Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Waumini fulani wameamua tutafute ukumbi mahala mkuubwaa mahala panapofikika tutalipa wenyewe Kwa harambee au mmoja mmoja kwa siri.

Mchungaji Kimaro popote ulipo ujue Mungu anataka kukuinua pakubwa sana.

Be encouraged @ Pastor.

Mchawi hasa akiwa mwanamke ni mtu mbaya sana!
Ulipaswa uandike 'be courageous'
 
Labda ni ile kauli yake ya kuwa Wakristo wengi si waaminifu na ni wezi. Ile kauli wengi tulikubaliana nayo ila lazima ingemletea shida.

Kuhusu Upendo TV, mimi nilichangia katika uanzishwaji wa ile TV kupitia kampeni aliyokuwa anafanya kwenye kipindi chake cha asubuhi kwenye Upendo Radio kwa hiyo kama walikuja kumuondolea kipindi chake lazima imguse. Alitumia nguvu kubwa na ushawishi wake kukusanya michango.

Mchungaji Eliona Kimaro Yuko Vizuri
 
Huyo

Huyo mchungaji alizaliwa Kwa ajili ya kufanya Kazi hapo kimara pekee?? Anatolewa tu, na mikia yenu ya kichaga itakamata makalio tu
Du ukabila tena, mbona huajawazungumzia Mchungaji Kombo na wengine ambao sio wachaga? Mchungaji wa kimara sio mchaga sasa uchaga unatoka wapi. Askofu wao Malasusa Mnyakyusa wapi mzee unakoelekea??? Mbona unaleta tena chuki za kisiasa/kikabila kanisani?
 
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
Sijaona point yeyote ya maana iliyosababisha asimamishwe,kumbe alizuiwa kwa hila asihubiri upendo tv mkatukosesha huduma tuliyokuwa tunahubiriwa majumbani basi Mungu wetu halali atamlipia tu,sidhani kama ni kweli mchungaji anaweza kuacha kuhubiri kwa kufuata kalenda ibada zote,hii hutokea kwa ibada chache na ni kawaida kwa wachungaji wengi tu.
 
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
Maelezo mazuri sana,kama anakiuka viapo anapaswa kushughulikiwa na kama anaona ni mkubwa kuliko taasisi basi ni vema akaanzisha kanisa lake,ili achunge kondoo wake nje ya Mfumo wa KKKT.Kanisa linabebwa na Kristo sio mtu au kiongozi mmoja.
 
Huyo

Huyo mchungaji alizaliwa Kwa ajili ya kufanya Kazi hapo kimara pekee?? Anatolewa tu, na mikia yenu ya kichaga itakamata makalio tu
Hata huelewi Rev. Kimaro alikuwa mchungji wa Kijitonyama, wewe unazungumzia Kimara mbona unaongozwa na chuki za kikabila????
 
Sijaona point yeyote ya maana iliyosababisha asimamishwe,kumbe azuiwa kwa hila asihubiri upendo tv mkatukosha huduma tuliokuwa tunahubiriwa majumbani basi Mungu wetu halali atamlipia tu,sidhani kama ni kweli mchungaji anaweza kuacha kuhubiri kwa kufuata kalenda ibada zote,hii hutokea kwa ibada chache na ni kawaida kwa wachungaji wengi tu.
Naweza kuubaliana na wewe kwani mimi sisali kanisa hilo, ila amekubali amri ya kanisa na kukaa kando kwa siku 60, kusubiri hatua zaidi za askofu wake na wakuu wake. Angeongea kupinga hayo ningeona shida wazi wazi ya utovu wa nidhamu. Tuache tuone kwani lipo mikononi mwa vongozi wake.
 
Judgment is spiritual more than professional as you may see, let the leadership of the church take their spiritual role to resolve this.
 
Kwenye hili nahisi pastor Kimaro ataenda kujitafakari.

Mimi ni muumini wa KKKT hapo Kijitonyama, shida iliyokuwepo kwa mchungaji Kimaro ni kwamba alikuwa anaenda kinyume na utaratibu wa kanisa na kibaya zaidi alishaonywa zaidi ya mara 3 ila shida yake akiitwa akaonywa anakuja kanisani anaanza kuongea kwa waamini na kurusha vijembe kwa viongozi wake.

Tarehe 8 ukiweza fatilia alichokifanya kwa pastor mwenzake ANNA maneno aliyoongea kumuhusu huyo mchungaji kuna jambo utaelewa.

Kimaro ana kiburi cha umaarufu. Mchungaji hafati kalenda ya kanisa, yeye anafanya mambo yake, aliitwa akaonywa ila akaja kanisani hadharani na kusema hawezi kupangiwa cha kufanya ila Mungu tu, sasa hapo kweli kuna utii?

Kimaro toka amekuja usharikani anazo nyimbo 6 tu anazoimba kutoka kitabu cha tumwabudu Mungu wetu, aliitwa akaambiwa hiki kitu ila akawa mkaidi, ni mchungaji anayependa yeye aongee zaidi, hapendi kuwapa wachungaji wengine nafasi ya kuhubiri, ikitokea mchungaji mwingine akahubiri basi na yeye baada ya mahubiri atasimama na kuanza kujazilishia kuonekana kwamba mwenzake hajafanya kama inavyopaswa.

Ni kimaro na masai wa kimara ambao ukifatilia utaratibu wanao ufanya kanisani siyo wa KKKT ila najua wachache sana wataelewa hili.

Kama mtaweza kumbuka pia aliondolewa kwenye vipindi vya upendo Tv kisa mambo yake hayo ya kufanya kinyume na utaratibu wa kanisa ikabidi wamuonye ila akakaidi, baada ya kuondolewa alikuja kanisani hadharani na kuanza kusimanga na kuongea mbovu na tokea hapo hajawahi kutangaza kitu chochote kinacho husu upendo kama magazeti.

Alitamba sana kwamba kwa jinsi alivyo barikiwa na Mungu hakuna mwanadamu wa kumshusha hapo alipo, na haya alikua anaongea kanisani mbele ya waamini na kujitapa kabisa.

Kwa sisi waamini wachache ambao tulikua tunamuona kanisani na kutambua madhaifu yake tulijua hana mda mrefu atapigwa chini na kweli leo kaondoka.

Wengi mnaongea hamjui kilicho nyuma ya huyu kimaro ila nakuhakikishia KKKT KIJITONYAMA haiwezi kutetereka kisa kimaro kuondolewa na alishasema akitolewa Kjitonyama basi ataanzisha kanisa lake, ngoja nione atakachofanya baada ya hili.

Namuombea hekima na maarifa atambue kosa lake arudi kundini na awe mnyenyekevu kwa Mungu na Viongozi na Kanisa kwa ujumla.

ANAYEFATA NI MASAI WA KIMARA MWISHO.
KANISA NI MALI YA MUNGU, sio saccos za KKKT. Mungu huabudiwa kwa roho, na kanisa halisi la Mungu lazima litoe solutions za matatizo ya waumini wake through maombi, na mafundisho yenye uzima. Zama za kufuatisha liturugia mpaka watu wanasinzia zimekwisha. Nawaunga mkono hawa pastors Kimaro na mastai at least wameleta uhai kwenye ibada za KKKT.
Kama kweli wanafanya hayo kwa ajili ya Kristo, hata wakiwatimua halafu wakaamua kuwa na huduma zao still watapata followers wa kutosha.
 
Ila kkkt mmezidi. Mpunguze migogoro. Jifunzeni kutoleta mambo yenu mitandaoni.
Kwetu huwezi kusikia mambo yanaletwa hadharani kiasi hiki.
Sio kwamba hayapo yanakuwepo maana popote walipokusanyika watu lazima migogoro iwepo.
Huwezi kuzuia mambo kuletwa mitandaoni,hata serikali na vyombo vyake inapambana na hilo Ila imeshindwa,ukiangalia aliyeleta mitandaoni ni huyohuyo Kimaro,na hata asingeleta yeye,bado waumini aliowaeleza hayo wangeleta tu,hizi ni zama za uwazi kikubwa ni taratibu tu zifuatwe na haki itendeke.

Kama wanasema alikuwa na semina anaendesha unadhani angeondoka kimyakimya baada ya barua si ndio ingeleta taharuki zaidi?watu wangeanza kuulizana mbona hayupo.
 
Duuh kazi ipoo sema Ulimi ukiutumia vibayaa nao unashidaa sanaaa.

Huo huo unahubiri dini leo huo huo kesho unaponda dini yako na watu wake wanaoiamini na kufata mafundisho unayowafundisha sasa sijui kipi ni kipi...!!

Anyway kuusifu uislamu na Ukatoliki ni kuonesha kkkt inazingua na hufurahii kuwa hapoo.
 
Kuna kanisa lisilokataza dhambi?? Kama lipo hilo sio kanisa la Kristo bali wanajua wenyewe ni kitu gani. Hata Yesu alionya juu ya dhambi na kufa msalabani ili tutapoanguka turudi kwake kwa toba. Huyo asiyekataza hana ushirika na KRISTO.
Mavazi wanavaa uchi makanisani
 
Huwezi kuzuia mambo kuletwa mitandaoni,hata serikali na vyombo vyake inapambana na hilo Ila imeshindwa,ukiangalia aliyeleta mitandaoni ni huyohuyo Kimaro,na hata asingeleta yeye,bado waumini aliowaeleza hayo wangeleta tu,hizi ni zama za uwazi kikubwa ni taratibu tu zifuatwe na haki itendeke.

Kama wanasema alikuwa na semina anaendesha unadhani angeondoka kimyakimya baada ya barua si ndio ingeleta taharuki zaidi?watu wangeanza kuulizana mbona hayupo.
Kwani si kaenda likizoo...!! Mchungaji kupewa likizo jambo la kawaida sema yeye ndo kayakuzaaa kuonesha kuwa kaonewaaa... aina ya wachungaji ambao usharika ukikuaa na wao ndo wameweka nguvu kuukuza huwa wana changamoto sana za kuongozaaa wao wako mbele sana kukemea ila ukweli na wao ni wachafu vile vile.
 
Back
Top Bottom