Mchungaji Daniel Mgogo ni mchungaji wa dini au ni motivational speaker?

Mchungaji Daniel Mgogo ni mchungaji wa dini au ni motivational speaker?

Naomba kujua kutoka kwa waumini wa huyu mchungaji Mgogo, je ni mchungaji wa dini au ni mtia hamasa(motivational speaker) wa dini?

Hua naona watu wengi wanapenda kuweka video clips za mahubiri yake kwenye social media statuses ila hakuna mahala au sijawahi kusikia akinukuu vifungu vya dini yake. Je ni mchungaji au ni motivational speaker? Yeye na mchungaji mitimingi wana uhusiano wowote?

Ahsante.
hakuna mchungaji Wa dini
!!
Dini haichungwi
 
Usimtazame mchungaji anacho sema bali fuata yale yalio muhimu Mungu amemfunulia

Hii ndio concept ya hovyo sana ya dini!

Ndio inafanya dini inakua very dangerous!

Yaani unamtoa dhamana muhubiri kwa kile anachokiwakilisha kwa wasiojua lolote which is nonsensical kabisa!

Hii inaitwa religious catastrophe!
 
watu wana crop, na kupost kile wanacho vutiwa navyo. sehemu ulyio isikia na kuiona i bet ni kijipande tu katika mahubiri yake, muda ule wa kutoa mifano n.k

ngumu kukuta watu wanapost mahubiri au vipande vinavyo toa ngumu chungu, kukemea dhambi n.k

lakini pia lengo la kuchunga ni ku guide, na hizo ni sehemu za ku guide.
Well said
 
Mchungaji mgogo anahubiri maisha halisi kabisa wanayoyaisha watu kila siku!

Mlishazoea kudanganywa na matapeli akina Gwajima na makasisi uchwara wanaokula sadaka kama mchwa!

Mimi sio mtu wa makanisa kanisa sana lakini navutiwa na staili ya mahubiri ya mgogo maana yanagusa maisha ya kawaida kabisa ambayo mtu yeyote anaweza kuyaishi!

Ana talanta ya ucheshi pia, kitu ambacho kinamfanya azidi kuvutia zaidi. Hachoshi kumsikiliza!
 
nilimsikia kwenye radio interview aliulizwa swali hilo alichojibu ni sawa na comment ya kwanza hapo juu
 
Hii ndio concept ya hovyo sana ya dini!

Ndio inafanya dini inakua very dangerous!

Yaani unamtoa dhamana muhubiri kwa kile anachokiwakilisha kwa wasiojua lolote which is nonsensical kabisa!

Hii inaitwa religious catastrophe!
Ni sawasawa na mafarisayo, walikuwa wanafundisha watu sheria ya Musa lakini wao kwa matendo yao hawakuifuata. Basi Yesu akawambia "Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa, fuateni wanayosema bali msifuate wanayotenda"
 
Watu wanamchukua vipande, NENO au mahubiri saa 1 mpaka na 1 na nusu sasa kakipande ka dakika 2 katakua na nini hapo
 
Ni sawasawa na mafarisayo, walikuwa wanafundisha watu sheria ya Musa lakini wao kwa matendo yao hawakuifuata. Basi Yesu akawambia "Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa, fuateni wanayosema bali msifuate wanayotenda"

Yesu concept again!
 
Yupo vizuri sana, anaandaa hadi semina za kuwafundisha wachungaji na viongozi wengine wa kanisa.
Hahaha...wewe jamaa unadadisi sana, anyway katika watu ninaowakubali zaidi katika kufundisha neno la Mungu ni mwalimu Mwakasege na anadai hakupita hata bible school.
 
Mitimingi ni nabii wa shetani.Ana promote ngono balaa!
Naomba kujua kutoka kwa waumini wa huyu mchungaji Mgogo, je ni mchungaji wa dini au ni mtia hamasa(motivational speaker) wa dini?

Hua naona watu wengi wanapenda kuweka video clips za mahubiri yake kwenye social media statuses ila hakuna mahala au sijawahi kusikia akinukuu vifungu vya dini yake. Je ni mchungaji au ni motivational speaker? Yeye na Mchungaji Mitimingi wana uhusiano wowote?

Ahsante.
 
Hizo clip anaweka mwenyewe hivyo na yeye amepapenda hapo alipoonyesha kwenye clip hasa YouTube.
 
Back
Top Bottom