Mchezo Mchafu: Kuna kina mama huwatuma mabinti kuingia vyumba vya wapangaji wa kiume, fumanizi la video hufanyika ni aidha utoe pesa ama unaenda jela

Mwenyekiti, mtendaji, wameshindwa wote mpaka DC, duuu.
 
Kabisa mkuu.hata sijui kuwapa watoto pipi nikitu kibaya sana maana ukibambikizwa ushahid upo mtaan unawarubun kwa kutumia pipi.
Tena skuiz awe mtoto wa kike au wakiume usithubutu kuweka nao mazoea ni hatari sana unaeza ukasingiziwa umemfanyia kitu mpaka uchunguzi ukamilike umesota nyuma ya nondo vibaya, hapa napokaa jirani kuna kitwisheni vitoto vinakujaga yani hata wakinisalimia najifanya sijawasikia huyo ndani kwang nafunga geti.
 
Hizo mbinu zao kwangu hazitafanya kazi , maana mimi n kauzu zaidi ya dagaa

Kuna kipind nilipanga sehemu kila mpangaji ana mita yake ya luku sasa ikitokea umeme kwako umekata na huna betri za kile ki remote basi unaweza kuingiza token kupitia kwa mpangaji mwenzako

Bibie kamtuma binti yake aje kuomba kuingiza umeme akili ikaniambia huu mtego nikamtolea extension dirishani nikatemana nae .

Vijana under 30 muusome uzi huu utawasaidia
 
Yaani mtoa maada uko vizuri Nakupongeza sana. Mimi nilihamia mkoa Fulani na nikiwa na mke wangu, Cha ajabu nikiwa siku hiyo mapumziko napenda sana kuakaa nje ya nyumba Kuna mti wa kivuri natulia na kiti changu ikifika jioni natoka kushtua Koo. Sasa Kuna kautaratibu wanawake walikaanza kakupitapita mara Kwa mara na mavazi yasiyofaa, Kwa kuwa ni mgeni nikajua nikawaida yao, sasa kunasiku nipo na kijana mmoja mpangaji mwenzangu nikamcheki kama kachalala na mke wake na mke wangu wamekuwa marafiki sana nikamwambia dogo tutoke Kidogo, tukatulia sehemu kupata Moja mbili. Nikamuuliza huu mtaa wakidada wanapitapita sana bila heshima nikiwa nipo nje au ni utaratibu wao? Dogo akaonyesha mshangao kuwa hujui kaka hawa nilipata taarifa Wanakuvizia wewe kwamba wamekuelewa sana, mtulivu na mcheshi sana hivyo kila mtu anajaribu bahati yake. Nilishtuka sana alafu Cha kushangaza ni wake za watu. Na nyumba jirani Kuna jamaa tunaheshimiana sana ila mkewe anatabia kama hizi akiniona tu anaanza tabia za ajabu na kusogea kuniongelesha na huyu aliwahi kunifata mpaka kanisani wakati sijawahi kuona anaenda kanisani Toka nifike, siku hiyo nilishangaa kumuona mwanae mdogo yupo karibu yangu nikajiuliza huyu kafika na nani? Kutopa jicho nikamuona huyu dada aseee nilishtuka sana na kushangaa kageuka na kujichekesha. Hakika nilimchunia mwanzo mwisho na ikawa mwisho kwake kuwa na mazoea na Mimi. ila nilishalikwepa hili Kwa kutokuwa na mazoea na watu. Mpaka sasa walishaacha tabia ya kupitapita maana msimamo niliuonyesha ni balaa hakuna salamu Wala Nini. VIJANA KUWENI MAKINI SANA MAANA UNAPOANZA KUJITEGEMEA NDIO UMEANZA MAPAMBANO YA MAISHA, HIVYO USIRUHUSU WANAWAKE NA MABINTI WAKUZOEE HOVYO. KUWA NA MSIMAMO NA KUKATAA TOKA MOYONI MAMBO YA HOVYO NDIVYO UNAVYOYAKARIBISHA MAENDELEO YA KUDUMU KATIKA MAISHA YAKO.
 
According to Intelligence strategy hii inaitwa "Counter attack techniques" we mbabe, safi sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kuna mwanangu jumba bovu lilimdondokea mchizi Ana boda take Si unajua kula kwa mama ntilie Hana mke basi akaweka mazoea na binti Wa mama ntilie kilichotokea binti akaambiwa na mama, yake ajitongozeshe wana wakamwambia huku uswahilini huyo maza Si mtu poa mwana katia pamba masikioni Mara binti amletee msosi free Mandela akaona ameula sasa bwana binti akamseti amletee msosi ghetto kwake mwana akaona yes Si unajua boda tena akabonda pombe za vikopo visungura kaiva yuko ghetto anamsubiri mtoto kafika ghetto hatua za kwanza, tuu mtiti mama mtoto wenzake wanne na mwenyekiti Wa mtaa hahaha mwana walimvua laki 4 eti mwanafunzi hiyo shule yenyewe haijui
 
Mkuu hizi huenda ndo mishe zako!!
 
Ni vizuri jifanye nice guy utaamin.
 
Upo zako chumbani umetulia mara ghafla mlango unagongwa ukija mlangoni unakuta Binti kavaa mtandio mwepesi halafu ana bonge la msambwanda, amekuja kuomba chaji huku analegeza sauti..hutoboi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…