Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Migogoro katika kanisa imeanza muda mrefu enzi za waanzilishi wa kanisa.

Kati ya wale wanafunzi wa yesu ambao ndio mwanzo wa kanisa ulianzia kwao nao walikuwa na mafarakano baina yao dhidi ya waamini .

Mwingine aliona yeye ni bora kuliko yule na yule alijiona ni bora kuliko huyo , waathirika wakubwa .

Baadhi ya taasisi za makanisa wamekua na mfumo mzuri wa kutatua migogoro yao bila waumini kuathirika, lakini taasisi nyingine athari zimekua kubwa mno na kupelekea kugawanyika kwa waamini .

Yote ya yote ni maslahi ya kidunia na wala sio maslahi ya kiimani.
 
Tatizo la KKKT limemuacha Kimaro akae hapo Kijitonyama muda mrefu mpaka akasahau kama yeye ni mtumishi wa Dayosisi ya mashariki na Pwani akaona kama vile kanisa la kijitonyama ni lake mbina pale msasani wachungaji hawakai muda mrefu?
 
Mimi ni muislamu lakini nasema huyu Pastor Kimaro ni bonge la Pastor na waliomfanyia hizo figisu hawana roho wa Mungu ndani yao.

# Baba Kimaro kama unasoma UJUMBE huu please tunaomba tunaomba ufungue kanisa lako.

Siku 60 ni nyingi sana.

😭😭😭😭😭😭
 
Ukisikia Yalaah.........

Kwa sababu hiyo imenilazimu kutii amri na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti kwenye ofisi ya Askofu kama nilivyo elekezwa" Asante
Imenilazimu, ni kauli ya kutokubaliana na kilichopo. Angesema tu, ninatii amri.

akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake
Nimeona video hapa



Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazo imba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu,
😅😅😀🤣 6 tu
 
Nilijua ipo siku KKKT watamfyatua out aidha kwa figisufigisu ili akimbie mwenyewe.KKKT haipendagi mtu alinyooka ktk ukweli,sasa jamaa uwa yupo straight forward uwa hapindipindi hata kidogo,so kwa Lutheran hiyo ni kasoro,pia kuna ngoma nyingine Askofu Bagonza huyu nae ni kisiki hawana cha kumfanya make huyu nae ni kichwa kingine ambacho kimenyooka na hakuna mtu mwenye uwezo nacho ndani ya KKKT
Sio kweli, hebu tuwe na subira kidogo
 
Kufuatia semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT KIJITONYAMA ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo...
Afadhali.... Sikio halizidi Kichwa. Huyu alianza kuota mapembe, kuwa jeuri na kiburi. Hata hivyo wamemvumilia sana nadhani wakiamini angebadilika. Asingebadilika. Sababu alishakuwa na kiburi kilichokomaa. Sasa aakaanzishe Kanisa lake maana hapo hakatazwi.
 
Mimi ni muislamu lakini nasema huyu Pastor Kimaro ni bonge la Pastor na walio mfanyia hizo figisu hawana roho wa Mungu ndani yao.

# Baba Kimaro kama unasoma UJUMBE huu please tunaomba tunaomba ufungue kanisa lako.

Siku 60 ni nyingi sana.

😭😭😭😭😭😭
Huyo Kimaro na Mgogo ndiyo wanalibeba kanisa, shida ni kwamba kazi ya Mungu lazima ipate upinzani wa shetani na hao wanao mletea figisu ndiyo mashetani wenyewe
 
Kwenye hili nahisi pastor kimaro ataenda kujitafakari
Mimi ni muumini wa KKKT hapo kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji kimaro ni kwamba alikua anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alisha onywa zaidi...
Kwamba si mtii si kweli, hata kusimamishwa ametii hadharani na ame address viongozi wake kwa heshima zote. Hapo naona umetoa allegations nyingi za uongo ingawa mimi si muumini wa Lutheran!

Kusema hafati ratiba ya Kanisa si kweli, sema huwa anakuwa na ratiba za ibada ya huduma yake nje ya litrujia ya kawaida mfano mafungo maalum.

Huyu mchungaji ana kundi kubwa la watu ambao hata si walutheri, hiyo pekee ni huduma na Kanisa lingepaswa kumsaidia kumlea ili aweze kuhudumia hao. Hata Mwakasege ambaye ni Mlutheri injili yake haina mipaka ndio maana pamoja na kutii ibada ya Kanisa lake lakini ana huduma yake.

Nafikiri Mchungaji Kimaro hajapata Askofu wa kuelewa huduma yake, wanataka awe kawaida afanye huduma kama kila mchungaji.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kwamba si mtii si kweli, hata kusimamishwa ametii hadharani na ame address viongozi wake kwa heshima zote. Hapo naona umetoa allegations nyingi za uongo ingawa mimi si muumini wa Lutheran...
Hapana. Jamaa alikuwa na kibri sana. Mimi nimemsikiliza mara nyingi. Hili la ibada ya mwisho sikuwepo. Ila amekuwa mtu wa madongo kwa wenzie na kutofuata taratibu. Anaongea mpaka wakati mwingine anapitiliza. Mi nadhani aanzishe tu Kanisa lake. Atapata waumini wengi tu
 
Huyo Kimaro na Mgogo ndiyo wanalibeba kanisa, shida ni kwamba kazi ya Mungu lazima ipate upinzani wa shetani na hao wanao mletea figisu ndiyo mashetani wenyewe
Wanalibeba kanisa maana yake Nini?

Unadhani kanisa Ni label ya mziki kwamba msanii flani anaibeba hio label na akiondoka shughuli imeisha?

Hakuna mkubwa kuliko taasisi.
 
Nimezaliwa katika familia ya kiluteri na kupata hadi kipaimara ila mambo hata ya migogoro upande wa viongozi yalinikera ukifuatilia chanzo pesa afu michango karibia mitano lol niliamua niwe tu nasali kwa ukawaida kwa mashahidi wa yehova watu walio na upendo wa hali ya juu wakiyaishi maisha ya viwango ya kikristo kwa matendo.kwanza kkkt inashangaza eti mtu anaweza akaacha kanisa lake la kkkt mtaani ila akawa anaenda kusali usharika wa kimara eti kisa mchungaji wa kimara anamvutia swali je akifa huyo mchungaji utaendelea kwenda huo usharika????
Hilo ni tatizo na ugonjwa sugu, nadhani kunakuwa na vitu mfano wa vikoba, huwa nashangaa sana kwa hili.
 
Kufuatia semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT KIJITONYAMA ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo...
Atoke akaanzishe kanisa lake mwenyewe, Makanisa nayo yana likizo, yaani mchungaji unakuwa umeajiriwa?kwani ni kampuni hiyo?uchungaji ni wito sio ajira,mtafanya watu wa act kua wachungaji ili waajiriwe nyie,jua ni kali sana mtaani 😂😂

ndio maana nilienda zangu mashahidi wa jehova
 
Back
Top Bottom