Kuna mchezo mpya siku hizi kina mama hasa wenye nyumba za kupanga huwa wanawafundisha mabinti wawe wanaingia vyumba vya wapangaji wa kiume kwa gia ya kuomba kuomba kuangalia tv, kuomba kuwafanyia usafi, kuomba kuingiziwa nyimbo au muvi, n.k. (mbinu kibao) sambamba na mitego ya kuwapandisha hamu ya kuwataka kimapenzi.
Mabinti hawa wengine wametolewa vijijini huko, ukiwauliza miaka washafundishwa waseme wana miaka 19 na hawasomi, siku ya tukio utaambiwa wana miaka 16 na wanasoma.
Wakiingia vyumbani, mama mwenye nyumba anastua marafiki zake kama wawili waje, wengine wanaleta kabisa mtendaji wa mtaa ama polisi ambao washanogewa na pesa za huu mchezo mchafu.
Wakiingia ndani humo hupewi hata nafasi ya kujieleza kila mtu anasema umelala na binti mwenye umri chini ya miaka 18, utajieleza kwamba mlikuwa mnacheki tu tv ila wao watakomaa umelala na binti mdogo, utajitetea alikwambia ana miaka 19 hapo utaoneshwa cheti (hata cha mchongo) kazaliwa 2007.
Hapo kuchomoka uwe na zaidi ya laki 3, kama una ka usafiri ama una vaa vizuri na una kazi tegemea kucheua milioni.
Wengine hutumia mbinu hii kuwatupia jela vijana waliopishana nao kauli
Wahanga wengi huwa ni vijana wa kiume chini ya miaka 30 bado wengi hawajakomaa vizuri kuwa na akili za utu uzima na miili huwa ina nguvu sana