Mchezo Mchafu: Kuna kina mama huwatuma mabinti kuingia vyumba vya wapangaji wa kiume, fumanizi la video hufanyika ni aidha utoe pesa ama unaenda jela

Mchezo Mchafu: Kuna kina mama huwatuma mabinti kuingia vyumba vya wapangaji wa kiume, fumanizi la video hufanyika ni aidha utoe pesa ama unaenda jela

Angekuwa mdogo wako au mwanao ndio kafanyiwa hivyo ungeelewa umuhimu wa DC kuwepo hapo, usichokijua ni kwamba huyo jamaa mchezo wa kukigonga hicho kitoto anao muda mrefu na taarifa zilishamfikia mpaka D, akitoka salama akatambike.

Tuviheshimu hivi vibinti chini ya miaka 18 la sivyo vitawatia sana matatizoni.
Mwenyekiti, mtendaji, wameshindwa wote mpaka DC, duuu.
 
Kabisa mkuu.hata sijui kuwapa watoto pipi nikitu kibaya sana maana ukibambikizwa ushahid upo mtaan unawarubun kwa kutumia pipi.
Tena skuiz awe mtoto wa kike au wakiume usithubutu kuweka nao mazoea ni hatari sana unaeza ukasingiziwa umemfanyia kitu mpaka uchunguzi ukamilike umesota nyuma ya nondo vibaya, hapa napokaa jirani kuna kitwisheni vitoto vinakujaga yani hata wakinisalimia najifanya sijawasikia huyo ndani kwang nafunga geti.
 
Hizo mbinu zao kwangu hazitafanya kazi , maana mimi n kauzu zaidi ya dagaa

Kuna kipind nilipanga sehemu kila mpangaji ana mita yake ya luku sasa ikitokea umeme kwako umekata na huna betri za kile ki remote basi unaweza kuingiza token kupitia kwa mpangaji mwenzako

Bibie kamtuma binti yake aje kuomba kuingiza umeme akili ikaniambia huu mtego nikamtolea extension dirishani nikatemana nae .

Vijana under 30 muusome uzi huu utawasaidia
 
Yaani mtoa maada uko vizuri Nakupongeza sana. Mimi nilihamia mkoa Fulani na nikiwa na mke wangu, Cha ajabu nikiwa siku hiyo mapumziko napenda sana kuakaa nje ya nyumba Kuna mti wa kivuri natulia na kiti changu ikifika jioni natoka kushtua Koo. Sasa Kuna kautaratibu wanawake walikaanza kakupitapita mara Kwa mara na mavazi yasiyofaa, Kwa kuwa ni mgeni nikajua nikawaida yao, sasa kunasiku nipo na kijana mmoja mpangaji mwenzangu nikamcheki kama kachalala na mke wake na mke wangu wamekuwa marafiki sana nikamwambia dogo tutoke Kidogo, tukatulia sehemu kupata Moja mbili. Nikamuuliza huu mtaa wakidada wanapitapita sana bila heshima nikiwa nipo nje au ni utaratibu wao? Dogo akaonyesha mshangao kuwa hujui kaka hawa nilipata taarifa Wanakuvizia wewe kwamba wamekuelewa sana, mtulivu na mcheshi sana hivyo kila mtu anajaribu bahati yake. Nilishtuka sana alafu Cha kushangaza ni wake za watu. Na nyumba jirani Kuna jamaa tunaheshimiana sana ila mkewe anatabia kama hizi akiniona tu anaanza tabia za ajabu na kusogea kuniongelesha na huyu aliwahi kunifata mpaka kanisani wakati sijawahi kuona anaenda kanisani Toka nifike, siku hiyo nilishangaa kumuona mwanae mdogo yupo karibu yangu nikajiuliza huyu kafika na nani? Kutopa jicho nikamuona huyu dada aseee nilishtuka sana na kushangaa kageuka na kujichekesha. Hakika nilimchunia mwanzo mwisho na ikawa mwisho kwake kuwa na mazoea na Mimi. ila nilishalikwepa hili Kwa kutokuwa na mazoea na watu. Mpaka sasa walishaacha tabia ya kupitapita maana msimamo niliuonyesha ni balaa hakuna salamu Wala Nini. VIJANA KUWENI MAKINI SANA MAANA UNAPOANZA KUJITEGEMEA NDIO UMEANZA MAPAMBANO YA MAISHA, HIVYO USIRUHUSU WANAWAKE NA MABINTI WAKUZOEE HOVYO. KUWA NA MSIMAMO NA KUKATAA TOKA MOYONI MAMBO YA HOVYO NDIVYO UNAVYOYAKARIBISHA MAENDELEO YA KUDUMU KATIKA MAISHA YAKO.
 
Ahahahahaha.
Mleta mada umenikumbusha mbali sana.
Kuna siku kuna kabint asubh asubh kamekuja nyumban et kanaomba msaada kanateswa kwa boss wake kanataka kurud kwao.Nilikua nimelala bado na ilikua weekend kamvua kananyesha nyesha.Wife kashaamka na watoto pia.
Bas wife akampiga maswali kishenziiiii kisha akaja kuniaamsha et "nimsadie achukue uamuzi gani".

Kwa mujib wa intelijensia ya kichwa changu nikajua kabisa huu ni mtego wife kuna kitu anataka ku confirm kama anachezewa mchezo like kuna kinachoendelea. [emoji23][emoji23] akil mtu wangu ..kwa kuligundua hilo nikatuliza nafsi kisha nikamwambia wife, unataka nifanyaje sasa kama wewe ushamuhoji, ? Akasema na wewe muulize ..
Nikamiuliza jina lake (naona wife anatutazama kwa makin sana asome kitu) .Aliponijib maswal kadhaa nikamwambia wife,
Msaidie ila usimruhusu huy kuondoka kwanza mpigie simu mjumbe aje amhoji kisha amchukue na kama unataka kumsaidia nauli mpe mbele ya mjumbe.
Nikarud ndani nacheeka rohoni. Wanawake bwana!!
According to Intelligence strategy hii inaitwa "Counter attack techniques" we mbabe, safi sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kuna mwanangu jumba bovu lilimdondokea mchizi Ana boda take Si unajua kula kwa mama ntilie Hana mke basi akaweka mazoea na binti Wa mama ntilie kilichotokea binti akaambiwa na mama, yake ajitongozeshe wana wakamwambia huku uswahilini huyo maza Si mtu poa mwana katia pamba masikioni Mara binti amletee msosi free Mandela akaona ameula sasa bwana binti akamseti amletee msosi ghetto kwake mwana akaona yes Si unajua boda tena akabonda pombe za vikopo visungura kaiva yuko ghetto anamsubiri mtoto kafika ghetto hatua za kwanza, tuu mtiti mama mtoto wenzake wanne na mwenyekiti Wa mtaa hahaha mwana walimvua laki 4 eti mwanafunzi hiyo shule yenyewe haijui
 
Kuna mchezo mpya siku hizi kina mama hasa wenye nyumba za kupanga huwa wanawafundisha mabinti kujenga ukaribu na wapangaji wa kiume ili kuingia vyumbani mwao kuangalia tv, kuomba kuwafanyia usafi, kuomba kuingiziwa nyimbo au muvi, n.k. (mbinu kibao) sambamba na kuwafunza mitego ya kuwazuzua kimapenzi. vijana walengwa huwa ni wale wa chini ya miaka 30, wengi bado hawajakomaa vizuri kiutu uzima.

Mabinti hawa wanaotumika kama chambo wengi huwa shule zishawashinda ama watoro waliotukuka, Binti anaweza kuwa na miaka 16 lakini ni mtundu si kidogo, upole wake ni script tu, ashafundishwa akwambie ana miaka 19 akutoe uwoga ila siku ya fumanizi watasema ana miaka 14 na umemlaghai aache kwenda shuleni.

Mpango mzima unakuwa hivi, Kama umekuwa na msimamo hutegeki kimapenzi basi hutumia mbinu zingine kuingia chumbani, mfano binti anakuja kuomba maji ya kumezea panado kichwa kinamuuma, akinywa maji anaomba apumzike nusu saa anaomba apumzike, hapo ndipo mama mwenye nyumba anastua matapeli wenzie wawili watatu waje, wengine wanaleta kabisa mtendaji wa mtaa ama polisi ambao washanogewa na pesa za huu mchezo mchafu.

Wakiingia ndani humo wanarekodi video kwa simu, hupewi hata nafasi ya kujieleza kila mtu anasema umelala na binti mwenye umri chini ya miaka 18, utajitetea kwamba mlikuwa mnacheki tv au alikuwa kapumzika anaumwa lakini haitasaidia, utajitetea alikwambia ana miaka 19 utaoneshwa cheti (hata cha mchongo) kazaliwa 2007 kiufupi hapa upo ndani ya 18 zao!.

Hapo kuchomoka hakuna kiwango maalum, watakukadiria kulingana na hali yako ya uchumi na ufundi wako wa maneno, ila wengi huwa wanachapwa laki 5 hadi 8. Hapo watamalizana kimya kimya, inakuwa siri na ndio maana ni ngumu kukuta habari hizi hadi uwe na ukaribu na wahanga.

kijana hawezi kubaki hio nyumba atahama tu hata kama kabakiza kodi ya miezi minne, muendelezo wa upigaji huu unaendelea kwa wapangaji wapya.

Kwa watu wasio na shida na hela bali kisasi ama kukomoana hutumia mbinu hii kuwatupia vijana jela, kwa wengine binti akiwa mzigo nyumbani hii ndio njia ya ndoa ya mkeka.
Mkuu hizi huenda ndo mishe zako!!
 
Tena skuiz awe mtoto wa kike au wakiume usithubutu kuweka nao mazoea ni hatari sana unaeza ukasingiziwa umemfanyia kitu mpaka uchunguzi ukamilike umesota nyuma ya nondo vibaya, hapa napokaa jirani kuna kitwisheni vitoto vinakujaga yani hata wakinisalimia najifanya sijawasikia huyo ndani kwang nafunga geti.
Ni vizuri jifanye nice guy utaamin.
 
Upo zako chumbani umetulia mara ghafla mlango unagongwa ukija mlangoni unakuta Binti kavaa mtandio mwepesi halafu ana bonge la msambwanda, amekuja kuomba chaji huku analegeza sauti..hutoboi
 
Back
Top Bottom