Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Washirikina combine.
Yule apingaye roho wa Bwana ataangamia tu.
 
Eti ukifa hatukuziki. Sasa mimi hata mnizike msinizike inanisaidia nini? Si nimeshakufa? Dini zingine ni vituko tupu yaani [emoji706][emoji706][emoji706]

Kwanza hakunaga mfi anaekosa mzishi.

Waache kutumia kuzika kama fimbo ya kutishia watu kulazimisha kwenda kusali jumuia.

Watu wenyewe wako mwilini na matendo ya mwili yamewatawala na hawapo tayari kutahiriwa na Neno mioyo yao wapate kuwa viumbe vipya.
 
Umeandika Ukweli Mtupu na umeeleweka.

Eliona Kimaro ameshajiinua sana na hana UTII

Anajipa mamlaka makubwa na kudharau wengine
 
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa...
Ubarikiwe sana kwa kueleza ukweli.

Ukweli unauma lakini ukweli hutibu.

Kimaro kama ana masikio na asikie sasa.

Karama tupewazo na Mungu zilitolewa bure, na zitumike bure kwa utukufu wa Mungu
 
Tii mamlaka, tii mamlaka, fuata miongozo Kama unataka miongozo yako fungua kanisa lako sikio halizidi kichwa kamwe
Hapa Umemaliza kila kitu.

Mfumo ndio unaombadilisha Mtu, Mtu habadilishi Mfumo

Kimaro aliikuta KKKT na misingi pamoja na taratibu zake

Kama hawezi au hataki hizo tamaduni basi akaanzishe kanisa lake
 
Mordenize ❌
Modernize✅
 
Umeongea jambo la msingi. Kimaro alianza kuwa na kiburi, ujivuni na kudhani yeye tayari ni mkuu na haambiliki. Shida ipo hapa.
 
Nadhani KKKT kuna shida kuanzia waumini wao tangu wakiwa watoto.
Hivi inakuaje mchungaji anayefanya mambo kinyume na miongozo ya taasisi yake iliyomuweka ndio anapendwa na kupata umaarufu? Kwanini waumini wenyewe wasimkatae?
Tatizo waumini siku hizi hawamfuati YESHUA wanamfuata mchungaji..... Si umeona mabango yameandikwa "daddy kimaro" [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…