Mchezo wa draft na sheria zake

Mchezo wa draft inaacha nafasi za kutembea kwa kila upande nafasi tano... mkicheza French type mtaishia kukosa nafasi kwa mmoja wenu iwapo mtagoma kulana kete.

Kwa mchezo wa British hakuna nafasi ya kutoa kete NNE za nyuma ili nafasi ibaki ya kuingia king bila kulana ili kupata nafasi ya kete za nyuma kusogea mbele....ukibisha Kumbuka enzi za kwenda kupambana na Sokwe kisiwa cha saanane Mwanza kwa mabingwa wa draft.
 
Kama ni force kingi lazima mpinzani ale kete ili aweze kuingia kingi na wewe uiue kingi yake

Sijui inawezekanaje kufika kingi bila mwezio kula hata kete moja na hata ikitokea hakuna hana ya kuvisha kingi mpaka hapo game litakuwa limeisha

Hii ni kwa wale wajubaaa tyuu kwa matutusa hamuwezi kuelewa
 
Unatumia kete za namna gan?, kinachotofautisha king na kete zngne ni kuipa utofauti iyo kete(king) sis tunatumia vzibo vya chupa so king tunaitambua kwa kuifunua kete
au kwa kuvibebesha
 
Duu nimekaa Na draft hapa nimeangalia sana lkn haiwezekan mpinzani asile hata 1 kabla ya we kufika kingi maana hutapata njia
Kuna aina za uchezaji mkibanana sana mmoja akaishiwa kete ya kucheza huwa inapelekea kugawa kete na kama ukimpa mpinzan kete zinazomfanya apate king lazma ataingia king bila wewe kua na kete. Possible kuwa na king na mpinzan asiwe na kete ya kuvisha
 
uhalisia wa aje unautaka mcheza draft mahiri pia mimi mwenyewe shakutana nayo hipo inatokea zaid kwa kupitia force king
Acha kuongopa sasa kama unampa mtu force king kwanini asiwe na kete? Maana ya force king ni kuwa unamlazimisha mpinzani wako ale kete ulizo mtega, kisha wewe unakula kete kadhaa mpaka king. Drafta unajua ama unasikia watu wakisimulia tu? Mi binafsi ni mchezaji mahili, uliza tukujibu sio unadanganya watu hapa, kwanza katika draft haiwezekani ule kete mpaka king bila mpizani kula kete, kwa sababu unaoita katika vyumba ambavyo lazima nae atakula.
 
Kuna aina za uchezaji mkibanana sana mmoja akaishiwa kete ya kucheza huwa inapelekea kugawa kete na kama ukimpa mpinzan kete zinazomfanya apate king lazma ataingia king bila wewe kua na kete. Possible kuwa na king na mpinzan asiwe na kete ya kuvisha
Ikitokea mmebanana sio kuwa kuna mmoja anaweza kuingia king, ila ni kywa mwenye zamu ya mwisho kucheza ndio atashindwa pakusukuma, kwa hiyo kitakachotokea ni kuwa anayekosa pakucheza atakuwa kafungwa kitu kinaitwa super(gori12) kwa mchezo mmoja kwa kuwa unamfunga wakati hakuna mmoja wenu alofika king.
 
ngoma iko hivi yeye anakupiga wewe force kukupeleka king, wewe utakula wakahuo yeye hajala kete hata moja, sasa ile king iliyo ingia anahitaji kuiua ili na yeye apate king! anakosa kete ya kukuvisha zoezi lake linakua limeshindikana. wewe umesema mtaalam lakin nashangaa unavyosema haiwezekan na wala sidanganyi.
 
Iko hivi Braza,
Umeforce King mwanzoni kabisa akala na kuingia King,
Yeye ndio amekula zako, wewe zake hujala,
Na amekula mpaka ameingia King,
Wewe utamvalisha yeye nini??
(Sio yeye atakuvalisha wewe nini)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…