BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Picha: Mchungaji Eliona Kimaro
Semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT Kijitonyama ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo.
Mchungaji Kimaro amesema anatumia fursa hiyo kuwaaga Washarika wake na kuanzia Januari 17 Mchungaji Anna ataendelea kuwa kiongozi wa Kanisa hilo.
Kwa mujibu wa barua, Mchungaji Kimaro atamaliza likizo yake ya lazima 17/03/2023 na barua inamuelekeza kuripoti makao makuu na sio usharika wa KKKT Kijitonyama ambapo atapangiwa sehemu nyingine.
Video: Mchungaji Kimaro akiwaaga waumini
"Mimi ni Mchungaji wa Lutheran ninayeheshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo changu cha kichungaji na maadili pia ya kichungaji kwa neema ya Mungu. Kwa sababu hiyo imenilazimu kutii amri na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti kwenye ofisi ya Askofu kama nilivyoelekezwa" Asante.
Video: Mchungaji Kimaro akiombea Waumini baada ya kuaga
UPDATES
Baadhi ya Waumini wa KKKT wajitokeza kupinga uamuzi wa Mchungaji Kimaro kupewa likizo
Waumini Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama wamekubaliana kutoingia ndani ya Kanisa hilo hadi watakwporudishiwa Mchungaji wao Dk Eliona Kimaro aliyepewa likizo ya siku 60.Uamuzi huo umefikiwa na waumini hao baada ya kukubaliana kufanya maandamano ya amani katika viwanja vya kanisa hilo hadi pale mchungaji wao atakaporudishwa au kupewa sababu za kupewa likizo hiyo.
Tazama baadhi ya video hapa chini:
Video hizo hapo juu zinawaonesha Waumini wa KKKT Usharika wa Kijitonyama wakipinga mchungaji wa usharika huo Dkt. Eliona Kimaro kupewa likizo ya siku 60.
PIA SOMA:
1. KKKT ni kubwa kuliko Mch. Kimaro, msihuzunike kuna jambo hamlijui, viongozi wake hawajakurupuka
2. Projects za Mchungaji Kimaro akiwa KKKT Kijitonyama
3. Kwenye sakata la Mchungaji Kimaro, nasimama na Kiongozi wangu Askofu Malasusa