Njoo tubadilishane mkuu, kama wa kwako kichwani ametulia! mimi ninae ana shape ya ajabu but kichwani mh....kichwa maji na amejaa wivu usio na maana. Njoo mkuu...Jamani wana Jamiiforums wenzangu nimebaki njia panda. Nilienda kumtambulisha mchumba wangu kwa wifi zake (dada zangu) juzi jumatatu huko kwetu sinza mida ya jioni baada ya kutoka kazini kwa kuwa tunafanya kazi ofisi za karibu pale posta.
Ila walichonijibu ni kuwa nitafute mwingine kwa kuwa huyu hana shape hawajampenda. Huyu mchumba angu yeye ni slander (mwembamba). Jamani naombeni ushauri wenu nifanyeje sasa nimebaki njia panda.
kAmuoe wema sepetu...true love is beyond relatives,religion,parent...msimuoe huyo binti mana humpendi., ungempenda usingeona madhaifu.yake
We unampenda mwenye shepu ipi
anaye oa ni mimi ila baraka za ndugu wa tumbo moja ni muhimu sana!!
heeee! Mamodo tuandamane haiwezekani tubaguliwe tunajiona
Usipoangalia utaolewa wewe!
acha ushamba wewe, kila mtu na chaguo lake, wewe kama moyo wako hujampenda huyo kaka sawa, lakini eti umuache kisa mwembamba? kwani yeye alipenda awe mwembamba? kwa nini hao dada zako hawakukwambia toka zamani kuwa ikiwa unatafuta mchumba basi tafuta mnene? hadi umempotezea kaka wa watu muda wake? shauri yako tafuta laana tu!!
How old are you?
sio suala la kupotezeana muda mkuu...nipe mbinu za kuwashawishi dada zangu ili tufikie muafaka bila kununiana aisee!!
Kama unajua hilo kwanini unakuja JF kusumbua ma GT!
Ila Sishangai as still nado uko kinda, good luck
Sishangai @ 29 years mtoto wa kiume huna maamuzi just dada zako wanakuhangaisha kwa mke unaempenda?? kweli??? your not serious....kama unaona ni usumbufu si unakaa kimya tu!!
Wao hawajaolewa bado ila wanafanya kazi mmoja ni lecturer chuo kimoja kikubwa mwingine ni senior tax officer TRA!!
Sishangai @ 29 years mtoto wa kiume huna maamuzi just dada zako wanakuhangaisha kwa mke unaempenda?? kweli??? your not serious....
mambo mengine sio ya kufanya uamuzi mgumu utakaojenga nyufa katika familia...ninatafuta namna ya kubadili their prejudiced mindset na kuona kuwa watu wote ni sawa...i think they need some sort of psychiatric counselling ili kuwabadili namna wavavyotazama mambo.
Simshauri tenaImagine twin unamshauri kitu mumeo anakwambia subiri kidogo,then ananyanyua simu kumpigia dada yake kwanza apewe go ahead!
Wallahi namnasa kofi!!
Mwanaume asiye na msimamo ni janga kubwa saana..!! Hafai hata kidogo..!!