Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Lini litakuwa safi?!! Unaweza kumtumikia Mungu na mali?!!
 
Usijidanganye wewe, hakuna kitu rahisi kuanzisha kama kanisa, tena kwa mtu kama Mch Kimaro akiamua akakohoa tu kho, Kanisa tiyar.
Huo ugumu unaosema sijui unamaanisha ni ugumu wa kuliandikisha au wa waumini??!!!
Anza w
Usijidanganye wewe, hakuna kitu rahisi kuanzisha kama kanisa, tena kwa mtu kama Mch Kimaro akiamua akakohoa tu kho, Kanisa tiyar.
Huo ugumu unaosema sijui unamaanisha ni ugumu wa kuliandikisha au wa waumini??!!!
Anzisha wewe kama rahisi
 
Mwambieni aanzishe kwani ye hapendi sddaka
Hata bila kuanzisha kwan sadaka anakosa?
Yaan mnawazA sadaka tu kwan mliambiwa kanisa ni mahala pa uchuuzi? Mpaka mliungana na mwendakuzimu ili mpige pesa!! kama shida yenu pesa Si mkauze nyanya huko kariakoo shimoni!!
 
Inaonekana katoliki walikulawiti unaonaje ukifungua mashitaka?
 
Usijidanganye wewe, hakuna kitu rahisi kuanzisha kama kanisa, tena kwa mtu kama Mch Kimaro akiamua akakohoa tu kho, Kanisa tiyar.
Huo ugumu unaosema sijui unamaanisha ni ugumu wa kuliandikisha au wa waumini??!!!



Mwambie huyo aisee!

Tena waumini wanasubiri atulie na kuisikilizia sauti na ridhaa ya Roho Mtakatifu akisema aanzishe huduma Au kanisa waumini watajitolea harambee na kukodi ukumbi au watu watatoa Kama kwa Bwana mahali temporary pa kuabudu hadi mipango ya badae.
 
Kama hawajamtendea kwa haki na Kweli basi Mungu atawafedhehesha vibaya sana Watesi, maadui, wanafiki, wachawi wanaofurahia hali yake ya sasa anayopitia.
 

Minamshauri kwa muda huu ni muda wake mzuri kujichimbie mahali kwa maombi, aseme na Mungu na awe mnyenyekevu sana wakati huu.

Akikurupuka kwa kiburi cha huduma yake kubwa ataharibu kila kitu.
Kazi ya Mungu ya kweli ina vita sana.
Akishinda jaribu hii atainuliwa sana
 

Ushauri mzuri sana huu
 
Kuna mambo mengi kwenye hili swala na likichukuliwa positive linaweza kuleta manufaa leo na kesho, mambo kama ya:-

1. Spiritual formation programs za wachungaji wa kkkt zikoje, je Kuna haja ya kuziboresha, kuzihuisha, kuzibadilisha kulingana na wakati au kuendelea nazo kama zilivyo kwamba hazina shida.

2. Pre-clerical criteria zikoje, nani anatakiwa kuingia kwenye mfumo wa uchungaji, sifa zake ni zipi, historia yake, malezi na familia anayotoka iweje, elimu nk.

3. Carrier development zikoje, baada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa na kuwa wachungaji, je wanaendelezwaje, wanapewa elimu zaidi, semina, warsha nk. Kuendana na wakati au alichokisoma miaka ile ndo hichohicho?

4. Masuala ya spiritual direction yamekaaje, je wanao walezi wa kiroho ambao wakipata changamoto zozote wanawafuata na kuwaeleza waziwazi kwa uhuru bila kuhofia mamlaka zao za kinidhamu? Je, spiritual directors wao kama wapo, wanazo sifa stahiki, wanapatikanaje? Kama hawapo, je si wakati mwafaka wa kuwa nao?

5. Umoja wa wachungaji ndani ya dayosisi upo? Uko imara? Huru? Wana uongozi wao wenyewe? Viongozi wa umoja wanapatikanaje, wanasaidiana vipi kabla mambo hayajafika kwa baba askofu? Upendo upo kati yao?

6. Mamlaka za kanisa zinathibiti vp wachungaji wao, sheria, katiba, busara ya kichungaji vipoje? Mamlaka ina mamlaka juu yake Ili isionee wanyonge na kuwaogopa wenye nguvu? Hapa namaanisha mfumo mzima wa uongozi wa kanisa juu mpaka chini. Mnyororo wa utii kwa mamlaka ukoje? Unafuata taratibu za kanisa au unategemea na uongozi uliopo? Adhabu, maonyo, makaripio, pongezi, vinatolewaje? Utunzaji wa Siri za kanisa je? Nani anatakiwa kusema nini kwa wakati gani na wapi.

7. Wachungaji wa kkkt wanalipwa mshahara na posho mbalimbali, vipi hizo stahiki zao wanazipata kwa wakati? Zinakidhi mahitaji, zinaboreshwa, mgawanyo wa keki ya kanisa uko sawa, anayehisi kaonewa anapata fursa ya kusikilizwa, asiyeweza kujisemea je?

Hayo na mengine mengi yakiangaliwa kwa mapana, unaweza kujikuta akina Kimaro wako wengi na ni zao la mfumo Wala sio wa kulaumiwa Bali kusikilizwa, kusaidiwa na kutumiwa kama SoMo la kujifunzia.

Ni Mimi baba wa watoto watatu, mume wa mke mmoja tu na mtumishi wa umma, Munywani.
 
Tushawahi pata mchungani KKKT hivyo hivyo kanisa linajengaa jengo jipya la kusalia mchungaji nae anajenga nyumba yake mahalii[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kanisa halijawahi kuisha yani kama vilehatutoi hela za ujenzi wakati Arambee kila jumapilii aisee waumini walimsnitch mchungaji huko dayosisi mpaka wakaamua aamishwe jamaa kuliko kuhama akaona bora aache uchungaji[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Sijui nataka kusema nin ila Penye maslahi na pesa hapakosi majungu na fitina kama Kimaro ni mchungaji wa kweli akubali na kutii alichoambiwa na Viongozi wa kanisaa.
 
Kwa taarifa yako tu, Kimaro sasa hazungumzii habari za nyumba, mashamba wala Vacation abroad
1. Ana Mjengo wa maana huko TEGETA (ambako unaweza kupokea Wachungaji yapata 10 kwa mpigo);
2. Amesomesha watoto yatima zaidi ya 100 mpaka kufikia level za Vyuo Vikuu (baadhi wamehitimu Master degree);
3. Kwenda Nje ya nchi ni kitu cha kawaida kwake hata majuzi katoka huko akiwa na wazee wa kanisa na baadhi ya waumini (tiketi alilipiwa na waumini nje ya nchi)
 
Hiyo kesi nimesema sio kwamba kimaro anakula sadakaa nimesema kuonesha Uongozi wa kanisa una nguvu hata kama hao waumini wataandamana..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…