Mchumi wetu Mwigulu Nchemba anaupiga Mwingi, hakika Rais Hakukosea

Mchumi wetu Mwigulu Nchemba anaupiga Mwingi, hakika Rais Hakukosea

Comrade Mushi

Member
Joined
Feb 25, 2023
Posts
5
Reaction score
7
Kisa cha Wakili Farah Maalim Mohammed na kielelezo cha makuu ya Tanzania.

#Zimesambaa video za Naibu Spika wa zamani wa Bunge la Kenya na Mbunge wa sasa wa jimbo la Dabaab Nchini Kenya Mh. wakili msomi na mchumi mwandamizi Faraah Maalim Mohamed akieleza Threat ya kiuchumi Tanzania wanaiweka katika ukanda huu wa maziwa makuu.

Faraah akihojiwa na kituo cha Citizen nchini Kenya mapema jana anaonyesha na kutufundisha mambo yafuatayo kwa ufupi.

1. Ukuaji wa uchumi wa Tanzania upo katika speed ya kushtusha katika kipindi cha miaka michache iliyopita hadi sasa kiasi ambacho si tu ni kama "alarming pace'' ila ni somo kwa mataifa jirani

2. Uwiano wa ufanyaji biashara baina ya nchi ya Tanzania na nchi za nje na zaidi zaidi Kati ya Kenya na Tanzania (trade balance) imekua kwa kiasi ambacho si tu kinashangaza, bali kinatoa nafasi kubwa ya kujifunza on what has really really happened!

Trade balance kati ya Kenya na Tanzania miaka kadhaa nyuma ilikua ni Kenya iki export zaidi kuja TZ kuliko importing kutoka Tanzania kitu ambacho kwa sasa ni completely tofuati kiasi ambacho hata wasomi wao wa uchumi hawaelewi how in the lighting speed Tanzania would've change the odds!

Je, haya yote ni bahati mbaya?

Tangu enzi za wachumi aina ya Adam Smith, Karl Marx an wengine ni kwamba it's an acceptable norm kwamba , Katika uchumi hakuna the so called BAHATI MBAYA ni lazima kuwe na efforts za makusudi ambazo zimefanywa kufanya kila kitu like how it seems to be. Hii ina maana kwamba haya tunayoyaona leo kama mageuzi ni lazima kuna efforts na utaalamu wa kiuchumi ambao unafanya haya yawe hivi. Hapa ndo smart moves behind 4Rs za Mheshimiwa Rais wa sasa Dkt. Samia Suluhu Hassan zinapokuja kupata mantiki. Niskiize;

Kuna 4Rs ambazo awamu ya sita chini ya Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inazitekeleza kisera ndo msingi wa mengi tunayoyaona na kuyaita mageuzi. Reforms kama sehemu ya falsafa za 4Rs inebeba sehemu kubwa ya maono ya Mama katika awamu hii na ndio haswaa imepelekea mageuzi mengi ya sera na sheria zetu katika ufanyaji biashara, uwekezaji na zaidi katika namna tunavyohusiana na wenzetu kwa maana mageuzi katika diplomasia yetu.

Utekelezaji wa mageuzi haya katika mfumo wa kisera na kikodi ,sambamba ba uimara wa timu za usimamizi kuanzia ngazi ya juu, ngazi ya wizara ,idara na hata watendaji wa chini ndo matokeo ya mengi tunayoyaona leo. Wizara ya Fedha kwa mfano kama msimamizi mama wa sera zetu za fedha na uchumi (Fiscal and Monetary policy) kuna namna imefanywa kazi katika level ambayo labda tunaiona kwa picha ndogo than how it's really looking. Niskiize tena hapa.

1. Uchumi ni namba na namba hazidanganyi wal hazijifichi. Ukiwa na utekelezaji chanya wa sera na mipango yako lazima positive impact katika ukuaji wa uchumi wako itaonekana. Leo wakati Dunia nzima ikiwa katika dilemma ya kiuchumi baada ya athari za COVID-19 na vita ya Ukraine, Benki ya Dunia katika Economic Updates yake ya 2023 inaitaja Tanzania kama Nchi yenye makadirio ya ukuaji mkubwa wa uchumi kwa mwaka ujao kuliko nchi zote za kusini mwa jangwa la Sahara. Ni bahati mbaya ? NO

2. Baada ya miaka kibao ya uwiano usio sawa wa kibiashara kati ya Tanzania na Kenya, leo wachumi waandamizi wa Kenya wanakiri kwamba Tanzania sasa ni tishio na ukuaji wake ni wa kutisha

3. Business Insider kama jarida kubwa kabisa la masuala ya uchumi na biashara linaitaja Tanzania kuwa tishio jingine la kiuchumi kwa ukanda wa Africa. Ni bahati mbaya pia? No.

Kama ilivyo desturi yetu, Watanzania huwa na kasumba ya kujichukulia poa. Mara nyingi huwa ni wazito kuziona hatua tunazopiga na tukiziona hatuzipi uzito but kama kuna nyakati kama taifa tunapita kipindi cha kujivunia ni sasa. Ukuaji wa uchumi wetu katika angle ya kitaalamu unatoa a picha that is worth cherishing.

 
Kisa cha Wakili Farah Maalim Mohammed na kielelezo cha makuu ya Tanzania.

#Zimesambaa video za Naibu Spika wa zamani wa Bunge la Kenya na Mbunge wa sasa wa jimbo la Dabaab Nchini Kenya Mh. wakili msomi na mchumi mwandamizi Faraah Maalim Mohamed akieleza Threat ya kiuchumi Tanzania wanaiweka
Uchawa nao ni taaluma. Hatusubiri tuelezwe na mtaalamu wa kutoka Daadab mpakani mwa Kenya na Somalia of what is going on in Tanzania! Sisi tupo Tz na tunajionea kama tupo vizuri au tupo hoi. Hatuhitaji mtaalamu wa Daadab!
 
Viwanda,vinyozi nk, wanashinda bila kufanya KAZI umeme hamna,

Uchumi unakuaje bila umeme wa uhakika?
 
Uchumi unakuwa Huku tunakopa ili serikali iweze kulipa madeni ya Hatifungani? Basi itakuwa uchumi tafakari yake ni ngumi kuelewa kama ilivyo ngumi kuelewa Neno la Mungu ambalo linahitaji jicho la roho
 
Kisa cha Wakili Farah Maalim Mohammed na kielelezo cha makuu ya Tanzania.

#Zimesambaa video za Naibu Spika wa zamani wa Bunge la Kenya na Mbunge wa sasa wa jimbo la Dabaab Nchini Kenya
Laiti watanzania tungekua wamoja kweny kuijenga nchi yetu na kuondokana na uchawa tungefika mbali san!!
 
😅😅😅jamaa alisema labda mjadili uganga lakini uchumi ni profession yake,so hqmumwambii lolote😅
 
Uchumi unakua lakini Kodi haikusanywi,

Inabidi ichukue MKOPO mpya tri 5, kulipa deni la MKOPO wa nyuma!!

Uongo una mwisho, tumekaribia mwisho.
Huyo poropesa mwigu,mimi nilijiuliza mtu anayechora jina lake kwenye mawe anaweza kuwa waziri wa fedha compitent kweli?😅🏃
 
You are politically right ila katika ulimwengu wa damu nyama umepuyanga na Dr Nshumbi
Balance of trade/balance of payments haiwezi toka Hasi kwenda neutral au chanya pasi kuwa na matendo kwenye uwanja wa Vita,ni tofauti na majira ya mwaka ambayo yapo tu hata Kama binadamu hatofanya lolote
 
Projects za kuwapa vijana mashamba zikifikia climax na bwawa la umeme na sgr vikaisha,kila mtu Africa mashariki na kati atataka kuja tz
 
Mnatumia nguvu nyingi kutuamnisha hawa waizi kwamba wachapa kazi,na huyo anayeongea hapo juu kwemye video mmemnunua tu aje kuongea ujinga wake.

Uchumi gani umekuwa kwa kasi hapa Tanzania?
 
Laiti watanzania tungekua wamoja kweny kuijenga nchi yetu na kuondokana na uchawa tungefika mbali san!!
Kweli mkuuu na hawa unaowaona wanafanya uchawa humu mara samia anaupiga mwingi,Mara mwiguru ni jembe mama hajakosea wote hawana kazi.

Mtu hauwezi kuwa na kazi ya kufanya ukapata Muda wa kuwa chawa,Unatembea na mtu matakoni.

Sasa huo uchumi umekuaje na machawa wanashindana wingi na Mashoga?
 
Viwanda,vinyozi nk, wanashinda bila kufanya KAZI umeme hamna,

Uchumi unakuaje bila umeme wa uhakika?

Umeme ulikua tatizo na ndio moja ya vipaumbele vya pesa nyingi zinazopatikana kupelekwa huko Tatizo linaisha
 
Uchumi unakuwa Huku tunakopa ili serikali iweze kulipa madeni ya Hatifungani? Basi itakuwa uchumi tafakari yake ni ngumi kuelewa kama ilivyo ngumi kuelewa Neno la Mungu ambalo linahitaji jicho la roho

Uko sahihi kabisa ili uelewe uchumi unahitaji Taaluma hiyo vizuri hasa ukizungumzia Uchumi wa kidunia
 
Back
Top Bottom