Mchezo wote nauelewa, Mangi ni msafi

Mange hana impact?
Huko ni kujilisha upepo sasa..!!
 
Hii ni mbinu mbovu kabisa wanayoitumia hawa wanaojifanya kuwa watetezi wa maslahi ya Tanzania wakati wakiwa ni wakala wa hao hao wanaotuvuruga kama taifa.

Tangu lini Lema akawa msemaji wa chama. Yeye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ndiyo iwe sababu ya kukihusisha chama kila maswala anayohusika nayo Lema?
 
Badala yake anamlazimisha Lema ajitokeze hadharani kujisafisha, kitu ambacho sio sawa kwa mtu wa level yake kuhangaika na Mange ambaye alishamzushia mpaka dada wa Lissu kukutana na JK hotelini akapingwa na hakusema chochote.
Misingi yako ni ipi? Last time kwenye issue ya Heche wewe na baadhi ya watu humu ndio mlikuwa wa kwanza kusema Heche ajitokeze ajisafishe, leo hii issue ya Lema unasema Brenda/Chama kimsafishe, Double standards sio?
 
Mkuu Kalamu Nadhani umenielewa tofauti kidogo. Sijasema CHADEMA imefanya maamuzi fulani ya kimakosa kwa maagizo ya Mange au wanaharakati wengine.

Hoja yangu ni kuhusu mwelekeo wa mijadala na ushawishi ndani ya chama. Kwa mfano, tunapoona mijadala ya tuhuma dhidi ya viongozi, madai ya usaliti na misimamo kuhusu maridhiano ikitawala mijadala ya wanachama, wakati mwingine hoja za wanaharakati zinaonekana kuwa na ushawishi mkubwa katika kuamua nani ni msaliti na nani ni mfia chama, je chama kinasemaje? Mfano hai ni hii case ya Mange vs Lema, uhisi kwa ushawishi mkubwa wa Mange na madai anayotoa dhidi ya Kiongozi kama Lema ilibidi uongozi uje front, kwa kukaa kimya huoni kuna damage inapatikana kwenye chama?

Hapo ndipo ninapohoji nafasi ya taasisi za chama na mifumo yake ya ndani katika kusimamia baadhi ya mambo.

Sipingani na haki ya wanachama kukosoa viongozi, wala siungi mkono maridhiano yasiyo na masharti. Ninachosisitiza ni kwamba chama kinapaswa kuwa na msimamo na mwelekeo wake wa kitaasisi, badala ya kuonekana kinayumbishwa na kila upepo wa mijadala ya mitandaoni.
 
Na bado chama kinakaa kimya kuona kiongozi wao anabagazwa sio? Huoni kwa kuendelea kukaa kimya kunafanya hata baadhi kutokuwa na imani na viongozi wao?
 
Hakukuwa na maandamano ya Amani na chama cha upinzani hakitakiwi kuwa chama cha vurugu na uasi

Uasi is not democracy
 
Hawa walimuita Dr Slaa msaliti na Gwaji boy akawa kamanda na baadaye Dr Slaa anakuja tena kuwa kamanda - hawana tofauti na mashabiki wa Simba na Yanga.

ndani ya viunga vya hodeidah port - Yemeni.
Wanaharakati ni vigeugeu mno, na itoshe kusema wengi wanaendeshwa na hisia.
 
Ngoja nikujibu hili lililowazi kabisa na jepesi sana kulielewa.

Ni nani anayeanzisha mijadala hii?
Najuwa utasema ni Mange. Mange kaitengeneza tu bila ya uhusika wa Lema?
Kama Lema ni kiongozi ndani ya chama; haelewi taratibu za chama kuhusu hayo yote anayotafuta kuyafumbua yeye?
Hiki chama kinaruhusu tu, kiongozi yeyote yule kutafuta njia zake za kutatua maswala mazito ya taifa hili kwa niaba ya chama; tena kwa kuhusisha hao hao wanaoleta mitafaruku yenyewe?

Hapa utamlaumu Mange, na siyo Lema. 'unless' kama Mange kavumbua tu uvumi na kumhusisha Lema bila ya sababu yoyote. Lakini si Lema mwenyewe kishakiri kuhusu juhudi zake na hao watu wanaotaka hata CHADEMA isiwepo kabisa?

Ni lini umesikia CHADEMA wakitamka rasmi kuhusu hizi habari za Lema anazoibua kila mara na kusambazwa na Mange, kana kwamba wapo mahala pamoja wakishirikiana kufanya kazi hii chafu?
Kwa nini CHADEMA ndio walaumiwe. Hawa wanachama wa CHADEMA waliomo humu mitandaoni ndio tuwachukulie kuwa wanakisemea chama?
Mimi na wewe tunamsemea nani humu sasa hivi, kwa sababu mimi siyo mwanachama wa CHADEMA, wala hiyo CCM marehemu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…