Mchezo wote nauelewa, Mangi ni msafi

Mchezo wote nauelewa, Mangi ni msafi

Mimi yapo maeneo nimemuelewa Mangi lakini amejaa ego na matusi kitu ambacho zamani hakuwa nacho zaidi ya usela. Chama kinaweza kuamua kumtumia mtu miongoni mwao kufanya kazi ya " usaliti" ili kujua yanayoendelea. Lakini Kaongea mambo ya hovyo na kumshushia hadhi kabisa
 
Kuna mambo yanachanyanya kwenye hoja yako

Wanaharakati wengi wako upande wa chadema because wanataka mabadiliko

But sio kila wanachosema au wanachotahadhalisha kiwe directly kama kimesemwa na chadema

Lazima kuweka tofauti ya taarifa za chadema kama chama na taarifa, za wanaharakati

Chadema haijawahi kusema lema ni dalali

But wanaharakati ndio wanasema lema ni dalali
Unadhani hawaelewi au wamepata sababu ya kuisimanga CDM leo.
 
Baada ya kuuawa Magufuli Lema alikiri kuwasiliana na Kikwete ili amfanyie mpango arudi Tanzania kuendelea na siasa, Lissu pia njia hiyo hiyo ingawa kawekwa magereza ili kumkomesha kwa kukiuka makubaliano. Wanasiasa wote wa vyama vyote shikizi na vya mfukoni wote lao moja tu.... Kutumia ujanja ujanja ili wapate ulaji. Lema kwa leo nakubaliana naye kwa kukiri kuwa wananchi ndio wanaoweza kubadilisha hali ya kisiasa nchini kamwe sio wanasiasa au vyama.
 
Mange hana impact?
Huko ni kujilisha upepo sasa..!!
Pamoja na kutokuwa shabiki wake huyo Mange kwa kutoamini anachokipigania; lakini huwezi kusema hana 'impact', wakati hao waovu wenyewe wanahangaika sana kuhusu hayo anayoyaibua.
Hamza Johari, baada tu ya kuapishwa alitangaza kuwa kapewa maagizo kumtafuta Mange. Mtu asiyekuwa na 'impact' hawezi kupewa umuhimu wa aina hiyo.
 
Misingi yako ni ipi? Last time kwenye issue ya Heche wewe na baadhi ya watu humu ndio mlikuwa wa kwanza kusema Heche ajitokeze ajisafishe, leo hii issue ya Lema unasema Brenda/Chama kimsafishe, Double standards sio?
Heche zimekuwa presented risiti zinazomhusu personally na kadi za magari yake binafsi unataka Brenda amjibie?

Mange aliwahi present ushahidi upi na wapi kumhusu Lema zaidi ya umbea wake?

Think.
 
Kama uongozi wa juu wa CHADEMA utakubali kuendeshwa na kupelekeshwa na wanaharakati, chama kitapoteza uelekeo zaidi ya vile kilivyopoteza wakati wa Mbowe.

Kwa jinsi nilivyomsikia Lema, ni kama vile uongozi wa juu wa CHADEMA haukubaliani na baadhi ya uzushi wa akina Mange, ila unaogopa kuupinga kwakuwa matokeo yake yanaweza kuwa ni kuwapoteza hao wanaharakati.

Nadhani, uongozi wa CHADEMA wanaogopa kuwapoteza akina Mange zaidi.
 
Mange hana impact?
Huko ni kujilisha upepo sasa..!!
Muwe mnasoma na kuelewa, narudia tena Mange hana impact yoyote field kama ipo niambie wapi na lini alisababisha nini kikatokea?

Juzi kaitisha maandamano kuwakumbuka waliofariki Okt.29, uliyaonea wapi hayo maandamano yake?

Narudia tena, Mange hana impact yoyote field.
 
Heche zimekuwa presented risiti zinazomhusu personally na kadi za magari yake binafsi unataka Brenda amjibie?

Kwani madai yenu kwa Heche yalianzia kwenye risiti?
Mange aliwahi present ushahidi upi na wapi kumhusu Lema zaidi ya umbea wake?

Think.
Fundamentally ni kitu kile kile wote ni viongozi wa CDM wanaotuhumiwa kwa umbea.
 
Muwe mnasoma na kuelewa, narudia tena Mange hana impact yoyote field kama ipo niambie wapi na lini alisababisha nini kikatokea?

Juzi kaitisha maandamano kuwakumbuka waliofariki Okt.29, uliyaonea wapi hayo maandamano yake?

Narudia tena, Mange hana impact yoyote field.
Rachel dangwa
 
Lema hata angekuwa mwongo basi uongo wake ukimsikiliza bila bias una make sense.
Mambo niyochukua katika press yake
1. Wanaharakati wanategemewa na kuhitajiwa sana katika kuitafuta na kuipambania Tanzania iliyo bora, lakin wawe wanafanya "fact check' kuepuka madhara ya double agents!
2. Wanaharakati watambue kufanya siasa ukiwa ndani jua risk ni kubwa na unaweza kupotea hujafika popote. Umakini(ujanja) unahitajika.
3. Huwezi kupata matokeo ya kisiasa kwa nguvu kati ya aliyeshika mtutu na aliyeshika NENO! Lazma uziangalie tambo zako au uingie msituni!
4.Uhasama wa wanasiasa unafanana na uhasama wa wanaoshitakiana mahakaman na mawakili wao wakinywa chai pamoja(nadhan wananchi ndo wateja)
5. Wananchi ndo tatizo kubwa kwa maendeleo yetu wenyewe kuliko wanasiasa kwa kutowapa ushirikiano, kujitoa na hamasa wale wanaotutetea.
Mwisho kabsa:
" IF YOU CAN'T DEFEAT THEM, JOIN THEM"
"EBYAKAFILE BISHAILWA KAYO!"
Aaa wanshekya munno
 
Lema kwa leo nakubaliana naye kwa kukiri kuwa wananchi ndio wanaoweza kubadilisha hali ya kisiasa nchini kamwe sio wanasiasa au vyama.
Hapo ndo amekamilisha ile ideology ya "PEOPLE'S POWER" lakini wananchi ili walete mageuzi hayo lazima wawe influenced na wanasiasa au social welfare na economic factors i.e kuporomoka kwa uchumi na ugumu wa maisha.
 
Sasa unategemea CDM wawe makini,Nani mwenye huo umakini .
Wakati wote Wana tamaa haina mfano
Wana tamaa Gani CHADEMA? Watu waliogoma kushiriki uchaguzi na kukosa ruzuku unawaita Wana tamaa. Wenye tamaa ya fisi wanajulikana ni CCM.
 
Ntaeleweka vibaya Ila Nataka kuwaeleza pamoja na kwamba mi na mangi ni maji na Mafuta

Ila TISS wamefanikiwa kuwagawa CHADEMA kwa kuwatumia baadhi ya wanaharakati kuwafarakanisha bila kujua

Kwa sasa harakati zimekuwa ni nani karipot wa kwanza , nani anatumia maneno makali nani anaonesha misimamo hata Kama ni ya kipuuzi

Suala la Mangi wamemsingizia hahusiki kabisa na kumpeleka Mkuu wa xxxx kwa Mgwai, alompelekea ni mtu wa nyumba ya xxxx ambaye mwaka ***** alifanikisha jambo!

Chadema muwe makini sana, si kila taarifa mnayopokea mrushe mtandaoni

Alafu Taasisi ijifunze ku address issues za chama kupitia formalities Siyo kila mwana harakati ni msemaji wa Chama

Soma pia

CHADEMA hawana emotional inteligence.
Wanachama wote wanatabia za nyegere.
 
Kwa madai yenu kwa Heche yalianzia kwenye risiti?

Fundamentally ni kitu kile kile wote ni viongozi wa CDM wanaotuhumiwa kwa umbea.
Madai yangu kwa Heche yapo kwa ushahidi uliotolewa dhidi yake mahakamani kumhusu, usinihusishe na wengine, ondoa wingi ukinijibu.

Zaidi hakuna fundamentals hapo.

Mmoja upo ushahidi wa kashfa kumhusu alioshindwa kuutolea majibu ikiwa inamaanisha yote aliyohusishwa nayo ni kweli, kama sio kweli ajitokeze kujibu

Mwingine anasingiziwa mambo ya uongo yasiyo na ushahidi wowote, ni umbea tu unaoaminiwa na wajinga, ndio maana anajiamini ni msafi anajitokeza personally kujisafisha.
 
Back
Top Bottom