Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Tatizo la KKKT limemuacha Kimaro akae hapo Kijitonyama muda mrefu mpaka akasahau kama yeye ni mtumishi wa Dayosisi ya mashariki na Pwani akaona kama vile kanisa la kijitonyama ni lake mbina pale msasani wachungaji hawakai muda mrefu?
..wala hajakaa hapo kijitonyama muda mrefu kivile...
Ni miaka minne na miezi tu. Kabla alikuwa kariakoo ambapo alidumu miaka zaidi ya 10
 
Anaitwa Mastai.

Hawa jamaa wanaogopeka sana.

Alikuwa Richard Hanaja.
Eliona kimaro.
Na MASTAI.

Hawa jamaa Wana uwezo mkubwa lakini wapo chini ya kanisa. Shida wanaota mapembe.

Sikio linataka kuzidi Kichwa.

Hakuna anaye waogopa Basi tu wanawaheshimu.
 
Nilijua ipo siku KKKT watamfyatua out aidha kwa figisufigisu ili akimbie mwenyewe.

KKKT haipendagi mtu alinyooka ktk ukweli, sasa jamaa huwa yupo straight forward huwa hapindipindi hata kidogo, so kwa Lutheran hiyo ni kasoro, pia kuna ngoma nyingine Askofu Bagonza huyu nae ni kisiki hawana cha kumfanya make huyu nae ni kichwa kingine ambacho kimenyooka na hakuna mtu mwenye uwezo nacho ndani ya KKKT.

Hapana huyu kuna vitengo vyake vya maombezi aliamzisha pamoja na tv yake on line ilimpa sana hela hii huduma hivyo pamoja na kusimishwa kuna wivu fulani wa kipato huenda hakunyoosha mkono kwa wakubwa.

Bado yule wa kimara ila yule mjanja anakula na wakubwa ndio maana pale yeye kawa msimamizi kawekewa mwingine kiujanja wanaongoza nae pale
 
Ilikua ku waalert kanisa kama sijasahau kuna kijana ndani ya kanisa alipewa
Mkopo akadai ameibiwa na akajinyonga sioni changamoto yoyote kwenye kauli ya kuwaweka sawa wakristo wawalee watoto wao sawa
 
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Asubuhi kabla nikiwa najiandaa kwenda kwenye shughuli zangu niliwawawza hawa wachungaji lakini hasa huyu wa Kimara na lawama zangu zikawa kwa viongozi wao.

Kwanza niseme wazi sina matatizo binafsi na hawa wachungaji, nawaelewa sana japo sipo KKKT lakini kwa kadri nionavyo imefika wakati wahamishwe ili kanisa mahalia liendelee kuponya nafsi na mioyo ya watu.

Ukweli ni kwamba imefika wakati waumini wao hasa wanawake nafsi zao zimeshikamana na hawa wachungaji kiasi kukosa nidhamu kwenye familia.

Kiukweli hebu wapewe majukumu mengine tutaendelea kukutana nao u-tube kwa kuwa mijadala yao huwa iko edited na msg za maana tunapata, kwa hili nawapongeza KKKT Ni matumaini yangu wachungaji watakuwa watii japo naelewa wafuasi wake ambao nafsi zao zimeshikamana na nao wanafunga na kusali mabadiliko yasitokee na pale huruma ya askofu itakapotokea na kuamua kutengua uamuzi wake itasomeka kuwa Bwana katenda.
 
Kimaro aliwasifu mapadre wakatoliki na kanisa la RC kwa mfumo mzuri ...nadhan wakubwa was kanisa lake hawakupenda
Hilo la kusifu mapadre na kanisa la RC wala si tatizo kabsaaa liliosababisha kusimamishwa kwake, mkuu we soma comment #15 aliyoandika 1-mother kafafanua vizuri sana kama hutamuelewa.. basi tuu
 
KIMARO itakuwa kwenye miradi yake nje ya kanisaa vijana walimpigaa helaa snaaa 😀 😀 😀 😀yani katusema vijana wa kikristo kwa uchungu mwingi kuwa sisi ni weziiii ila ninachojua wizi hauna diniiii... Alikosea kuchanganya wajibu wake na maslahi yake binafsi.
 
Asubuhi kabla nikiwa najiandaa kwenda kwenye shughuli zangu niliwawawza hawa wachungaji lakini hasa huyu wa Kimara na lawama zangu zikawa kwa viongozi wao.
kwanza niseme wazi sina matatizo binafsi na hawa wachungaji nawaelewa sana japo sipo KKKT lakini kwa kadri nionavyo imefika wakati wahamishwe ili kanisa mahalia liendelee kuponya nafsi na mioyo ya watu.
ukweli ni kwamba imefika wakati waumini wao hasa wanawake nafsi zao zimeshikamana na hawa wachungaji kiasi kukosa nidhamu kwenye familia.
kiukweli hebu wapewe majukumu mengine tutaendelea kukutana nao u-tube kwa kuwa mijadala yao huwa iko edited na msg za maana tunapata.
kwa hili nawapongeza KKKT Ni matumaini yangu wachungaji watakuwa watii japo naelewa wafuasi wake ambao nafsi zao zimeshikamana na nao wanafunga na kusali mabadiliko yasitokee na pale huruma ya askofu itakapotokea na kuamua kutengua uamuzi wake itasomeka kuwa Bwana katenda.
Kabisa ila watu hawalioni hili
Ila ni jambo la ajabu hkianza kuwafatilia hawa wachungaji utagundua kuna kitu wanafanya
 

Dayosisi imefanya maamuzi sahihi sana, na tena yamechelewa mno.

Huyu na mwenzake wa Kimara ni wachungaji wachache ndani ya kanisa wenye kiburi kilichokomaa na kuzeeka.

Mchungaji amekuwa mtu wa kusema hovyo ili kujipatia umaarufu wa kidunia, ni juzi tu ametoka kusema vijana wa kikristo hawaaminiki na yeye anawaamini sana vijana wa kiislam, hii sio kauli ya kusemwa na Mchungaji.

Mchungaji Kimaro kama kweli ana Mungu ndani yake, atumie hizo siku 60 kijitafakari na kufanya toba, kiburi chake kiliinuka zaidi na akataka kujitwalia utukufu wa Mungu.

Ni muda sasa KKKT iangalie sana watu wa kuwabariki kuwa wachungaji na kuwapa sharika, kutokana na ugumu wa ajira watu wengi wanapigania kuwa wachungaji ili kupata uhakika wa ajira hapo baadae. Kanisa lipime sana watu, lichuje kwa kumshirikisha Mungu.

Washarika wote wanamlilia Mchungaji wakae chini na wajitafakari kama ni wakristo kweli, wanaamini katika Mungu au katika Mchunga?


Kabisa sema watu wana mihemko tu hawajui kinacho endelea
Ila jamaa ana kiburi balaa na haishimu mamlaka wala viongozi
 
Askofu Malasusa anatakiwa kuwa mkali kidogo, amekuwa mpole na imekuwa ni nafasi kwa wachungaji kujiinua na kuwa viburi.

Huu ni muda wa kuwaonyesha hawa wachungaji kwamba kanisa ni la Mungu na sio mali yao wala umaarufu wao si kitu ndani ya kanisa.

Wakiachwa watalivunjavunja kanisa.
Sahihi kabisa,
Hakuna mkubwa kuliko kanisa
 
Nilihisi hiki kitu. Makanisa kama KKKT, Anglican na RC yanaongozwa kitaasisi.. nilivyomuona Kimaro nilijua tu kuna kamba ameiruka na atafyatuliwa tu.

Nampenda lkn akiamua kuwa KKKT basi na ayafuate ya KKKT
Kabisa umeongea kweli
Ukitaka utaratibu wako unafungua tu kanisa na kuanzisha ya kwako
 
Back
Top Bottom