Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata huku kwetu kanda ya ziwa walipokuwa wanashughulika na mradi wa kutoa maji ziwa Victoria kwenda shinyanga na sehemu nyingine walimaliza mbwa wa wenyejiHahahahahahaa walipokuwa wanajenga daraja la ruvu, nyoka wote, vyura, samaki, paka na mbwa vyote viliisha.... so huoni kwamba hawa watu sio wenyewe kabisa??
wabaya sana hawa wapuuzi kuna mitaa wamezalisha dada zetu kwenda mbele sooni tutakuwa na taifa la china ndaani ya tanzania waondoleweHawa jamaa utafikiri wana immune fulani mwilini wanakula kila kitu kinachotembea yaani hawali mawe tu.
Na kwa ujangili ni wa tatu duniani wanatisha
Mkuu, Avatar yako inadhihirisha hiyo moja!! pili Misitu inapunguwa kwa kukata miti na biashara haramu ya magogo!! tatu mazingira yamechimwa mashimo makubwa ya migodi, nne mmongonyoko wa ardhi...tano tabianchi maji ya baharini huongrezeka ndani ya ardhi kavu nchini...sita mvua na mafuriko... na hatimaya WaChina huona nyuma ya pazia,,, mimi na wewe hatuoni wala kujua kuna nini!!!kwanini iwe jangwa kwa habari hii? amekamatwa na meno ya ngiri na siyo magogo au miti. labda ungehofu kupungua wanyama.
Mkuu kawaulize polisi waliomkamata, watakuwa na majibuJAMANI ...HATA MENO YA NGIRI TUNALALAMIKA HIVYO? HIVI HAPA TZA YANA FAIDA GANI HAYO MENO, AU SINA UFAHAMU HUO?
TANAPA wamekuja na proposal ya kutaka iendeshwe kijeshi.Nakumbuka Rais Magufuli kwenye kampeni alisema, "Nitagawa kombania, platuni na section ya Tembo, ili kila Tembo atakaetolewa ndovu, viongozi wa section husika wote, mtajibu shutuma!!! Kwa wanajeshi wanaelewa nasema nini" mwisho wa kumbukumbu..
Wachina wanaojidai kuwa ndio wafadhili wetu wakubwa wa miradi mbali mbali hapa nchini baadhi yao wanatumia mwanya huo kutuhujumu hasa pale wanapoamua kuwa soko huru la kununua nyara za taifa letu hasa viungo vya wanyama wetu.
Jana uwanja wa ndege jijini DSM amekamatwa mchina akiwa na meno ya ngiri akijaribu kuyatorosha kwenda nayo kwao.
===============
Jeshi la Polisi la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) linamshikilia raia wa China kwa tuhuma za kukutwa na meno mawili ya ngiri anayodaiwa kuyatengeneza kama vidani kuvihadaa vyombo vya usalama.
Kamanda wa Polisi JNIA, Martin Otieno alisema jana kuwa raia huyo ni mkazi wa Guangdong alikamatwa juzi saa 7.30 mchana wakati akijiandaa na safari ya kuelekea Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Alisema polisi wa JNIA kwa kushirikiana na maofisa wa wanyamapori walitilia shaka begi lake wakati linafanyiwa ukaguzi.
Otieno alisema mtuhumiwa huyo alipokuwa anakaguliwa kwenye mashine za ukaguzi ndipo walibaini kuwa ameficha vidani vya meno hayo ndani ya begi lake dogo.
“Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika eneo la ukaguzi wa mwisho wa abiria tulipomhoji alidai kuwa vidani vya meno hayo amenunua Afrika Kusini,” alisema Otieno.
Otieno alisema mtuhumiwa huyo alidai kuwa alinunua vidani vya meno hayo kwa ajili ya urembo lakini walipochunguza hakuwa na kibali kinachoonyesha nchi aliyonunua.
Kamanda Otieno aliwaomba wananchi kuwa na uzalendo wa nchi yao wanapoona mtu anasafirisha rasilimali za nchi watoe taarifa Jeshi la Polisi.
Alisema polisi wataendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo ya mipakani na viwanja vya ndege ili kudhibiti aina hiyo ya utoroshaji wa nyara.
Otieno alisema uchunguzi unaendelea ili kumfikisha katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazomkabili.
Chanzo: Mwananchi
Aisee!Wakimaliza meno ya ngiri waje wachukue nyayo zetu huenda ni dawa ya kupasulia miamba
Ndiyo mkuuKumbe meno ya Ngiri nayo dili