Mchumba kakataliwa kisa shepu

niikuulize swali km wewe unataka kuoa dada zako wanakushauli uachane na huyo mchumba wako, swali langu kwako ni hili cku dada yako akija na mchumba wake unadiliki kumwambia dada yako kuwa ujampenda bwanake? atimaye atafute mwingine acha ujinga wewe ni mtoto wa kiume na anayeoa ni wewe na c dada zako, umeongelea swala la baraka kutoka kwa ndugu zako wa tumbo moja kwani wao ni nani? ni mungu eti anatoa baraka? ndugu hukusaidia mawazo tu na c mahamzi ya kuoa kwako.
 
....unataka mchumba wako au mchumba wa dada zako?





#MosKwito !
 
koroga hamira kwenye maji halafu mnyweshe
 
Sina hakika kama unamapenzi na huyo Dada, maana anaeoa ni wewe na sio Dada zako so its your choice kusuka ama kunyoa
 


Na wao wakileta waume watarajiwa uwape mapendekezo yako pia(Kama hawajaolewa)
 
Kwani waoaji ni hao dada zako au wewe mwenyewe???? Ina maana wewe huna maamuzi yako kama mwanamme? Pili uzuri wa mwanamke sio shape, ni tabia yake tu. Je kama wakimtaka mwenye shepu na mara akaugua na kumpelekea shepu yake kuharibika na kuwa BETINA Je, wataendelea kumpenda au ndo watakutafutia mwingine?? Na je huyo mke wako ni wao dada zako wanakwenda kuishi nae au ni wewe? Hao dada zako wameolewa amaaa!!! Mmmmmh siku zote mtu hawezi kukuchagulia mke au mume, ni moyo wako ndio wenye maamuzi.
 
Siku hizi wanaume tunadhalilishana sana...Sasa na wewe mwanaume mzima unakuja kulia kulia kwa kushindwa kufanya maamuzi madogo kiasi hiki?
 
Tena tukalale barabarani pale karume!! Tukemee ubaguzi wa ki umbo.
Ila twin wanaume wa kuamuliwa na dada zao tunawahitaji kweli?

sio issue ya kuamuliwa na dada zangu wewe...kuna masuala ya kuomba ushauri kwa watu wako wa karibu na mengine ya kufanya maamuzi magumu bila kuathiri uhusiano uliopo!!
 
sio issue ya kuamuliwa na dada zangu wewe...kuna masuala ya kuomba ushauri kwa watu wako wa karibu na mengine ya kufanya maamuzi magumu bila kuathiri uhusiano uliopo!!

Unaomba ushauri kuhusu shape ya mkeo mtarajiwa! Uoe mke kibonge kisa madada vibonge au mwembamba kisa dada zako wembamba?
Kuna masuala ya kuomba ushauri Yes ila si katika hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…