Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Kuna maneno niliyasikia juuu yake nikasema kama ni kweli basi anakosea kikubwa kumuombea
 
Ila kkkt mmezidi. Mpunguze migogoro. Jifunzeni kutoleta mambo yenu mitandaoni.
Kwetu huwezi kusikia mambo yanaletwa hadharani kiasi hiki.
Sio kwamba hayapo yanakuwepo maana popote walipokusanyika watu lazima migogoro iwepo.
Kwenu wapi
 
Kkkt ni platform, yeye ana kipaji, sasa tuue kipaji kwasababu za wivu? Shetani amewazidi uwerevu?

Kwani huyo mchungaji ana hubiri Quran? Si vitabu vya kikristu? Amehubiri mambo ya kumpinga kristu? Shida yenu ni nini? Kukubalika kwake, kupendwa kwake?kipaji chake?
Nafikiri shida ni kanuni na taratibu. Kuna muda lazima tukubali kuzifuata na kama hatupendi tutafute njia stahiki za kubadili kanuni na taratibu hizo. Kama inashindikana unawaachia taratibu zao unaenda kufanya kinachoendana nawe.
 
Mimi ni muislamu lakini nasema huyu Pastor Kimaro ni bonge la Pastor na waliomfanyia hizo figisu hawana roho wa Mungu ndani yao.

# Baba Kimaro kama unasoma UJUMBE huu please tunaomba tunaomba ufungue kanisa lako.

Siku 60 ni nyingi sana.

😭😭😭😭😭😭
Uko sahihi sana, wahavivina wanataka makanisa yasiyosali wala kufundisha kweli waende kule kulala, wafanye dhambi bila kukemewa, makanisa ya aina hiyo ambako hata mapepo hayafukuzi ni sawa na baa za pombe tu.

Kanisa lazima liwe na nguvu aisee, watu wako na mashida mengi na wa nahitaji solutions kutoka kwa Mungu kupitia wachungaji.
 
Kkkt ni platform, yeye ana kipaji, sasa tuue kipaji kwasababu za wivu? Shetani amewazidi uwerevu?

Kwani huyo mchungaji ana hubiri Quran? Si vitabu vya kikristu? Amehubiri mambo ya kumpinga kristu? Shida yenu ni nini? Kukubalika kwake, kupendwa kwake?kipaji chake?

Kwa hili shetani atakuwa kanyakua kombe kabisa. Au kuna wakuu wa hilo kanisa machawi? Au maabudu shetani so wanapata tabu sana kuona maombi yanapigwa na neno linahubiriwa pale?

Uamsho wa kanisa lazima uanzie ndani ya kanisa na mwenye kanisa ni Yesu sio dayosisi na makorokoro mengine.
 
Law 1: Never outshine the master

Make your masters appear more brilliant than they are and you will attain the heights of power

When it comes to power, outshining the master is perhaps the worst mistake of all.

Never take your position for granted and never let any favors you receive go to your head.
 
KANISA NI MALI YA MUNGU, sio saccos za KKKT. Mungu huabudiwa kwa roho, na kanisa halisi la Mungu lazima litoe solutions za matatizo ya waumini wake through maombi, na mafundisho yenye uzima. Zama za kufuatisha liturugia mpaka watu wanasinzia zimekwisha. Nawaunga mkono hawa pastors Kimaro na mastai at least wameleta uhai kwenye ibada za KKKT.
Kama kweli wanafanya hayo kwa ajili ya Kristo, hata wakiwatimua halafu wakaamua kuwa na huduma zao still watapata followers wa kutosha.
Uko sahihi,Kanisa ni mali ya Mungu na Kanisa ni lazima litoe suluhisho la matatizo ya watu,ndio maana mimi huwa napingana na watu ambao wakiona kuna mtumishi anaombea watu wapone magonjwa au kupata ndoa nk wanaitwa matapeli,hatuwezi kuwa tunaenda kanisani kama sehemu ya utamaduni,kanisani natakiwa nipeleke shida zangu zitatuliwe,iwe ni kimbilio langu.

Ila kuhusu huyu Mchungaji alipaswa aombe hekima ya namna ya kuchunga kondoo hasa akijua kwamba anahudumu kupitia taasisi yenye taratibu zake ambazo amekula viapo.vinginevyo achukue njia kama ya Mwakasege ili Kristo aendelee kuhubiriwa.
 
Kwani si kaenda likizoo...!! Mchungaji kupewa likizo jambo la kawaida sema yeye ndo kayakuzaaa kuonesha kuwa kaonewaaa... aina ya wachungaji ambao usharika ukikuaa na wao ndo wameweka nguvu kuukuza huwa wana changamoto sana za kuongozaaa wao wako mbele sana kukemea ila ukweli na wao ni wachafu vile vile.
Ndio maana nikasema yeye ndio kayaleta mitandaoni,na ndio hapo unaona kwamba hapo yeye ndio kakosa busara kwa namna alivyoongea kana kwamba anataka watu wahisi kuna kitu kimejificha
 
Tokea lini wa KKT wakawa na wachungaji wanawake
Mbona wapo wengi tu ,Hata Msasani Lutheran mchungaji msaidizi ni mwanamke,Mbezi beach alikuwepo yule mama wa kizungu amestaafu nafikiri mwaka jana alikuwa anaongoza ibada ya Kiingereza.
 
Shida ni kwamba siku akiona maji shingoni na akaamua kung'atuka!!! Atasepa na kondoo wengi sana, tuombe yasitokee hayo, make hata mimi wa huku mbali namkubali haswa.
Haina mashiko, makanisa na kama zilivyo taasisi zingine hukumbana na changamoto kama hizi na inajua namna ya kuzishughulikia.

Hatua waliyochukua ni nzuri sahihi na ya kitaasisi, wao watafanya uchunguzi wao watakuja na majibu na si lazima watutangazie. Wakatoliki huwa wana (tuna) utaratibu ulionyooka kwa wale wanaoenda kinyume na taratibu za Kanisa, ukileta za kuleta wanakususpend au ban na hakuna hata anayejua kinachoendelea na wala wa kulalamika.

Mifano ni mingi; Askofu Milingo, Pd Nkwera, Dr Slaa, Padre mmoja mkenya na orodha ni ndefu. Ila hasa Lutheran wanalea sana vimelea vya watumishi kuwapanda vichwani.

All in all huwezi jifanya uko juu ya taasisi inayokusimamia/ajiri na ukabaki salama. NEVER.
 
Law 1: Never outshine the master

Make your masters appear more brilliant than they are and you will attain the heights of power

When it comes to power, outshining the master is perhaps the worst mistake of all.

Never take your position for granted and never let any favors you receive go to your head.
Our master is the Lord Jesus Christ. Alisema kwenye occasion fulani "Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, bali mwanafunzi atafanana na mwalimu wake anapofuzu mafunzo yake".

Tatizo makanisa mengi ya KKKT wanataka yawe kama saccos au chama cha siasa badala ya kuwa nyumba ya sala ya kumwadhimisha Mungu kwa Roho na kweli.
 
Hana lolote huyo!

Ukimsoma vizuri kwa utulivu utagundua yeye Kuna mawili;
1. Ama ndiye Mchungaji Anna
Au
2. Ni wale wanafiki na mahasidi wa kanisa.

Wachawi nao wanasali makanisani!

Lakini Pastor Kimaro kama mmemuonea mjue Mungu anaenda kumuinua zaidi.

Roho wa Mungu ampe subira na hekima kuvuka jaribu hilo.

Ikimpendeza Roho namshauri afanye kama huduma ya Mwakasege.

Au aanzishe kanisa .
Maneno AMA na KAMA yanaonyesha ni dhahiri na wewe unahisi tu. Ukitoa hukumu toa kwa uhalisia na si hisia.
 
Back
Top Bottom