Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Tatizo la KKKT limemuacha Kimaro akae hapo Kijitonyama muda mrefu mpaka akasahau kama yeye ni mtumishi wa Dayosisi ya mashariki na Pwani akaona kama vile kanisa la kijitonyama ni lake mbina pale msasani wachungaji hawakai muda mrefu?
..wala hajakaa hapo kijitonyama muda mrefu kivile...
Ni miaka minne na miezi tu. Kabla alikuwa kariakoo ambapo alidumu miaka zaidi ya 10
 
Anaitwa Mastai.

Hawa jamaa wanaogopeka sana.

Alikuwa Richard Hanaja.
Eliona kimaro.
Na MASTAI.

Hawa jamaa Wana uwezo mkubwa lakini wapo chini ya kanisa. Shida wanaota mapembe.

Sikio linataka kuzidi Kichwa.

Hakuna anaye waogopa Basi tu wanawaheshimu.
 

Hapana huyu kuna vitengo vyake vya maombezi aliamzisha pamoja na tv yake on line ilimpa sana hela hii huduma hivyo pamoja na kusimishwa kuna wivu fulani wa kipato huenda hakunyoosha mkono kwa wakubwa.

Bado yule wa kimara ila yule mjanja anakula na wakubwa ndio maana pale yeye kawa msimamizi kawekewa mwingine kiujanja wanaongoza nae pale
 
Ilikua ku waalert kanisa kama sijasahau kuna kijana ndani ya kanisa alipewa
Mkopo akadai ameibiwa na akajinyonga sioni changamoto yoyote kwenye kauli ya kuwaweka sawa wakristo wawalee watoto wao sawa
 
Ilikua ku waalert kanisa kama sijasahau kuna kijana ndani ya kanisa alipewa
Mkopo akadai ameibiwa na akajinyonga sioni changamoto yoyote kwenye kauli ya kuwaweka sawa wakristo wawalee watoto wao sawa
Alikuwa wa kanisa hili hili???
 
Asubuhi kabla nikiwa najiandaa kwenda kwenye shughuli zangu niliwawawza hawa wachungaji lakini hasa huyu wa Kimara na lawama zangu zikawa kwa viongozi wao.

Kwanza niseme wazi sina matatizo binafsi na hawa wachungaji, nawaelewa sana japo sipo KKKT lakini kwa kadri nionavyo imefika wakati wahamishwe ili kanisa mahalia liendelee kuponya nafsi na mioyo ya watu.

Ukweli ni kwamba imefika wakati waumini wao hasa wanawake nafsi zao zimeshikamana na hawa wachungaji kiasi kukosa nidhamu kwenye familia.

Kiukweli hebu wapewe majukumu mengine tutaendelea kukutana nao u-tube kwa kuwa mijadala yao huwa iko edited na msg za maana tunapata, kwa hili nawapongeza KKKT Ni matumaini yangu wachungaji watakuwa watii japo naelewa wafuasi wake ambao nafsi zao zimeshikamana na nao wanafunga na kusali mabadiliko yasitokee na pale huruma ya askofu itakapotokea na kuamua kutengua uamuzi wake itasomeka kuwa Bwana katenda.
 
Kimaro aliwasifu mapadre wakatoliki na kanisa la RC kwa mfumo mzuri ...nadhan wakubwa was kanisa lake hawakupenda
Hilo la kusifu mapadre na kanisa la RC wala si tatizo kabsaaa liliosababisha kusimamishwa kwake, mkuu we soma comment #15 aliyoandika 1-mother kafafanua vizuri sana kama hutamuelewa.. basi tuu
 
KIMARO itakuwa kwenye miradi yake nje ya kanisaa vijana walimpigaa helaa snaaa πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€yani katusema vijana wa kikristo kwa uchungu mwingi kuwa sisi ni weziiii ila ninachojua wizi hauna diniiii... Alikosea kuchanganya wajibu wake na maslahi yake binafsi.
 
Kabisa ila watu hawalioni hili
Ila ni jambo la ajabu hkianza kuwafatilia hawa wachungaji utagundua kuna kitu wanafanya
 
Kabisa sema watu wana mihemko tu hawajui kinacho endelea
Ila jamaa ana kiburi balaa na haishimu mamlaka wala viongozi
 
Sahihi kabisa,
Hakuna mkubwa kuliko kanisa
 
Nilihisi hiki kitu. Makanisa kama KKKT, Anglican na RC yanaongozwa kitaasisi.. nilivyomuona Kimaro nilijua tu kuna kamba ameiruka na atafyatuliwa tu.

Nampenda lkn akiamua kuwa KKKT basi na ayafuate ya KKKT
Kabisa umeongea kweli
Ukitaka utaratibu wako unafungua tu kanisa na kuanzisha ya kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…