Mchora katuni Opptertus John Fwema ashikiliwa na Polisi kwa Makosa ya Mtandao

Mchora katuni Opptertus John Fwema ashikiliwa na Polisi kwa Makosa ya Mtandao

Au ujifanye shujaa na kusema wewe bingwa umeiondoa Covid kwa maombi ya siku 3..mwisho wa siku tunakuzika wewe na wasaidizi wako
"...one of his security guy...the darkest one...died due to covid..." Tundu Antipas Lissu (former opposition party president candidate)
 
Sasa kwa hiyo Cartoon unaweza kuthibitisha makosa yake?
Acha kupaza sauti kwenye mambo usiyoyajua utachekwa kukusaidia google torn inayoitwa " innuendo " isome kwa makini elements zake ukishaelewa uwaelimishe na vilaza wenzako
 
Mimi ni Muumini wa uhuru wa kutoa maoni ila na huwa naamini ya kuwa kila afanyae jambo basi pia yupo tayari kwa matokeo hasi au chanya.
 
Kipanya katuni zake huwa hazipo straight kama huyu, Masudi anaficha maana sana ukiigundua unakua genius, sasa huyu ndugu anafungua code zote msomaji hapati tabu kufafanua

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna lolote umeona katuni ya Kipanya ya hivi majuzi? je inahitaji code? ni kama vile kuna kuchagua nani wa kumkamata.
 
Acha kupaza sauti kwenye mambo usiyoyajua utachekwa kukusaidia google torn inayoitwa " innuendo " isome kwa makini elements zake ukishaelewa uwaelimishe na vilaza wenzako
Hebu tuelezee hiyo katuni ina maana gani
 
You nailed it, kwa mtazamo wangu hapo waliomkamata mchoraji ndiyo walitakiwa kukamatwa, hivi tangu lini kumchora mwanasesere amevaa ushungi mwekundu ni kosa? Au kuandika mlemavu wa miguu anayesota ni kosa? Au wamshitaki kwa kuchora bendera ya taifa kwenye sufuria
Wanaounga mkono huu upuuzi ni mateja wa madaraka.

CCM ni chama changu, lakini moyo unaniuma namna tunavyofanya siasa uchwara
 
Cartoonist Oppter John Fwema anashikiliwa na polisi kituo cha Oysterbay. Nimeongea na mdogo wake na amenambia kuwa Oppter alikamatwa nyumbani kwake Bunju siku ya Ijumaa tarehe 3 September 2021kwa makosa ya mtandao. Taarifa zaidi zinaendelea kupatikana Polisi na kwa familia na tutajuzana zaidi.

Oppter anafahamika kwa katuni zake zenye ujumbe wa kukosoa serikali.


View attachment 1960305 mchoro wa Katuni uliomuingiza matatani

View attachment 1960306 ukurasa wake wa Instagram

View attachment 1962105

=≈========UPDATE==========

Polisi wamezuia dhamana yake. Kwa mujibu wa ndugu na jamaa wanaofuatilia wamenijuza kuwa
Wanasheria nguli wamejitokeza kufuatilia sakata la msanii huyu.

Inawezekana uwepo wa wanasheria ukapelekea haki kutendeka bila kukiuka haki za mtuhumiwa.

Nitaendelea kuwajuza zaidi kadiri taarifa sahihi zinavyopatikana

===≈====== UPDATE ==========
02/10/2021
Mpaka naandika ujumbe huu, ndugu wanasema kesi imeshikiliwa na RCO, tangu amekamatwa hakuchukuliwa maelezo ambapo amehojiwa Alhamisi wiki hii.

Wanasheria wameshajitokeza kufuatilia haki za mchoraji huyu wa vibonzo.

===≈====== UPDATE ==========
04/10/2021
Wakili Msomi Jebra Kambole amejitolea kushughulikia suala la Mchoraji Optter Fwema.

Ameshawasiliana na ndugu wa mshikiliwa kwa ajili ya taratibu za kisheria.

Mashirika na majukwaa ya kimataifa wameanza kufuatilia na kuanzia leo sauti zitapazwa.

-------------SAHIHISHO------------

Watu wengi wanamfananisha mchoraji Optter na mwanavibonzo mwingine aitwaye Fredy ambaye alitumia sana kalamu yake kuwachora upinzani wakati wa uchaguzi
Tuone watatumia kisingizio gani kumshikilia.
 
Mheshimiwa Oppter kazi yako ni nzuri sana.Mungu akubariki sana.

View attachment 1960333
Tuliwaambia mlio sema magufuli ni dictator [emoji1787][emoji1787][emoji1787]sasa mtajua kuwa kuna dictator mwenye akili na dictator mpumbavu hao ni vitu viwili tofauti kabisa ,sasa sijui wapinzani mtakwenda kushitaki wapi maana sifa ya madictator wapumbavu ni kuuza nchi kwa manufaa ya watu weupe hivyo wanapendwa na mabeberu tofauti na JPM alikuwa dictator wa kupigania nchi dhidi ya mabeberu
 
Tuliwaambia mlio sema magufuli ni dictator [emoji1787][emoji1787][emoji1787]sasa mtajua kuwa kuna dictator mwenye akili na dictator mpumbavu hao ni vitu viwili tofauti kabisa ,sasa sijui wapinzani mtakwenda kushitaki wapi maana sifa ya madictator wapumbavu ni kuuza nchi kwa manufaa ya watu weupe hivyo wanapendwa na mabeberu tofauti na JPM alikuwa dictator wa kupigania nchi dhidi ya mabeberu
CCM haijawahi kuwa na la maana.Adui yetu ni CCM wala siyo mtu fulani ndani ya CCM.
 
Alitumia njia nyepesi sana kufikisha ujumbe inabidi apate shule kwa Kipanya. Jamaa anachora katuni very intriguing and intricate with lots of confusions.
 
Back
Top Bottom