Mchungaji apigwa na wananchi wa Kigoma kwa kuzuia waganga wa kienyeji "Kamchape" wasiingie eneo la kanisa kutafuta uchawi

Ndio maana mambo yanazidi kwenda kombo.
 

Hakuna kitu kinaumiza kama msomi uwe katikati ya wajinga.

Watakulazimisha ukubali imani zao za ushirikina kinguvu. Ukipinga unasingiziwa mchawi
 
Ingawaje uchawi upo

Lakini sasa hii njia wanayoitumia hao kamchape ,haifai

Kwanza waganga nao ni wachawi
 
Hakuna kitu kinaumiza kama msomi uwe katikati ya wajinga.

Watakulazimisha ukubali imani zao za ushirikina kinguvu. Ukipinga unasingiziwa mchawi
almanusura watusingizie ni wachawi tulivyowapinga. Kwanza hatukuchanga ili mganga huyo atoe uchawi shuleni. Tuliona anafanya udanganyifu kwa kujifanya anafukua uchawi ardhini huku akikimbizana na jini alikamate na kulifungia kwenye kitambaa huku hatulioni. Hawa watu wanapaswa kukamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kuleta taharuki na uchonganishi katika jamii
 

Ha ha ha. Mimi nazijua mbinu zao.

Kuna video nyingi youtube za waganga wa zamani zinaleza jinsi waganga wanavyotapeli watu.

Hicho wanachofunika wanajifanya wanakikimbiza nakijua ni nini. Kinakuwa kina hema hema
 
Hawa watu hawatoi uchawi wala majini, wanachofanya ni maigizo tu. Unakuta wanavamia nyumba ya mtu na kudai kuna uchawi. Waliwahi kumjeruhi titi bibi mmoja kwa kumchanja na kitu chenye ncha kali wakidai mwilini mwake kuna uchawi wanamtolea kwa nguvu bila ridhaa yake. Wale huenda nyumba ambazo wamedokezwa kuwa yumkini mkazi wa hapo anaamini ushirikina au kwenda kumdhalilisha tu kuwa ni mchawi. Ni washenzi afadhali ya wale wanaofanya mazingaombwe hawadhalilishi watu
 
Pole Mkuu Kigoma napaelewa vyema
 
Acheni kuwa nyoronyoro, wapeni kipigo cha haja mpaka wajisaidie haja kubwa hadharani, hawatarudi tena, Kijiji na wananchi wake wake chini wapitishe azimio huo upuuzi ni marufuku atakayekaidi afanywe mfano, wataacha
 
"Nikapiga simu polisi ...polisi hawaji
Piga simu polisi hawaji
Nikampigia simu baba askofu alikuwa Dodoma
Ndipo naye akapiga simu polisi baadaye wakaja"

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…