Mchumba kakataliwa kisa shepu

Mchumba kakataliwa kisa shepu

Jamani wana Jamiiforums wenzangu nimebaki njia panda. Nilienda kumtambulisha mchumba wangu kwa wifi zake (dada zangu) juzi jumatatu huko kwetu sinza mida ya jioni baada ya kutoka kazini kwa kuwa tunafanya kazi ofisi za karibu pale posta.

Ila walichonijibu ni kuwa nitafute mwingine kwa kuwa huyu hana shape hawajampenda. Huyu mchumba angu yeye ni slander (mwembamba). Jamani naombeni ushauri wenu nifanyeje sasa nimebaki njia panda.
Njoo tubadilishane mkuu, kama wa kwako kichwani ametulia! mimi ninae ana shape ya ajabu but kichwani mh....kichwa maji na amejaa wivu usio na maana. Njoo mkuu...
 
kAmuoe wema sepetu...true love is beyond relatives,religion,parent...msimuoe huyo binti mana humpendi., ungempenda usingeona madhaifu.yake

kila binadamu ana mapungufu yake na hakuna aliyemkamilifu!!
 
Hv nyie mnasoga post kwanza au,post inamuhusu mdada na co mkaka lol
acha ushamba wewe, kila mtu na chaguo lake, wewe kama moyo wako hujampenda huyo kaka sawa, lakini eti umuache kisa mwembamba? kwani yeye alipenda awe mwembamba? kwa nini hao dada zako hawakukwambia toka zamani kuwa ikiwa unatafuta mchumba basi tafuta mnene? hadi umempotezea kaka wa watu muda wake? shauri yako tafuta laana tu!!
 
Kumbe dada zako wanaoa na si wewe?? Ngoja na mkeo atakuoa wewe!!! Ningekuwa wewe nisingepoteza muda wa kuuliza hapa?? Ninayeoa ni mimi na hakuna wa kuniingilia isipokuwa Mungu mwenyewe!!!! Mnapenda kuendekeza mambo yasiyo na kistaarabu!!! Usipokuwa makini hutakuwa na ndoa ya chaguo lako na itakugharimu!!
 
Sishangai @ 29 years mtoto wa kiume huna maamuzi just dada zako wanakuhangaisha kwa mke unaempenda?? kweli??? your not serious....

mambo mengine sio ya kufanya uamuzi mgumu utakaojenga nyufa katika familia...ninatafuta namna ya kubadili their prejudiced mindset na kuona kuwa watu wote ni sawa...i think they need some sort of psychiatric counselling ili kuwabadili namna wavavyotazama mambo.
 
mambo mengine sio ya kufanya uamuzi mgumu utakaojenga nyufa katika familia...ninatafuta namna ya kubadili their prejudiced mindset na kuona kuwa watu wote ni sawa...i think they need some sort of psychiatric counselling ili kuwabadili namna wavavyotazama mambo.

Is it a psychiatric of psychological problem?. IF ITS THE FORMER AND NOT THE LATER THEN DON'T ASK THEIR OPINION.
 
Mwanaume asiye na msimamo ni janga kubwa saana..!! Hafai hata kidogo..!!
 
Na hao dada zako wana shepu gani haswaaa mpaka waikosoe ya mkeo mtarajiwa? Hao ndo wale mawifi wa kuwapa kubwa... kama vipi piteni ndani mkamridhishe na kaka enu maana mnampenda sana hawezi kohoa bila nyie kusema!
 
Back
Top Bottom