Mchungaji Atuganile Mwakyosa aanika machafu yote ya Martha Mwaipaja akidai anafanya matendo machafu kinyume na tamaduni za Tanzania

ni kweli, labda tuangalie ni nini kinasababisha anguko kubwa la waimbaji wa injili hususani wa kike, je ni kiburi cha uzima, ni fedha au uzinzi?
 
Jaribu la mtu si kama ni mtenda dhambi ila ni kikombe tuu lazima akinyweee
 
Martha mwenyewe kimyaaa. Kaa kimya mwaya😀
 
Inawezekana huyo mchungaji alisagwa kama ni kweli amesema hayo maana nimesoma title tu. Inabidi na yeye atubu. Vinginevyo ni mchungaji mpenda kiki na mchumia tumbo.
 
Je hilo ni jukwaa sahihi la kusigana?

Wenye akili tushajua maslahi binafsikwa upana wake hapo.
 
Dini zote zinakataza kueneza uchafu na aibu za watu
Je huyu ni mchungaji kweli?
Mbona mafundisho yanakataza huu unafiki na adhabu yake ni kali sana?
Yuko sahihi kwa mujibu wa neno hili

2 Timotheo 4: 2 "....... karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho."

Isaya 58:1 "Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…