ila hao dada zangu wao wote ni vibonge kweli kweli aisee!!!
Yaani mpaka nakushangaa ujue, kwani hao dada zako ndo wanamuoa huyo binti wa watu?
Ww huna msimamo kwa maamuzi ya maisha yako?
Ulienda kumtambulishaa ili dada zako wakusaidie kumdescribe dada wa watu au kwasabu umeridhika naye na ukaona anafaa kuwa mkeo?
Aibu iwe kwako, kuwa na msimamo ww
Achana na mtoto wa watu ishi na dada zako ili msinuniane....
Hapo bado mitihani ya ndoa.
bi dada mfano achelewe kushika mimba?
Uafrika kazi.
heeee! Mamodo tuandamane haiwezekani tubaguliwe tunajiona
Jamani wana Jamiiforums wenzangu nimebaki njia panda. Nilienda kumtambulisha mchumba wangu kwa wifi zake (dada zangu) juzi jumatatu huko kwetu sinza mida ya jioni baada ya kutoka kazini kwa kuwa tunafanya kazi ofisi za karibu pale posta.
Ila walichonijibu ni kuwa nitafute mwingine kwa kuwa huyu hana shape hawajampenda. Huyu mchumba angu yeye ni slander (mwembamba). Jamani naombeni ushauri wenu nifanyeje sasa nimebaki njia panda.
Kuna mamodo wengine wamezidi aisee! miguu kama mikono! akisimama kama kapiga sarakasi(kasimamia mikono).heeee! Mamodo tuandamane haiwezekani tubaguliwe tunajiona
uko serious ama utani mkuu
mambo mengine sio ya kufanya uamuzi mgumu utakaojenga nyufa katika familia...ninatafuta namna ya kubadili their prejudiced mindset na kuona kuwa watu wote ni sawa...i think they need some sort of psychiatric counselling ili kuwabadili namna wavavyotazama mambo.
Sasa mkuu upo Njia panda gani hapo sinza nije nikupitie kwa gari yangu?
anaye oa ni mimi ila baraka za ndugu wa tumbo moja ni muhimu sana!!
Kuna mamodo wengine wamezidi aisee! miguu kama mikono! akisimama kama kapiga sarakasi(kasimamia mikono).
ila hao dada zangu wao wote ni vibonge kweli kweli aisee!!!
sasa mkuu ukifanikiwa kwenye hilo kwa dada zako na huyo mchumba ndo shepu itabadilika!