Mchina amenakili Range Rover Evoque na kuiita yake Land Wind

Mchina amenakili Range Rover Evoque na kuiita yake Land Wind

bora mana wabongo tunajua nakili uchawi tu
 
1472427094999.jpg
Aisee hii Gari balaaa
 
Deng Xiaoping ndo shikamoo zaidi. Huyu bwana ndiye aliyeleta fikra mpya kwa wachina. Pamoja na nia njema ya Mao Zedong, fikra zake zilikua mgando. Deng kwa kuwa aliwahi kuishi Europe, akachukua falsafa za Ulaya akaziharmonize kuendana na sera zao za Kisoshalist. Hivyo akaruhusu uwekezaji, huyu ndiye aliyesababisha Wachina kutoka na kujifunza Technolojia nje ya China. Kwa kifupi huyu ndiye MZEE RUKSA wa TAIFA LA CHINA!
Huyu jamaa ana documentaries zinazoonyesha maisha yake. Kama zipo tuwekeee tumcheki uwezo wake
 
Mchina katutoa kwenye ushamba, otherwise tungeendelea kuyaona kwenye Runinga...Asante sana Mchina wewe ni Jembe..nina uhakika after 1 Century tutaanza kumiliki JET kwa kila mtanzania, mpaka yule anaeishi porini na akina swala atamiliki pia...
 
Mchina anamaana basi, hapo unaweza ukaitandika speed hiyo land wind halafu ghafla tairi yako ya nyuma ukaiona imekutangulia mbele.
sio kwelii ingekua inatokea hivyo kwenye magari kama yutong higer zungtong na mabas mengine ya kichina ambayo sasa ni usafiri mkubwa kwa safari za mbali na ni comftable
 
Bila mchina,wengi tungeonaga vitu vingi vizuri katika video tu.
 
Minimelipenda hilo gari lakini sijapenda walivyotohoa hilo jina kutaka lifanane na Range rover au Land rover linaleta inferiority. Kwa mimi ningependa kama wangetoka na brand yao tu kama walivyofanya kwa yutong hagie n.k mbona yamekubarika sana tu. Ila lilivyo hakuna shida, na limependeza hasa, kwani magari kufanana ni kawaida.

Mi huwa sipendi kununua kitu kilichotoholewa jina eti nionekane na mimi namiliki kitu cha gharama wakati si Kweli namdanganya nani?

Wachina waache kutohoa majina, wajiamini waanze kutengeneza na wao brands zao zisimame, tupo tunaoangalia unafuu wa bei na matumizi tutanunua tu. Mimi binafsi siwezi kununua Scania moja wakati naweza kupata Yutong mbili kwa pesa hiyo hiyo na chenji ya mtaji inabaki, kwanza napunguza risk, pia naongeza turnover. Kwahiyo wajiamini tu.
 
Back
Top Bottom