Let me do this for my bebe..[emoji3526]
Ni kweli, Katiba ya JMT imebainisha haki ya kutoa maoni. Lakini hakuna haki isiyo na mipaka. In other words, yaani siyo tu kwasababu Katiba imekuruhusu kutoa maoni yako ndiyo ujiachieee mpaka uwajeruhi wengine, lazima uwe na kiasi kwani haki yako inapoishia ndiyo haki ya mwenzako inapoanzia.
Sasa ikumbukwe kwamba Urais ni Taasisi. Na kila Mamlaka imetoka kwa Mungu (Warumi 13). Katuni za huyo jamaa, kwa mfano hiyo ya mama anapiga ngoma halafu yupo na JK...hiyo ni lugha ya picha na ina tafsiri kwamba mama ni DHAIFU, eti JK ndiyo anaongoza nchi kwahiyo mama anaendeshwa tu! In Law this is termed as defamation, which is defined as ruining the reputation of another, sasa siyo 'another' kama mimi an ordinary civilian, huyo ni Rais wa nchi (Amiri Jeshi Mkuu), kwahiyo hapo ameidhalilisha Taasisi ya Urais.
Sasa hii defamation inaweza kuwa slander (kwa maneno) au libel (kwa maandishi including CARTOONS).
Bebe nadhani umenielewa kidogo. Ajifunze kwa mwenzake KP (Masoud Kipanya), yule kumkamata ni shughuli manake Katuni zake kuzielewa ni mtihani!).