KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Naitwa David Frank Kameta, baada ya kupata wakati mgumu muda mrefu ikiwepo kusalitiwa na mtu ambaye nilimuamini, sasa naona ni bora Dunia ijue kinachoendelea. Hapa nazungumzia usaliti wa rafiki yangu Emmanuel Robert Kakoti jina lake maarufu wengi mnalijua, kwa sasa ni mchezaji maarufu katika klabu kubwa katika Ligi Kuu Bara.

Alichukua jina langu kwa makubaliano maalum kuwa atalitumia muda mfupi lakini amenigeuka na kuendelea kulitumia kwa miaka mingi, hataki kurejea katika jina lake halisi huku akinisababishia hasara nyingi na mzozo katika familia yangu.

Stori yetu ipo hivi…
Tuliishi pamoja Mbeya, tulisoma wote ingawa alikuwa mbele yangu darasani, mimi umri wangu ni miaka 32 (nilizaliwa 1994), yeye mwenzangu alianza kucheza mpira tukiwa wadogo, hayo hayakuwa mambo yangu.

Mwaka 2017 au 2018 (sikumbuki vizuri), Emmanuel akiwa timu ya Mbeya City alionyesha utovu wa nidhamu, uongozi ukamfungia usajili pamoja na kufungiwa kutumia majina yake yote halisi kwenye soka. Hiyo ilimfanya aonekane kama amefutwa kwenye Ulimwengu wa soka.

View attachment 3657241
Kikosi cha Mbeya City cha Msimu wa 2017/2018 ambacho Emmanuel Robert Kakoti alikuwepo (jina la nne kutoka juu).​

Kuna siku ilikuwa deadline ya usajili, Emmanuel aliniomba, "Mwanangu, usajili unafungwa leo na nimekosa nafasi, naomba nisaidie cheti chako cha kuzaliwa nitumie kwenda Mbeya Kwanza. Nikianza tu kucheza, nitabadilisha jina kwenye leseni na kurudisha jina langu halisi."

Sababu ya urafiki na huruma, nilimpa cheti changu, akafanikiwa kusajiliwa Mbeya Kwanza kwa jina langu la David Frank Kameta. Aliendelea na maisha yake ya soka katika timu ya Lipuli ya Iringa, lakini ilikuwa ni kinyume na ahadi yetu, hakubadilisha jina hilo. Nilimsisitiza kuwa anatakiwa kurejea katika jina lake halisi lakini aligoma.

Aliposajiliwa katika timu yake ya sasa ya Kariakoo, akaanza kunikwepa, akawa ananipa majibu ya mkato. Huku nyuma mimi nikaingia katika mgogoro wa kifamilia wakiniambia nimeuza jina.

View attachment 3657258
Document yangu ya TRA

View attachment 3657260
Cheti changu cha kuzaliwa​

Baada ya msiba wa mzee wangu, familia ilikaa kikao na kunisema sana, nilipompigia simu Emmanuel mbele ya familia hakupokea. Nilituma ujumbe kumtaka ache kutumia jina langu, alinijibu kwa dharau: "Fata sheria yoyote, mimi siachi kulitumia."

Nilipofuatilia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Pasipoti, nilikuta mfumo unaonyesha uwepo wa watu waliofungamana japokuwa yeye aliandika amezaliwa Mwaka 2000 au 2001.

Hali hiyo imeniletea athari kubwa sana kiakili na kisheria kwani jamii inaamini niliuza utambulisho wangu na kuna fursa kadhaa nimezikosa kwa sababu yake, nimeamua kuandika hapa baada ya kuona uungwana wangu umeniponza na mtu ananiletea dharau.
Duh! mwana kazingua na hapo kimemlamba
 
Mimi nilisajiria watu laini kitamburisho cha nida, wametoka wakanikazia mwana, mi nikaenda shop zote za laini husika nikapiga panga futa zoote jina😁🤣joking
 
POINT KUBWA HAPA SIO JINA BALI NI DUCHU ALISHAFUNGIWA KUCHEZA MPIRA ukamsaidia kufanya udanganyifu ili atimize ndoto zake.

*asingeweza tena kutumia jina lake halisi.(jina lake na utambulisho wake ulikua umeshachafuka katika soka)

*akakuomba atumie jina lako ili apambanie ndoto zake,ukambles kwa makubaliano Flanflan,,,

*mwamba kavuja jasho kupitia jina(nyota) yako,hatimaye mambo yamemnyookea kiasi.
Akawa bize,konekshen na marafiki wakabadilika.ukaanza kuhisi anakupuuza. Au...

*pengine ulinza kudemand huge na kumtishia kumharibia kwa sababu una siri zake.

*ima kakutana na wajanja wa mjini wakampa ujasiri na maarifa zaidi ya kuhalalisha udanganyifu wenu(wake) na kukukwepa kabisa wewe kisheria.kwamba wewe ni wewe na yeye ni yeye hata kama mnafanana majina.

Ndio maana ana jeuri ya kukwambia nenda popote.ijapo ukienda mtasababishiana matatizo makubwa,hasa kwa jamaa yako.
LAKINI USIFANYE HIVYO.MSIHARIBIANE.

.ila cha msingi bwana imanuel kakoti DUCHU.anatakiwa AKUMBUKE kuwa..
ALIFUNGIWA KABISA KUCHEZA MPIRA.
Basi asikuone kama Fala.akupe heshima yako.maana ulimpa kwa wema.na kiimani,mafanikio hayaletwi tu na kipaji.majina pia hubeba baraka au laana.ndio maana kwa jina lake ALIKATALIWA.Lakini kwa jina jingine mlango ukafunguka.

Nachokushauri wewe muache tub kwanza ipo siku atakumbuka wema wako.japo tayari taarifa hizi tayari atakua amezipata.

Ingawaje kisheria wote mnamakosa.
Ila kiupambanaji kama vijana mlikua sahihi kusapotiana.

Mmekosea,mkakoseana,sameheaneni.

FUTA UZI.
 
Duchu miaka 34,afu akabane na watu wa nje huko kwenye CAF champion league wenye miaka 23 halisi,akimuacha hampati,atacheza rafu tu!Afrika Kila kitu ni laana tu!
 
"Usajili kwa jina lisilo lake ni ukiukaji mkubwa wa uaminifu wa soka. Ikiwa utagunduliwa ndani ya miaka 5, mchezaji (na mara nyingi klabu/chama) anatarajiwa adhabu kali ya faini + kusimamishwa kwa angalau miezi 12."

"Baada ya miaka 5, uwezekano wa mashtaka ya FIFA unapungua sana, lakini athari za mechi zilizochezwa na uamuzi wa chama cha taifa bado zinaweza kutumika. Sheria za chama cha taifa(Nchi) zinaweza kuwa kali zaidi au zinaongezea kanuni za FIFA."
 
Back
Top Bottom