Kuna mambo mengi kwenye hili swala na likichukuliwa positive linaweza kuleta manufaa leo na kesho, mambo kama ya:-
1. Spiritual formation programs za wachungaji wa kkkt zikoje, je Kuna haja ya kuziboresha, kuzihuisha, kuzibadilisha kulingana na wakati au kuendelea nazo kama zilivyo kwamba hazina shida.
2. Pre-clerical criteria zikoje, nani anatakiwa kuingia kwenye mfumo wa uchungaji, sifa zake ni zipi, historia yake, malezi na familia anayotoka iweje, elimu nk.
3. Carrier development zikoje, baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa na kuwa wachungaji, je wanaendelezwaje, wanapewa elimu zaidi, semina, warsha nk. Kuendana na wakati au alichokisoma miaka ile ndo hichohicho?
4. Masuala ya spiritual direction yamekaaje, je wanao walezi wa kiroho ambao wakipata changamoto zozote wanawafuata na kuwaeleza waziwazi kwa uhuru bila kuhofia mamlaka zao za kinidhamu? Je, spiritual directors wao kama wapo, wanazo sifa stahiki, wanapatikanaje? Kama hawapo, je si wakati mwafaka wa kuwa nao?
5. Umoja wa wachungaji ndani ya dayosisi upo? Uko imara? Huru? Wana uongozi wao wenyewe? Viongozi wa umoja wanapatikanaje, wanasaidiana vipi kabla mambo hayajafika kwa baba askofu? Upendo upo kati yao?
6. Mamlaka za kanisa zinathibiti vp wachungaji wao, sheria, katiba, busara ya kichungaji vipoje? Mamlaka ina mamlaka juu yake Ili isionee wanyonge na kuwaogopa wenye nguvu? Hapa namaanisha mfumo mzima wa uongozi wa kanisa juu mpaka chini. Mnyororo wa utii kwa mamlaka ukoje? Unafuata taratibu za kanisa au unategemea na uongozi uliopo? Adhabu, maonyo, makaripio, pongezi, vinatolewaje? Utunzaji wa Siri za kanisa je? Nani anatakiwa kusema nini kwa wakati gani na wapi.
7. Wachungaji wa kkkt wanalipwa mshahara na posho mbalimbali, vipi hizo stahiki zao wanazipata kwa wakati? Zinakidhi mahitaji, zinaboreshwa, mgawanyo wa keki ya kanisa uko sawa, anayehisi kaonewa anapata fursa ya kusikilizwa, asiyeweza kujisemea je?
Hayo na mengine mengi yakiangaliwa kwa mapana, unaweza kujikuta akina Kimaro wako wengi na ni zao la mfumo Wala sio wa kulaumiwa Bali kusikilizwa, kusaidiwa na kutumiwa kama SoMo la kujifunzia.
Ni Mimi baba wa watoto watatu, mume wa mke mmoja tu na mtumishi wa umma, Munywani.