Mchumi wetu Mwigulu Nchemba anaupiga Mwingi, hakika Rais Hakukosea

Si unajua Watanzania kila kitu tunajua ukute Mwalimu wa Kiswahili anaongelea uchumi Daktari anakua mchambuzi wa soccer sisi hatushindwi jambo lazima tujifunze kukubali tusiyoyajua
 
Huyo poropesa mwigu,mimi nilijiuliza mtu anayechora jina lake kwenye mawe anaweza kuwa waziri wa fedha compitent kweli?[emoji28][emoji125]

Ndio bahati tuliyopata tokea uhuru kwa taarifa yako Hakuna kama Mwigulu angekua mwingine kwa namna taifa lilipopitia na Dunia kuweka uchumi stable namna hii si kitu kidogo
 
Mnatumia nguvu nyingi kutuamnisha hawa waizi kwamba wachapa kazi,na huyo anayeongea hapo juu kwemye video mmemnunua tu aje kuongea ujinga wake.

Uchumi gani umekuwa kwa kasi hapa Tanzania?

Inategemea Unafanya kazi gani kwa mda gani kama livivu uchumi usitegemee kuona umekua tuache kulaumu tufanye kazi
 

Hoja yako ndio Kipimo cha unachowaza na kuzunguka kwenye akili yako Kama unaajira lazima uwe na utimamu hata kujadili mambo muhimu yanayofanywa na viongozi juu ya maendeleo ya taifa letu
 
Wapumbavu watabeza, shida Tanzania ina maadui wa ndani yake na nje yake!,
Labda niipongeze awamu hii ya sita (6)kwa jinsi na kwa haraka walivyoweza ku stimulate uchumi DUMAVU wa iliyokuwa awamu ya tano, na kuunyanyua na kuufikisha hapa ulipo na unapielekea,
ASANTE MAMA SAMIAH.
 
Uchumi unakuwa Huku tunakopa ili serikali iweze kulipa madeni ya Hatifungani? Basi itakuwa uchumi tafakari yake ni ngumi kuelewa kama ilivyo ngumi kuelewa Neno la Mungu ambalo linahitaji jicho la roho

Umepatia hapo tu kuelewa uchumi ni ngumu hasa kama huna taaluma hiyo
 
Uchumi unakua lakini Kodi haikusanywi,

Inabidi ichukue MKOPO mpya tri 5, kulipa deni la MKOPO wa nyuma!!

Uongo una mwisho, tumekaribia mwisho.

Nakukumbusha msikilize Vice wa US kasemaje kuhusu Uchumi wa taifa letu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…