Mchumba wangu ananishirikisha katika kila kitu cha maendeleo anachofanya

Mchumba wangu ananishirikisha katika kila kitu cha maendeleo anachofanya

Mshaurini huyu jamani...

MCHUMBA WANGU ANANISHIRIKISHA KATIKA KILA KITU CHA MAENDELEO ANACHOFANYA!

Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba ambaye yeye ana miaka 30, nampenda sana na yeye anaonyesha kunipenda kwakua kashanitambulisha mpaka kwao na kwetu pia nimeshamtambulisha. Tatizo nikua mpenzi wangu huwa ni muwazi sana, ananishirikisha katika kila kitu chake cha maendeleo anachokifanya na mara nyingi anakua anataka mawazo yangu, akitaka kununua kiwanja, kujenga, akitaka kitu chochote hata kama ni mapazia anataka tufanye pamoja.

Mimi nafanya kazi nayeye pia anafanya kazi, haniombi pesa na wala hajawahi lakini tatizo nikua kwakua ananishirikisha katika mambo yake basi nashindwa kumuomba pesa kubwa kubwa kwaajili ya kufanya mambo yangu kwani kila hela yake najua imeenda wapi? Kwa mfano labda nataka laki mbili ninataka kununua kitu changu labda kutoka na marafiki, nikimumba pesa ananiambia hana si tumenunulia kitu flani, ukiangalia kweli alinunua hicho kitui na alinishirikisha hivyo naona aibu hata kumkasirikia kwani kinakua cha maendeleo na najua pesa yake yote.

Naumia sana kwani mimi kama msichana nahitaji kudekezwa na kufanyiwa suprize za zawadi kama marafiki zangu ambao wanaweza kufanyiwa birthday na wapenzi wao, kutolewa out, kununuliwa nguo na zawadi. Mimi nikihitraji kitu inabidi nimuambie mapema kabla ya mshahaara ili aniweke kwenye bajeti na sanasana atakupa elfu hamsini hata laki hakupi kwani anakua anafanya vitu vingi vya maendeleo ambavyo ananiomba ushauri na ukiangalia anakua kweli hana kwani hata yeye hafanyi hizo starehe.

Kinachoniuma zaidi nikua hawezi kufanya maamuzi yake mwenyewe kama mwanaume ni lazima aniambie na mara nyingi hupenda kufuata ushauri wangu na si wake. Kunipenda kweli ananipenda lakini nina wasiwasi je tukiona itakuaje kwani mara nyingi anasema tukioana itakua vizuri kama tukishirikiana kwenye mambo ya familia eti mshahara wangu nao tufanyie mambo ya maendeleo wakati yeye kama mwanaume anatakiwa kufanya kila kitu, niko njia panda na waza je huyu ni mtu sahihi kwangu au nifanyeje?
Hapo tunashindwa kumshauri. Mwambie kuwa Hapa duniani kuna njia mbili tunazikimbilia " Njia ya Uhai na maradhi na Njia ya Kufa na kusahaulika" Je yy anataka akimbilie njia gani? Mwambie kua Anawindwa na " Ukoo wa Mashetani na Ukoo wa Malaika" Je anataka kujiunga na familia gani? Nadhani kwa hao atapata majibu sahihi....
 
Huyo binti anashida sehemu mtu anakushirikisha vitu vya maendeleo hupendi[emoji849][emoji849][emoji849]!!!!!!

Kuna viumbe sijui ua vinataka nn ili kuridhika....... AJABUUUU!
Na pia anakazi yake inayomuingizia kipato
ila anataka jamaa aache kufanya vitu vya maendeleo waende wakajirushe
 
Back
Top Bottom