Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Kuna maneno niliyasikia juuu yake nikasema kama ni kweli basi anakosea kikubwa kumuombea
 
Ila kkkt mmezidi. Mpunguze migogoro. Jifunzeni kutoleta mambo yenu mitandaoni.
Kwetu huwezi kusikia mambo yanaletwa hadharani kiasi hiki.
Sio kwamba hayapo yanakuwepo maana popote walipokusanyika watu lazima migogoro iwepo.
Kwenu wapi
 
Nafikiri shida ni kanuni na taratibu. Kuna muda lazima tukubali kuzifuata na kama hatupendi tutafute njia stahiki za kubadili kanuni na taratibu hizo. Kama inashindikana unawaachia taratibu zao unaenda kufanya kinachoendana nawe.
 
Uko sahihi sana, wahavivina wanataka makanisa yasiyosali wala kufundisha kweli waende kule kulala, wafanye dhambi bila kukemewa, makanisa ya aina hiyo ambako hata mapepo hayafukuzi ni sawa na baa za pombe tu.

Kanisa lazima liwe na nguvu aisee, watu wako na mashida mengi na wa nahitaji solutions kutoka kwa Mungu kupitia wachungaji.
 

Kwa hili shetani atakuwa kanyakua kombe kabisa. Au kuna wakuu wa hilo kanisa machawi? Au maabudu shetani so wanapata tabu sana kuona maombi yanapigwa na neno linahubiriwa pale?

Uamsho wa kanisa lazima uanzie ndani ya kanisa na mwenye kanisa ni Yesu sio dayosisi na makorokoro mengine.
 
Law 1: Never outshine the master

Make your masters appear more brilliant than they are and you will attain the heights of power

When it comes to power, outshining the master is perhaps the worst mistake of all.

Never take your position for granted and never let any favors you receive go to your head.
 
Uko sahihi,Kanisa ni mali ya Mungu na Kanisa ni lazima litoe suluhisho la matatizo ya watu,ndio maana mimi huwa napingana na watu ambao wakiona kuna mtumishi anaombea watu wapone magonjwa au kupata ndoa nk wanaitwa matapeli,hatuwezi kuwa tunaenda kanisani kama sehemu ya utamaduni,kanisani natakiwa nipeleke shida zangu zitatuliwe,iwe ni kimbilio langu.

Ila kuhusu huyu Mchungaji alipaswa aombe hekima ya namna ya kuchunga kondoo hasa akijua kwamba anahudumu kupitia taasisi yenye taratibu zake ambazo amekula viapo.vinginevyo achukue njia kama ya Mwakasege ili Kristo aendelee kuhubiriwa.
 
Ndio maana nikasema yeye ndio kayaleta mitandaoni,na ndio hapo unaona kwamba hapo yeye ndio kakosa busara kwa namna alivyoongea kana kwamba anataka watu wahisi kuna kitu kimejificha
 
Tokea lini wa KKT wakawa na wachungaji wanawake
Mbona wapo wengi tu ,Hata Msasani Lutheran mchungaji msaidizi ni mwanamke,Mbezi beach alikuwepo yule mama wa kizungu amestaafu nafikiri mwaka jana alikuwa anaongoza ibada ya Kiingereza.
 
Shida ni kwamba siku akiona maji shingoni na akaamua kung'atuka!!! Atasepa na kondoo wengi sana, tuombe yasitokee hayo, make hata mimi wa huku mbali namkubali haswa.
Haina mashiko, makanisa na kama zilivyo taasisi zingine hukumbana na changamoto kama hizi na inajua namna ya kuzishughulikia.

Hatua waliyochukua ni nzuri sahihi na ya kitaasisi, wao watafanya uchunguzi wao watakuja na majibu na si lazima watutangazie. Wakatoliki huwa wana (tuna) utaratibu ulionyooka kwa wale wanaoenda kinyume na taratibu za Kanisa, ukileta za kuleta wanakususpend au ban na hakuna hata anayejua kinachoendelea na wala wa kulalamika.

Mifano ni mingi; Askofu Milingo, Pd Nkwera, Dr Slaa, Padre mmoja mkenya na orodha ni ndefu. Ila hasa Lutheran wanalea sana vimelea vya watumishi kuwapanda vichwani.

All in all huwezi jifanya uko juu ya taasisi inayokusimamia/ajiri na ukabaki salama. NEVER.
 
Our master is the Lord Jesus Christ. Alisema kwenye occasion fulani "Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, bali mwanafunzi atafanana na mwalimu wake anapofuzu mafunzo yake".

Tatizo makanisa mengi ya KKKT wanataka yawe kama saccos au chama cha siasa badala ya kuwa nyumba ya sala ya kumwadhimisha Mungu kwa Roho na kweli.
 
Maneno AMA na KAMA yanaonyesha ni dhahiri na wewe unahisi tu. Ukitoa hukumu toa kwa uhalisia na si hisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…