwenye cheti na hati ya kusafiria anaonekana amezaliwa 2000/2001!! Kazi kweli kweli.

Ndiyo mambo yale yale eti Selemani Mwalimu ana miaka 20! Emmanuel Okwi amestaafu na miaka 33! 😆
 
Basi ndo kishamlamba tena kwa ushamba wake anaweka vyeti tin mpaka na picha kabisa kama anamtumia babaake kudadadeki kumbe analichonga kaburi lake mwenyewe ngoja wanayanga waamke walivalie njuga ataelewa athari zake soon, maana sababu inaonekana alitaka amfanye mwenzie kitega uchumi mwenzake amemchomolea may be kwa kuchoka kwa vizinga
Mbona Sospeter Bajana aliyekuwa akitumia jina la Bryson Rafael hakufungwa wala kupotezwa!! Aliendelea kucheza Azam Fc na msimu uliopita akajiunga na JKT Tanzania kama sijakosea.

Kilichotokea kwenye hili sakata ni ukosefu wa uelewa au elimu ya uraia ambapo kisheria ni kosa kumpa mtu nyaraka ambazo siyo za kwake, na kuzitumia kwenye kufoji taarifa zake.
Kama wale watumishi wa umma waliofoji vyeti hawakufungwa kipindi kile; busara hizo hizo zitumike kwenye hili tukio.

Emmanuel Kakoti aka Duchu (David Kameta fake) amrudishie tu mwenzake cheti na jina lake ili maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom