Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Bora kidogo nimepata mwanga
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
 
Asante sana baba kwa ufafanuzi. Binafsi swala la Mch. Kimaro kuongea kauli tata zisizo na ushahidi/data limekuwa likinikera sana. Anyways, Mungu atuongoze katika hili.
 
Semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT Kijitonyama ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo.

Mchungaji Kimaro amesema anatumia fursa hiyo kuwaaga Washarika wake na kuanzia Januari 17 Mchungaji Anna ataendelea kuwa kiongozi wa Kanisa hilo.

Kwa mujibu wa barua, Mchungaji Kimaro atamaliza likizo yake ya lazima 17/03/2023 na barua inamuelekeza kuripoti makao makuu na sio usharika wa KKKT Kijitonyama ambapo atapangiwa sehemu nyingine.

Amesema:
"Mimi ni Mchungaji wa Lutheran ninayeheshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo changu cha kichungaji na maadili pia ya kichungaji kwa neema ya Mungu. Kwa sababu hiyo imenilazimu kutii amri na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti kwenye ofisi ya Askofu kama nilivyoelekezwa" Asante.
Kazi ya Dk Shoo na genge lake, hawataki mtu awazidi umaarufu.

Walianza kumuondoa Mwaikali. Ukiwazibia ulaji wanaweza hata kukuua
 
Mimi Nimezaliwa katika familia ya kiluteri na kupata hadi kipaimara ila mambo haya ya migogoro upande wa viongozi yalinikera ukifuatilia chanzo pesa halafu michango karibia mitano lol niliamua niwe tu nasali kwa ukawaida kwa mashahidi wa yehova watu walio na upendo wa hali ya juu wakiyaishi maisha ya viwango ya kikristo kwa matendo.

Kwanza KKKT inashangaza eti mtu anaweza akaacha kanisa lake la KKKT mtaani ila akawa anaenda kusali usharika wa Kimara eti kisa mchungaji wa Kimara ni maarufu anamvutia swali Je, akifa huyo mchungaji utaendelea kwenda huo usharika wa Kimara?
Kuwa KKKT hadi umri wa kipaimara ni miaka ya kujivunia kama mKKKT aliyekomaa kweli? Wacha kudanganya watu. Kipaimara ndo kwanza unakariri amri 10 za Mungu?!
 
Ndo maana mnadanganywa na kina Kimaro. Mussa na Eliya wapi na wapi?Baada ya Mussa aliinuliwa Joshua.

Binafsi simkubali Kimaro ni motivational speaker na si mchungaji.
Huyo hamna kitu....yan kuna wajinga humu hata kanisa hawalijui maishani mwao lakini ndio wapo front balaa
 
Mimi nilikua nasali kkkt kila j2.. na nilikua nasali Kariakoo Kimaro akiwepo.

Nilikuja kujua Askofu Malasusa amebadilisha katiba ili awe askofu milele nilichoka sana. Niligundua huyu askofu ni mroho na yupo kikaz sio kiroho nina miaka mitatu sijawahi kanyaga kanisani.

Huyu askofu ana figisu sana na alikua karibu sana na mwenda kuzimu. Kimaro anajituma sana anastahili kuwa juu na hayo matamshi yalikua ni mambo madogo tu ya kurekebishana..

Yule ni binadamu anaeituma sana... just imagine huamka toka Kimara hadi kanisani kwake saa 10 alfajiri kwa ajili ya morning glory
We ni mpumbavu sasa hiyo si ndio kazi yake.
 
Umeongea kweli ila na mimi nijazie

1:-Matamshi yake yalikuw na ukakasi na alikuw ana jikweza

2:-Kujiongelea iman zngne na hii ikawa inaonyesh haamini yeye anachosimamia na alichoagizwa

3:-Ameongoz usharik wa kimara ila nawez sema amelew sifa/umaarufu/Pesa ambako amejeng kiburu na kuto tii mamlaka

Kifup huyu jamaa ni maarufu lakn nazan atakuw anakubalik nawachache hasa wamama na watu ambayo hawawez kujua hayo mapungufu yake ni makubwa mnooo kwa nafas aliyopew na alivumiliw sana

N vyem kam hakuamin ukristo , urutel angejiuzulu na kuanzisha anachoamin yeye kwa aman angepat watu wake
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
 
Umeongea kweli ila na mimi nijazie

1:-Matamshi yake yalikuw na ukakasi na alikuw ana jikweza

2:-Kujiongelea iman zngne na hii ikawa inaonyesh haamini yeye anachosimamia na alichoagizwa

3:-Ameongoz usharik wa kimara ila nawez sema amelew sifa/umaarufu/Pesa ambako amejeng kiburu na kuto tii mamlaka

Kifup huyu jamaa ni maarufu lakn nazan atakuw anakubalik nawachache hasa wamama na watu ambayo hawawez kujua hayo mapungufu yake ni makubwa mnooo kwa nafas aliyopew na alivumiliw sana

N vyem kam hakuamin ukristo , urutel angejiuzulu na kuanzisha anachoamin yeye kwa aman angepat watu wake
Kweli umeongea kitu kizuri sana,
 
Back
Top Bottom