Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Lutheran kuna shida sehemu nyingi, mchungaji akionekana yuko karibu na anakubalika na waumini anahamishwa.
Hapana, lazima kutakuwa na shida sehemu.

Lutherani mnao wachungaji wengi tu ambao ni wazuri mno. Ingekuwa wachungaji wazuri ndiyo wanakuwa targeted, hata hao wengine nao vile vile wangekuwa wana matatizo. You have the best, ila hamjijui!
 
Kimaro huenda ni Kama Tunfu Lissu.
Ukiwa na akili sana nayo ni shida.

Unakuta kabia Mchungaji Kimaro anaona umehubiri Utumbo na uongo ndani yake. Sasa akija kujazilizia anaonekana anakosa adabu[emoji1787][emoji1787]
Hata mchungaji mastai nae akija mchungaji mwingine kuhubiri bas akimaliza mastai ataanza upiyaa kbsa na Wala hapiti kule uliko pita wee wa mwanzo [emoji23][emoji23][emoji23] masege anampata Sana mastai

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ingekua ni mimi na uzinzi wangu basi kanisa lingenitenga na kunisimamisha huduma lakini cha ajabu kanisa ndio limekua likiwalimda na kuwatetea mapadri na maaskofu wanaolawiti watoto hivyo ni mkakati wa kanisa kuhakikisha wanalawiti watoto na kisha kulindana.

Papa mwenyewe amekiri kwamba aliwalinda na kuwatetea maaskofu waliokua wanatuhumiwa kulawiti watoto.
Bwana wetu Yesu alikuwa karibu na wale ambao jamii iliwaona waovu kuliko wale ambao jamii iliwaona watakatifu. Sasa wewe ulivyo punguani unahimiza kanisa liwatenge wale wanaotenda dhambi.
 
kwenye Biblia yako ya MAKABAYO,ila kwa sisi tunaosoma vitabu 66 , lipo:
wewe hapo umevaa sketi ya mtumba ambayo wazungu wametoa fungu la kumi, umevaa pedi ambapo ni msaada wenzio wametoa fungu la kumi, leo asubuhi umefanya tendo la ndoa[morning glory] na mume wako kwa kutumia Durex condom toka marekani ambapo ni fungu la kumi la wazungu kwa nchi maskini, acha mkono na roho korosho, lipa zaka.
Hizo ni Kodi za wamarekani sio fungu LA 10
 
Kufuatia semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT Kijitonyama ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo...
Duh
Mnamuondoa Eliyona mnamleta Anna?
1 Timotheo 2:12
[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
But I suffer not a woman to teach, nor to usurp authority over the man, but to be in silence.
Ikiwa ya kwamba mnalisaliti neno ambalo kwalo mnajihalalisha kusimamia wengine mtashindwa nini kulana wenyewe kwa wenyewe?

Kkkt kwa kiasi kikubwa inaendeshwa kama chama cha siasa.

Fitina nyingi, uchawa mwingi na hata ushirikina mwingi hasa kwenye uchaguzi.

Hiyo Dayosisi ya mashariki na Pwana ina vita vya mda mrefu kati yake na watu wa ukanda wa kaskazini uliochagiza hata askofu wake Malasusa kuungana na Magu katika mkakati wa kuwademolish hawa watu.
Kuna mch mmoja huko kutoka kanda ya kaskazini aliyekuwa mkuu wa jimbo kwa wivu aliondolewa na kupelekwa huko Mwanarumango.

Sasa wakati Kimaro akitendewa haya yule Maksai wa Kimara Korogwe atie maji na baadae aliyekuwa Ubungo Plaza kabla ya kuhamishiwa Mbezi luis ajiandae kwa panga la Alex G.
 
Mngejua watu jinsi wanavyomtukuza Mungu Kwa uamsho Mkuu ulokuwa Unaendelea huko KKKT msingelifanya hayo ya uharibifu kwenye kazi ya Mungu.

Hamtaki advancements? Mnataka ukristo wa kupoa ambao mnaenenda kama wasio amini?
Hpn mkuu Sina shida na mahubiri yake nawapenda Sana ila kuamishwa Ni sawa tu wote Ni kondoo hvyo kimaro nae aje huku kongowe kuleta neno Hilo huku

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Na hao wachungaji wawili ndio wanaojaza wahumini kkkt angalau kunaonekana kuna waumini maana wanajua kuenenda na mahitaji ya sasa ya waumini nyie endeleeni kuwakera waumini tu.
Kwahiyo kabla hawajaja duniani Hao walutheri walikuwa hawapo? Mbona manabudu watu. Waambie wakaanzishe makanisa Yao tuone hiyo kkkt ikitetereka
 
Umeongea kama mtoto wa darasa la 2. Mbona wakatoliki wengi huwa wana akili na uelewa? Tumsifu Yesu Kristo ni salamu ambayo mkristo yeyote anaweza itumia. Kuelezea mambo mazuri wanayofanya wengine ni akili ya ku appreciate. Migogoro ipo hata Roman Catholic sema tu wewe ni mtoto huelewi. Unamfaham Father Nkwera? Unawafaham Charismatic? Kila Taasisi ina taratibu zake. Ziheshimiwe.
Hapo kwenye charismatic umepuyanga bwana mdogo, ila kwa yule padre wa Riverside umepatia, japo nao ni mgogoro wa kipumbavu na ni wa kimafundisho zaidi , sio wa kiuchumi kama ilivyo huko kwingine.
 
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Kwa jinsi ulivyotoa hili wasilishon lako yaonyesha una chuki binafsi na Mch Kimaro
 
Askofu Dr Alex ghae malasusa ndiye kiongozi wa dayosi hyo ya mashariki na pwani DMP ....hvyo katk hili Kuna Jambo ameliona kwa muda na kwamba hajakubalina nalo kwa utaratibu wa dr kimaro

Hvyo Kama wahumuni na kkkt kijitonyama mnaona hakubalini na hili Ni vyema atafutwe askofo malasusa au msemaji wa dmp kulisemeha hili

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ila kkkt kuna shida nyingi sana hawajaweka utaratibu mzur ni nadra sana kuona mapadri wanagombana au wanatoa siri za kundi mbele ya waumini
 
Mimi pia ni msharika wa KKKT kijitonyama.

Yaliyo chini ya PAZIA ni Mengi mno.

1. Kimaro aliota mapembe.

2. KKKT hatukuwa na utaratibu wa mchungaji kukaa USHARIKA mmoja zaidi ya miaka Mitano.

3. Sikio lilitaka kuzidi Kichwa.
Yani alianza kujiona yeye ni mkubwa mno, anafaa kuwa Askofu, Mapinduzi ya Malasusa nk.

4.Kwa Alex Atasubiri sana.
Hata hivyo wamemvumilia mno kimaro.

5.kutofuata utaratibu wa kalenda.
Nyimbo,

Alikuwa na fujo nyingi sana

Stola za beighali.
Haya kama mambo ya CCM Tena??
 
Mimi pia ni msharika wa KKKT kijitonyama.

Yaliyo chini ya PAZIA ni Mengi mno.

1. Kimaro aliota mapembe.

2. KKKT hatukuwa na utaratibu wa mchungaji kukaa USHARIKA mmoja zaidi ya miaka Mitano.

3. Sikio lilitaka kuzidi Kichwa.
Yani alianza kujiona yeye ni mkubwa mno, anafaa kuwa Askofu, Mapinduzi ya Malasusa nk.

4.Kwa Alex Atasubiri sana.
Hata hivyo wamemvumilia mno kimaro.

5.kutofuata utaratibu wa kalenda.
Nyimbo,

Alikuwa na fujo nyingi sana

Stola za beighali.

Inaelekea waumini mlikuwa hamumpendi sema mnacheka nae kinafiki
 
Inaonekana mkuu na wewe ni mmoja wa wanaomfanyia figisu huyo mchungaji, eti unamuombea arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu, kwahiyo ina maana yeye kazi anayoifanya ni kumtukuza shetani...!
Kweli kabisa
 
Kwa jina alilotengeneza nadhani ni muda sasa wa kufungua kanisa lake ajipigie pesa wa wajinga wajinga wanaomshobokea.
 
Back
Top Bottom