secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 2,998
- 4,948
Huyu Mchungaji watu wanamweshimu sana kutokana na uwezo wake wa kuangusha watu kwenye madhabahu Kwa maombi makali, pia alikuwa vizuri katika kunena Kwa lugha. Siku moja alitaka anifanyie toba ili nipate kuokoka nami nikamkubalia Kwa masharti ya kunijibia maswali kadhaa naye alinikubalia na mazungumzo yetu yalikuwa kama ifuatavyo:-
MIMI: Mchungaji kwa nini mtu akifa huwa mnasema "bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake lihimidiwe" au wakati mwingine mnasema "kazi ya mungu haina makosa"
MCHUNGAJI: Kwa sababu mungu ndiye anayemleta mtu hapa duniani na mwenye uwezo wa kumchukua yaani kumtwaa.
MIMI: Kwa hiyo mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kuichukua roho ya mtu, si ndiyo?
MCHUNGAJI: Ndiyo maana yake.
MIMI: Na mungu ndiye anayepanga namna binadamu atakavyokufa, yaani yeye ndiye hupanga labda mtu atakufa Kwa kuugua kichwa, kuugua tumbo, kupigwa radhi na kadhalika.
MCHUNGAJI: Hivyo ndivyo inavyokuwa.
MIMI: (Baada ya kunikubalia niliyoyasema kwenye swali lililotangulia nilijisemea ndege amenasa kwenye tundu) Sasa Kwa nini mtu akifa Kwa kuuawa na mtu mwingine yule mtu anayesababisha kifo cha marehemu anahesabika kuwa mwenye dhambi wakati mungu ndiye alinayepanga kwamba kifo cha marehemu kingesababishwa na mtu mwingine?
MCHUNGAJI: (Akijifanya amepigiwa simu, aliliongea kwenye simu na kuonesha sura ya kupanic) "...amefariki!, mama yangu.... Duh..."
Oya min -me Mbaga Jr, Kumbe chungaji wa watu maswali yalimwelemae akajifanya amepigiwa simu ili anitoroke.
Kweli alinitoroka.