KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwa maoni yangu huyu bwana anastahili kuwa mahakamani muda kwa kosa la kusaidia uhalifu kutendeka. Kumpa mtu cheti cha shule au kuzaliwa ni kosa kisheria, hivyo asione sifa kuwa alimpa Duchu cheti. Kwanza anapaswa kujua cheti hakichezi mpira hivyo asidhani kuwa anaweza kumuharibia kazi Duchu sababu atakosa cheti cha kuzaliwa (kama kweli anatumia cha Mtu).
Ingekuwa anazungumzia cheti cha kitaaluma labda tungeweza kumuona anadai kitu cha maana lakini kama jina David Kameta mbona wanyakusya wengi ni Kameta au David Kameta? Sasa hao wote atawanyang'anya jina lake?
 
Kw Kwa maelezo yake duchu alifungiwa kucheza mpira,ndio sababu ya kutotumia jina lake.

Wote hapo wanamakosa,ila wakifika mbali duchu ndio ataathirika zaid maana huyu mwingine ni kama hana cha kupoteza.
 
ulisahau esau aliuza uzaliwa wake wa kwanza ikawaje
 
Wewe utakuwa hujasoma post yote ukaelewa pengine rudia kusoma mkuu.
 
Tupe mrejesho baada ya kumlipua kuna jitihada zozote za kutaka kuweka mambo sawa?
 
Wewe mleta post una kesi ya kujibu.Halafu kitendo cha kutofautiana mwaka wa kuzaliwa inaonyesha ni watu wawili tofauti na hicho cheti chako ni vile vya zamani,havisomi hata kwenye mfumo wa RITA,yawezekana yeye alishaomba cheti kingine akaomba na NIDA,hiovyo wewe itakua ngumu kudhibitisha kuwa ni kweli ili Duchu awe na kesi ya kujibu.
Bilashaka kwa huu ukimya kwenye huu uzi,unaweza ukawa unaashiria kuwa uko kwenye mikono salama ukihojiwa.
Kama nakuona unavyojuta kujipa kesi ambayo hukuwa na ulazima wakua nayo,pole sana.Hii mitandao tuitumie vizuri.
 
Pitia account ya Facebook na Instagram ya Davidkameta utagundua ukweli kuanzia apo
 
Ndugu yangu endelea tu kupambana na hali yako kwa kuwa kesi kama hizo zipo sana kwa viongozi wa chama tawala.

Labda pengine kwa kuwa tu wewe u mgeni humu jukwaani lakini wapo viongozi maarufu hapa nchini wanahusika na "tradeoff" ya majina yao ya asili.

Yapo majina ya akina Bashite, Maderu, n.k. yenye kutabanaishwa na matumizi ya majina yasiyokuwa ya asili yao. Lakini pia kijana wangu umetumia ID ya "anonymous" wakati huo huo unajimbulisha kwa uwazi kabisa kupitia majina yako yote matatu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…